Wednesday, June 30, 2010
Muda wa usajili line waongezwa
SERIKALI imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani ili kuwezesha wananchi wengi waweze kujisajili baada ` kusikiliza kilio chao ili kuwapa fursa zaidi ya kujisajili.
Hayo yalisemwa jana Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msollla wakati akiwasilisha hotuba yake ya makadrio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo.
“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu imesikia kilio cha wananchi wengi. Imeongeza muda wa usajili wa simu za viganjani hadi Julai 15, mwaka huu baada ya hapo simu zote ambazo hazijasajiliwa zitafungwa,” alisema Profesa Msolla .
Aidha Waziri Msolla alisema jumla ya kampuni 14 hadi sasa zimepewa leseni ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu.
Aliongeza kuwa idadi ya watumiaji wa simu kwa kigezo cha njia za simu (line) zinazotumika imefikia 18,207,390, hivyo idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na watumiaji 3,542,563 waliokuwepo mwaka 2005.
Alisema idadi ya simu za mezani hadi sasa ni 174,800 ilinganishwa na 154,420 zilizokuwepo mwaka 2005.
“Hii ni sawa na ongezeko la la asilimia 13.2 . ukuaji huu umepanua wigo wa mawasiliano ya simu na kuongeza huduma nyingine zinazoendana na matumizi ya simu hapa nchini
Alizitaja huduma hizo kuwa ni upatikanaji wa taarifa, huduma za mtandao, ulipaji wa Ankara za simu, maji, umeme na huduma za kibenki.
Awali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1, mwaka 2009 hadi Desemba 31, mwaka 2009.
Awali mamlaka hiyo iliongeza muda wa mara ya pili wa miezi sita wa kusajili simu hizo, kuanzia Januari mwaka 2010 hadi Juni mwaka huu baada ule wa kwanza kuonyesha watu wengi walikuwa hajajisajili. SOURCE: BUNGE.
Usajili wa line za simu mwisho leo
WATU wakiwa katika kibanda cha usajili wa namba za simu za mkononi. Zoezi hilo bado linaendelea Jijini Dar es Salaam. Picha na Amran Mnjagila.
*********************************************
Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitaongeza muda wa kusajili laini za simu za mkononi na kwamba namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungiwa kupiga, kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi (SMS).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema baada ya saa sita usiku ya Juni 30 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungwa kupiga, kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi kwa siku 90 hadi Septemba 30 mwaka huu.
“Katika kipindi hiki cha siku 90 endapo mtumiaji atasajili namba yake itafungwa na kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo Septemba 30 zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao kabisa,” alisema Nkoma
Alisema Mamlaka hiyo imekubaliana na makampuni ya simu kufanya uhakiki wa usajiliwa laini za simu za wateja kwa kutumia namba 106 kupitia simu za mkononi na kwa wateja wa mitandao iliyoko katika mifumo ya GSM, wateja wanatakiwa kuingiza *106# , wateja wa mfumo wa CDMA watatakiwa kupiga namba hiyo na watapokea taarifa za usajili.
“Hivi karibuni muswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ulipitishwa na Bunge kwa sheria , sheria hiyo inafanya usajili wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa sheria hiyo, kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai. Adhabu ni faini na kifungo au vyote kwa pamoja,” alisema Nkoma.
Mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka jana mamlaka hiyo ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma ya mawasiliano, kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiao huduma mbalimbali, kuimarisha usalama wan chi na nk.
Wakizungumza mara baada ya tamko hilo la mkurugenzi wa TCRA, viongozi wa kampuni za simu za mikononi za TTCL, Zain, Tigo, Vodacom, Sasatel, BOL, kwa nyakati tofauti waliilalamikia hatua hiyo ya serikali wakisema kwamba iatawasababishia usumbufu wateja wao na kuwapa hasara kubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Zain Tanzania, Khaled Mehtadi alisema wanakubaliana na mpango huo wa serikali, lakini wanaomba uongezwe muda kwa kuwa kazi ya kukusanya data kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ni kubwa na haiwezi kumalizika haraka kutokana na wateja wengi kujitokeza dakika za mwisho.
"Pia alisema kuwa iwapo serikali itaendelea kung'ang'ania uamuzi wake wa kufungia laini basi kampuni hiyo itapata hasara ya kadri ya asilimia 25 kwa kuwa wamewekeza fedha nyingi kulipa mawakala zaidi ya 50,000 nchi nzima na bado kazi haijamalizika,"alisema.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya simu za mikononi ya TTCL, Ernest Nangi alisema kuwa kama walivyo waendeshaji wa kampuni zingine za simu wanaona kuwa bado wanahitaji muda kuweza kukabili changamoto hiyo.
Kwa upande wa kampuni za Tigo kupitia Meneja wa Huduma kwa Wateja, Harieth Rwakatare na Vodacom kupitia Mkurugenzi wake Francois Swart walisema kuwa zoezi hilo ni gumu na kwa maana hiyo wakaitaka serikali na wateja wao kuwa wavumilivu ili waweze kulikamilisha kama inavyopaswa. SOURCE: TCRA
Tuesday, June 29, 2010
Marubani wa JWTZ wafa ajalini
WANAJESHI wawili ambao ni marubani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kambi ya Ngerengere mkoani hapa, wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuligonga gari la watalii na kupinduka.Ndege hiyo ya Jeshi ambayo inatumika katika mafunzo ya kijeshi, jana ilitua barabarani na kusababisha ajali iliyoua marubani wawili wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) baada ya kugongana na lori lililokuwa limebeba watalii.
Ndege hiyo ndogo yenye namba F59119 iligongana na gari hilo eneo maarufu kwa jina la Zimbabwe lililo Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata wilayani Handeni.
Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo ya nadra sana kutokea walieleza kuwa waliiona ndege hiyo ikishuka kabla ya kutua katikati ya barabara na baadaye kujaribu kuruka tena, kitu kinachoonyesha kuwa rubani alikuwa katika harakati za kuinusuru.
Walisema, hata hivyo, ndege hiyo ilishindwa kuruka juu na kuserereka barabarani.
Walisema wakati ikiyumba, ndege hiyo nusura iligonge basi la kampuni ya Simba Mtoto lililokuwa likitokea jijini Tanga kuelekea Dodoma.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Jafari Mohammedi ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio hilo, aliwataja waliokufa kuwa ni rubani wa ndege hiyo Meja Kathbet Leguna (41) na mwanafunzi wake Luteni Andrew Yohana Kijangwa (31).
Mmoja wa wafanyakazi wa gari hiyo iliyogongana na ndege hiyo Solomon Talalai alisema ndani walikuwepo watu 24 ambao 19 kati yao ni raia kutoka Uholanzi, wanne kutoka Kenya na mmoja Mtanzania. Imeandikwa na Hussein Semdoe na Burhani Yakub, Handeni:SOURCE:MWANANCHI
Friday, June 25, 2010
Waziri Mkuu akutana na vijana wa Dodoma
Thursday, June 24, 2010
Jaji Mkuu aapisha mawakili 128
Mke wa Rais Mama salma Kikwete, akimpongeza mwanae, Ridhiwani Kikwete, kwa kumpa shada la maua baada ya kutunukiwa Cheti cha kuwa Wakili wa kujitegemea, wakati wa hafla ya kuwatunuku mawakili 128, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Jaji mkuu wa Tanzania Mh.Augustino Ramadhan leo amekabidhi hati za uwakili kwa mawakili 128 katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam
Katika tukio hilo lililofanyika mapema leo tarehe 24 ambapo Mwenyekiti wa WAMA na mke mheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete amehudhuria na kushuhudia zoezi zima la kupatiwa kwa hati mawakili hao.
Aidha katika zoezi hilo limeonesha kuwa ni la kufurahisha kwa familia ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mtoto wake ambaye sasa ni wakili Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete kuwa miongoni mwa mawakili waliotunukiwa hati hizo leo.
Katika sherehe hizo pia mawakili wa kujitegemea walifika kushuhudia tukio hilo ambapo walifurahishwa sana na wenzano kutokana na uvumilivu waliokuwa nao hata kufikia hatua ya kupata hati ya kuwa Wakili.
Pia wamewataka mawakili hao kutumia vizuri heshima waliyopewa ili kuepukana na kinachoisumbua serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania(Utumiaji mbovu wa madaraka na kutokutenda haki)kitendo ambacho kinaitesa jamii nzima ya Watanzania.
Wednesday, June 23, 2010
Kinara wa mihadarati akamatwa Jamaica
Christopher Dudus jambazi sugu wa mihadarati Jamaica
Polisi nchini Jamaica wamemkamata kiongozi sugu wa biashara za mihadarati nchini humo Christopher Dudus Coke viungani mwa mji mkuu, Kingston.
Bwana Coke ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu, anatakiwa nchini Marekani kwa mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na biashara haramu za silaha.
Juhudi za kumkamata Coke mwezi jana zilisabisha vurugu nchini humo ambapo watu zaidi ya sabini waliuawa.
Mkuu wa polisi nchini Jamaica, Owen Ellington, alisema kuwa maafisa wake wa polisi wameonywa dhidi ya kutokea vurugu zingine kufuatia kukamatwa kwa bwana Coke.
Huenda akafikishwa mahakamani katika muda wa masaa arobaini na nane.
Bwana Coke alitajwa kama mmoja wa majambazi sugu zaidi duniani, ingawa wafuasi wake wanasema yeye ni kiongozi wa jamii.
Ajitokeza kumvaa Dk Mwakyembe
Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Kazi Duniani(ILO) Rhoda Mwamunyange (mwenye blauzi ya pinki) akitangaza jana jijini Dar es salaam nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Jimbo hilo hivi sasa liko chini ya mheshimiwa Dkt Harrison Mwakyembe. Wengine kushoto ni Mpambe wa Rhoda na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise. Picha na Tiganya Vincent, Dar es salaam
Tuesday, June 22, 2010
Mhadiri Suza ang'ara kimataifa
MHADHIRI wa chuo cha SUZA, Dk Mohammed Ali Sheikh, anayefundisha somo la kemia, ametajwa kuwa miongoni mwa wanasayansi mia duniani wa mwaka 2010.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam kutoka katika taasisi ya kimataifa ya "Biographical Centre "(IBC),ilieleza kuwa mhadhiri huyo anayefundisha somo hilo ametajwa kuwa miongoni mwa wanasayansi bora duniani.
ilieleza kuwa Kila mwaka taasisi hiyo inatangaza wanasayansi bora 100 ambao wanapatikana duniani, kwa somo la sayansi ambao wanapatikana kwa njia ya utafiti maalumu wa kina.
"IBC inaamini kuwa utafiti huu unalengo la kuwavutia wanasayansi mbalimbali wa mjini, na vijijini hata wa kimataifa kwa bila ya kupendelea jinsia ambao wametoa mchango wa kutosha katika elimu ya sayansi,hivyo Dk Sheikh anavyo vigezo hivyo na sasa ni mwanachama wa IBC," alisema sehemu ya taarifa hiyo.
Sehemu ya taarifa hiyo pia ilisema kuwa Dk Sheikh anaongoza kitengo cha biashara na ushauri wa taaluma katika chuo cha Suza.
Kwa sasa Dk Sheikh amekuwa mwanachama wa wanasayansi mbalimbali wa taaluma na jumuiya ya wanasayansi, ambazo ni pamoja na jumuiya ya Kijapan ya mazingira na kemia, afya na uongozi ya Canada, teknolojia ya majini, iliyopo nchini Canada,Jumuiya ya kimatiafa ya mazingira na uchambuzi wa kemia,umoja wa elimu ya fizikia ya dunia, na elimu ya sayansi ya dunia.
M-NET LAUNCHES SENSATIONAL SEASON 5
The 5TH edition of M-Net’s BIG BROTHER AFRICA will launch just days after the newest World Cup Champions are crowned, and with the golden prize of USD 200 000 once again up for grabs, a breathtaking new game will be well and truly on!
And this time, Big Brother fans in over 40 countries across the continent are going to get a show that’s more edgy, more tactically challenging and more intensely strategic than ever before.
So says M-Net Africa Managing Director Biola Alabi who was delighted to make the news official.
“What a great moment this is – to bring back a show that our audience loves for an incredible 5th time. We wanted season 4 (Big Brother Revolution) to be special but it exceeded our hopes. With the volume of interaction the show received from fans, it was clear that season 5 was definitely on the cards.
So we’ve been developing what we believe will be thrilling new format changes.”
Now, with the news out in the open, M-Net has confirmed that the latest BIG BROTHER AFRICA will begin on July 18, and will be screened live 24/7 for 91 days on DStv Channel 198 for DStv Premium and Compact subscribers.
And breaking with tradition, M-Net has announced it won’t be calling for entries for the new show.
The company has revealed that having run the series 4 times previously, they’re now head-hunting contestants from a database of previous entries submitted for the show.
“We want to invest more broadly in season 5 and having already been introduced to a world of interesting characters from previous searches, there’s limited value in spending extensively in another search for contestants,” says Alabi.
Monday, June 21, 2010
Jk achukua fomu
RAIS Jakaya Kikwete jana alianza rasmi mbio za kutetea nafasi yake ya urais na kueleza kuwa vipaumbele vya serikali yake mpya vitasukumwa na misingi kumi, ikiwemo kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais, Rais Kikwete alisema vita dhidi ya rushwa itaenda sambamba na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria, demokrasia na mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma.
“Nitatumia bidii yangu yote kufanya kampeni ya kukipigania chama chetu kipate ushindi mkubwa na mara tutakapofanikiwa, vipaumbele vya serikali ijayo vitasukumwa na misingi kumi ifuatayo,” alisena Rais Kikwete na kuongeza:
“Kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa na umoja, amani na usalama, Kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea kwa kuchukua hatua madhubuti za kuharakisha zaidi mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda”
Alisema vipaumbele vingine ni kuongeza jitihada na mipango zaidi ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini ili wawezze kushiriki na kunufaika na uchumi wwetu unaokua. Lakini vilevile tutaweka mkazo katiak ulitambua na kuliwezesha kwa namba yak kundi la wajasiriamali wa tabaka la kati ili waweze kushiriki katika uwekezaji mkubwa katika nchi yetu.
Urais Zanzibar Speed 100
WAGOMBEA wanane kutoka chama cha mapinduzi CCM leo wamechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar baada ya rais aliyepo madarakani Amani Abeid Karume kumaliza vipindi vyake viwili vya uongozi kwa mujibu wa katiba.
Takriban wagombea wote wanane wanaotaka kuwania kinyanganyiro hicho wamezungumzia suala la kudumisha amani na kuendeleza maridhiano yaliofikiwa na Rais wa Zanzibar Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. iwapo watapata ridhaa ya wananchi ya kuiongoza Zanzibar.
Wagombea waliochukua fomu leo ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha ambaye alichukua fomu saa 3: 00 asubuhi na kuzungumza na waandishi katika Hoteli ya Bwawani. Ali Karume alichukua fomu saa nne asubuhi, Alli Juma Shamhuna alichukua fomu saa tano, Bakari Mshindo saa sita mchana, Dk Billal akachukua saa nane, Dk Shein saa tisa na Mohammed Aboud saa 10 jioni.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu, Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud alisema Zanzibar hivi sasa iko kwenye mazingira mazuri zaidi kuliko nyakati nyingine zozote katika historia yake.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein aliahidi kuwa atahakikisha Wanzanzibari wanaishi kwa amani na kuendeleza utamaduni wao wa kuvumiliana na kusaidiana.
Akizungumza katika hilo Balozi wa Italia Ali Karume alisema pamoja na kuwa anaunga mkono maridhiano, lakini suala la kura ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya ndio au hapana hawezi kutaja msimamo wake kwa kuwa kura ya maoni itategemea wakati husika.
Waziri Kiongozi Mstaafu Dk Mohammed Gharib Bilal alisema endapo Wazanzibari watampa ridhaa ya kuongoza ataendesha nchi kwa misingi ya utawala wa sheria huku akisisitiza suala la nidhamu katika utawala wake.
Kamishna wa Elimu na Utamaduni, Hamad Bakari Mshindo alisema kwamba Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendeleo ikiwemo elimu. Habari ya Salma Said na Picha za Martin Kabemba wa Zanzibar. SOURCE: MWANANCHI
safari za treni reli ya kati zaanza
KAMPUNI ya Reli nchini (TRL) imezindua rasmi safari moja kwa wiki ya treni ya abiria badala ya tatu kama ilivyo zoeleka.
Safari hizo zilizinduliwa jana baada ya kusitishwa kwa miezi sita kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha sehemu mbalimbali za nchini na kusomba daraja na reli za Kampuni hiyo.
Akizungumza na Mwananchi katika Makao Makuu ya TRL muda mfupi kabla ya kuzindua safari hiyo kwa kupeperusha bendera yenye rangi ya kijani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Hundi Chaudhary alisema kwa sasa wanaanza na safari za Kigoma.
“Kwa sasa tunanza na safari za kigomo pekee kwa sababu hatuna mabehewa ya kutosha na safari hii itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki ambayo ni kila Ijimaa,”alisema Chaudhary.
Alisema treni hiyo imeondoka na mabehewa 15 badala ya 21 ikiwa na abiria 600 tu kwa ajili ya abiria wa Kigoma ambao wanapata shida kutoka na mkoa huo kukosa miundombinu sahii kwa usafiri wa basi.
Kuhusu usalama wa treni hiyo ambayo imemaliza miezi sita bila ya kufanyakazi kiasi cha kusababisha mabehewa sita kushindwa kufanya kazi kutokana na ubovu Chaudhary alisema, kuna usalama wa kutosha na abiria wote watafika salama.
“Hii treni inausalama wa kutosha na mafundi wetu pamoja na watalaam kutoka Mamla ya Udhibiti wa Safari za Majini na nchi kavu (Sumatra) wameikagua na kuridhika na matengenezo madomadogo yaliyofanywa kabla ya safari hiyo kuanza,”alisema Chaudhary.
Wakati Mkurugenzi huyo akisema hayo baadhi ya abiria waliosafiri na treni hiyo jana walisema kurejea kwa safari hiyo imewasaidia na itaendelea kuwasaidia kwa sababu ni miezi sita sasa wamekuwa wakisafiri kwa shida.
“Safari hii ilivyonza leo imetusaidia sana kwa sababu sisi wananchi wa Kigoma tumesaulika kwa kipindi kirefu ndani ya nchi hii na tunapata shida kila siku,”alisema Amina Saidi.
Saidi alisema, tangu safari za treni hiyo zilipositishwa hajawai kusafiri kwenda Kigoma kutoka na shida ya usafiri na kwamba alishakata tamaa ya kufasiri kwa sababu hana uwezo wa kwenda Kigoma kwa usafiri wa basi. Picha na taarifa za Jackson Odoyo. SOURCE: MWANANCHI.
Sunday, June 20, 2010
Mashindano ya UMISETA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Wapili kushoto) akizungumza na washiriki wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) wakati alipofungua mashindano hayo kwenye uwanja wa Shirika la Elimu la Kibaha Juni 20, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua Mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) kwenye uwanja wa Shirika la Elimu KIbaha Juni 20, 2010. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Mghembe na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hajati Amina Mrisho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Washiriki wa Mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari TANZANIA (UMISETA) wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Juni 20 , 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Uzinduzi bodi ya TIC
Thursday, June 17, 2010
Adam Mwakibinga afariki dunia
MHAKIKI Kurasa wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, Sunday Citizen na Mwanaspoti, Adam Mwakibinga amefariki dunia baada ya kuugua.
Taarifa zilizotolewa jana na ndugu zake zilieleza kwamba Adam alifariki saa 10 :00 jioni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi kwa muda.
Ndugu hao walisema kuwa mipango ya mazishi ya marehemu Mwakibinga inafanyika jijini Dar es Salaam na Mbeya na taarifa zaidi kuhusiana na mahala yatakapofanyika mazishi zitatolewa leo.
Marehemu Mwakibinga alizaliwa miaka 46 iliyopita mjini Dodoma na alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi mwaka 1974 na akahitimu katika shule ya Msingi Mwenge mkoani Tabora.
Baadaye alijiunga na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Kazima iliyopo mjini Tabora ambako alihitimu kidato cha nne mwaka 1985.
Mwaka 1986 alijiunga na kidato cha tano katika shule ya Sekondari ya Mkwawa na kuhitimu kidato cha sita mwaka 1988 akiwa amefanya vizuri katika masomo yake.
Mara baada ya kuhitimu kidato cha sita mwaka 1988, Mwakibinga alijiunga na Kozi za uandishi wa habari ngazi ya cheti. Alijiunga na Kampuni ya Mwananchi Communications Julai 10, 2006.
Katika uhai wake marehemu Mwakibinga amewahi kufanya kazi mbalimbali ambapo mwaka 1988 hadi 1995 alifanya kazi ya ukarani wa mapato wa Mamlaka ya Maji Dodoma. Mwaka 1995 alifanya kazi ya usanifu Gazeti la Dar Leo hadi mwaka 2005. Mwaka 2005 hadi 2006 alikuwa Mwakilishi wa Kampuni ya Busines Times Ltd wilayani Rungwe. Marehemu Mwakibinga ambaye hadi anafariki ameacha watoto wawili. Mungu ailaze mahala pema peponi Ameen!
TBC launches a unique reality talk show dubbed 'Daladala'
TANZANIA Broadcasting Corporation (TBC) yesterday launched a unique reality talk show dubbed 'Daladala' which gives chance to people at the grassroots level to air their views and discuss a wide range of issues that affect their daily lives.
The programme will be aired through TBC 1 and 2 between 6pm and 6.30 pm. However, because of the ongoing world Cup Soccer matches, the programme will go on air at 3.30pm to 4pm.
"All the discussions will take place inside a special daladala fitted with electronic equipment to facilitate recordings," noted the Programme Manager, Furah Piniel.
A representative from the Information Department (Maelezo), Mr Abraham Nyantori, commended the move of giving chance to the voiceless in the country, promising full government support.
Mr Nyantori said his office will monitor the programme and point out any shortcomings that need to be addressed. "This is a very good move that will expose issues that touch daily lives of the common people in the community," he said.
The bright coloured daladala, which has been transformed into a mini mobile TV-studio with the help of Western technicians, will operate as a normal daladala taking in passengers, transporting them to their various destinations.
"There will be no charges, the only target is to get their views on various issues affecting their social lives," noted Daniel Kijo, one of the presenters of the talk show, who will be assisted by a conductor, Christina Mbuga, popularly known as Bibi Kiroboto.
Daniel Kijo noted that different topics will be picked, researched and introduced to the passengers for discussion during their rides to daily duties.
"We aim at raising awareness and encouraging the public to debate on important issues as perceived and experienced by the common Tanzanians," Kijo noted.
On her part, Bi Kiroboto commented, "Everyone wants to talk about what is affecting him or her. Some people are quite bitter at times. Others use abusive language.
But the programme is edited before being aired," Bibi Kiroboto explained. The Daladala was made possible by help of Tanzania Media Fund.
Wednesday, June 16, 2010
Siku ya mtoto wa Afrika cheki
Wakati wiki hii na hasa jana ilikuwa siku ya toto wa Afrika hebu cheki watoto wa kike waliodaiwa kuwa wanatokea katika kijiji cha Iziwa nje ya jiji la Mbeya wakijificha kupiga picha huku wakiwa wamebeba mafurushi ya kuni wakiwa wanasaka wateja katika maeneo ya mabatini jiini hapa (Picha na Hawa Mathias, Mbeya)
Father Nkwera akiwa kizimbani
Leader of Marian Faith Healing Centre (MFHC), Fr Felician Nkwera, leads his followers for a prayer inside the courtroom on Tuesday shortly after the Court of Appeal directed that an appeal in which the group challenge ban to participate in Catholic Church services in Sumbawanga, and which was dismissed by the High Court in 2004 or being time barred, be heard afresh.
Monday, June 14, 2010
Bomoa bomoa yakumba nyumba 89 Kibamba
ZAIDI ya kaya 89 hazina makazi baada ya nyumba zao kubomolewa katika maeneo ya Kibamba mji mpya kwa amri ya mahakama ya Kinondoni.
Wakizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki jijni Dar es Salaam waathirika wa bomoabomoa hiyo waliopo hapo juu pichani wakiwa katika vibanda baada ya kubomolewa nyumba zao walidai kuwa hawajawahi kuambiwa chochote juu yao kuishi katika eneo hilo.
“Tumeishi hapa kwa miaka minne sasa na hatujawa kusikia chochote kuhusu eneo hili wala kuambiwa kuwa ni eneo lenye mgogoro,”alisema Ferster Fumbe.
Alisema kuwa kilichowashangaza zaidi kuhusu suala hilo ni hatua ya watu waliodai kuwa wametumwa na mahakama hiyo kuja na Askari Polisi pamoja na kundi kubwa la wahuni kwa ajili ya kuboa nyumba hizo.
Jumbe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 7 asubuhi akiwa na wiki mbili tangu alipojifungua mtoto wake wa kiume kwa njia upasuaji na kwamba ghafla akashtukia kundi kubwa la watu kunvamia na kunaza kuboa nyumba yake huku baadhi yao wakichukua vitu ndani. Jackson Odoyo: Source MWANANCHI.
Sunday, June 13, 2010
Maandamano kumuunga mkono JK
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo mchana(picha zote na Freddy Maro)
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo cha utii kwa Chama Cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wakati wa maandamano ya kumuunga mkono yaliyofanyika mjini Dodoma.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Kaimu Mwenyekiti UVCCM Beno Malisa, na Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba.
Baadhi ya vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakiandamana kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua fomku kwaajili ya kugombea nafasi ya urais 2010.
mwaka huu.
Friday, June 11, 2010
Kitukuu cha mzee Mandela chafariki Dunia
(Pichani Mzee Nelson Mandela na Mtukuu wake Zanani mwaka 2008)
Habari za kusikitisha kutoka Afrika Kusini. Mtukuu wa Nelson na Winnie Mandela, Zenani mwenye miaka 13 amefariki katika jali ya gari. Habari kutoka huko zinasema kuwa walikuwa wanarudi kutoka kwenye sherehe za ufunguzi wa mashindano ya World Cup. Dereva wa gari alikuwa amelewa!
Pole sana familia ya Mandela. Mungu ailaze roho ya Zenani mahala pema mbinguni. AMEN.
*********************************************************************
Kutoka New York Times:
JOHANNESBURG — Heartbreak intruded on the opening day of the soccer World Cup when Nelson Mandela’s 13-year-old great-granddaughter Zenani was killed in an auto accident here early on Friday. In response, Mr. Mandela canceled a much-heralded appearance at a tournament depicted as a triumphant showcase for his country and his continent.
Zenani Mandela was returning home from the event’s Thursday night kickoff concert in Soweto, an extravaganza with stars like Alicia Keys and Shakira that was meant to launch the contest on a joyous note. At its conclusion, the sky lit up with fireworks as happy attendees made way to their parked vehicles.
According to police, Zenani died in a one-car accident on a Johannesburg highway. The man behind the wheel, who has yet to be named, was accused of drunk driving and may also be charged with culpable homicide, the police said.
PICHA NA HABARI NIMEZIKWAPUA TOKA KWA DA CHEMI
Mariam Migomba 'Mami' aibuka mtangazaji nyota
Hatimaye lile shindano la kumsaka mtangazaji bora wa vipindi vya taarab mwaka huu hapa nchini lilifikia tamati usiku wa siku ya Jumapili taehe 6/6/2010 ndani ya ukumbi wa hoteli ya Travertine, Magomeni jijini Dar ambapo mtangazaji nyota wa redio ya TBC1 Mariam Migomba 'Mami' aliibuka kidedea dhidi ya mtangazaji wa redio ya Times FM, Khadija Shaibu 'Dida'.
Katika mpambano huo ulioendeshwa kwa ustadi mkubwa na mtangazaji mwenzao Maimartha Jesse aliyekuwa MC, Mariam Migomba alipata kura 425 dhidi ya 386 za Dida ambapo pamoja na burudani ya kundi la Jahazi Modern Taarab mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Kinondoni, Mhe Idd Azzan.
Mratibu wa shindano hilo, Kaka Mwinyi, alisema kuwa, amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na shoo hiyo ambayo ilikwenda vizuri na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi na mashabiki wa watangazaji hao waliokuwa na shauku ya kujua nani kati yao atatwaa taji la umalkia huo.
"Haikuwa kazi rahisi kuwakutanisha watangazaji hao katika jukwaa moja kwa dhumuni la kushindana, lakini, nashukuru Mungu mambo yalikwenda bara-bara na karibu kila aliyekuwemo ukumbini pale Travertine alionesha kuridhika na matokeo kwani hakukua na kuzomea wala kurusha chupa kama zilivyo shoo nyingine," akasema Kaka Mwinyi.
Aidha, katika shoo hiyo mbali ya washiriki hao kupata tuzo maalum zilizochongwa kwa nakshi kila mmoja, pia, walipata zawadi ya pesa taslim (kiasi hawakutaka kitajwe hadharani) walizokabidhiwa na Mbunge wa Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan aliyekuwa Mgeni Rasmi wa shoo.
Wakati huo huo, Kaka Mwinyi amesema kuwa, baada ya shoo hiyo, anajipanga kufanya shoo kubwa zaidi na ya aina yake itakayohusisha watangazaji wote wa kike wa runinga na redio nchini kabla ya mwezi Desemba mwaka huu ili kuleta changamoto miongoni mwa wadau wa tasnia hiyo adhimu ya habari kwa njia ya redio na runinga.
brought to you by
kaka Mwinyi - 0713 552211 or 0655 002015 or 0777666888
Tuesday, June 08, 2010
Mpigapicha Habari Leo amshukuru Rais Kikwete
MPIGA mpicha wa magazeti ya Serikali yanayochapisha magazeti ya Habari Leo na Dailynews (TSN), Athuman Hamisi amemshukuru Rais Jakaya Kikwete na uongozi wake kwa msaada mkubwa pindi alipokuwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata ajali mbaya mwaka 2008 na kusababisha ulemavu wa kudumu.
Hamisi aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari (Maelezo) wakati akizungumzia ajali ailiyoipata Septemba 12, mwaka 2008 katika eneo la Kibiti wakati akiwa njiani kuelekea Kilwa kikazi.
Alisema anamshukuru Rais Kikwete baada ya kwenda kujulia hali alipokuwa Muhimbili pamoja na Afrika Kusini alipokuwenda kwa ajili ya upasuaja mkubwa baada kuumia shingo na uti wa mgongo.
“Kweli hujafa hujaumbika huu ni usemi wa siku nyingi lakini siku ukimtokea kwako ndio unaona thamani ya msemo huo hali kadhalika kuwa hakuna barabara ndefu isiyokuwa na kona,” alisema Hamisi
Anasema kuwa baada ya ajali hiyo alipelekwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha Mifupa Moi kwa siku 15 kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hamisi ambaye kabla ya kuwa mlemavu alikuwa mpiga picha maarufu alisema kuwa Septemba 28, mwaka huo huo alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa upasuaji katika kipindi cha mwezi Oktoba na Novemba 2008 katika hospitali ya Millpark iliyopo mjini Johannesburg.
Alisema kuwa upasuaji wake ulichukua muda wa saa nane katika hospitali iyo iliyochini ya shirika la kimataifa la Netcare ambapo alikaa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa kipindi cha miezi mitano na wiki mbili kabla ya kuamia katika wodi ya nne ambayo ni ya wagonjwa wa kawaida.
Alisema kuwa upasuaji ulichelewa baada ya madaktari kuamua kutibu kwanza vidonda vya kichwani vilivyotokana na ajali hiyo.
Kwa sasa mimi naendelea vizuri ingawaje siwezi kusimama wala kutembea na baadhi ya viungo vyangu havifanyi kazi kutokana na kuvunjika kwa uti wa mgongo mpaka kiuno,”alisema Hamisi .
Alisema ni vigumu kuamini kwa watu waliomuona katika hospitali ya Muhimbili , Moi na siku alipoondoka kwenda Afrika ya Kusini kuni hali yake ilikuwa mbaya sana tofauti na sasa.
Hamisi aliwasili nchni Mei 8,mwaka huu kutoka Afrika ya Kusini alipokuwa kwa ajili ya matibabu yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.
Miongoni mwa matu wengine waliojeruhiwa katika ajili hiyo mwandishi ni Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kupata ajali ya pikipiki na Athony Siyame.
Vile vile ametoa shukrani kwa Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii, uongozi wa TSN, Ofisi ya Mawasiliamo Ikulu, pamoja na waandishi wa habari ikiwemo wadau wote kwa kwa sala zao pindi alipokuwa hospitali. Habari ya Hadija Jumanne. SOURCE: MWANANCHI.
Sunday, June 06, 2010
Safari ya Twiga Stars Marekani yaiva
Mlezi wa timu ya soka ya wanawake ya Twiga stars Rahma Al Kharoos akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam jana, kuhusu kukamilika kwa safari yao ya wiki mbili ya timu hiyo nchini Marekani mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, ambapo itacheza mechi nne za kirafiki za kujipima, kulia ni Ibrahim Khatrush. Picha na Michael Jamson
Bendera ya Taifa
HUYU jamaa sijui ni kwamba anaipenda nchi yetu au anazuga, lakini habari ndiyo hii raia wa Australia, Jock Biduull amekuwa akiwashangaza mamia ya wakazi wa Arusha kutokana na kuamu kufunga bendera ya Taifa katika gari lake na kuranda nalo mitaani kwa takriban siku tatu sasa.
Raia huyo ambaye yupo nchini akifanya kazi za kujitolea katika shule ya St Jude iliyopo wilayani Arumeru mkoani hapa, ametundika bendera ya Taifa mbele ya gari lake na kuranda nalo mitaali bila hofu.
Hata hivyo, wakati raia wa kawaida wamekuwa wakiona kitendo hicho ni ukiukwaji wa katiba ya nchi hasa kuhusiana na hadhi ya Bendera ya Taifa, lakini hata hivyo hakuna chombo chochote za usalama ambacho kimemkataza.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika eneo la Arusha Hoteli mjini hapa juzi, Biduull alisema ameamua kufunga bendera ya Taifa la Tanzania mbele ya gari lake kutokana na kuipenda nchi hii.
"Mimi sijuwi kama ni kosa ila tangu nimekuja Tanzania nimeipenda sana na nimeona nifunge kwenye gari bendera ya nchi hii,"alisema Biduull.
Mkuu wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) mkoani Arusha, Shillinde Ngalula akitoa maoni yake kisheria kuhusiano na kuweka kwenye gari bendera ya Taifa alisema ni makosa mtu asiyeruhusiwa kuiweka.
"Kama ni kweli huyo mzungu anatembea na bendera ya Taifa kwenye gari atakuwa amekiuka sheria ya Nembo za Taifa hivyo ni makosa kwani pia anaweza kusababisha kutisha watu bila sababu za msingi,"alisema Ngalula.
Hata hivyo hakuna afisa wa polisi ambaye alikuwa tayari kuzungumzia ni kwa nini Rais huyo wa Autralia ameshindwa kukamatwa wala kuhojiwa kutokana na kuweka bendera ya Taifa kwenye gari lake na kutamba nayo mitaani. Habari na picha ni za Mussa Juma wa Arusha: SOURCE MWANANCHI.
Njiti tuu zinatembea kwa madenti
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...