Sunday, December 26, 2010

Rais Kikwete amteua Jaji Mkuu mpya


TAARIFA YA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Jaji Othman anachukua nafasi ya Jaji Augustino Ramadhani anayestaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 27 DIsemba, 2010.
Kwa sasa Jaji Othman ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na pia ni mtaalamu binafsi juu ya hali ya Haki za Binadamu huko Kusini mwa Sudan, hadi mwezi Agosti 2011.

Jaji Othman alizaliwa tarehe 1 Januari, 1952, ana shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) kutoka katika Chuo Kikuu cha Webster, Geneva-Uswisi.

Amewahi kuwa Makamu wa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Rwanda huko Arusha na amewahi kushika nafasi sawa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali huko Timor Mashariki.

Jaji Othman pia, amewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kama vile Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Jaji Othman ataapishwa kesho tarehe 27 Disemba, 2010 katika viwanja vya Ikulu saa 4:00 asubuhi.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Ikulu
Dar es Salaam
26 Disemba, 2010

Makazi mapya ya Spika Makinda

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika kutoka kwa Maafisa wa Bunge pamoja na wakandarasi kutoka Wakala wa Ujenzi (TBA).. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Jengo la Makazi ya Spika linavyoonekana kwa sasa

Thursday, December 23, 2010

Profesa Ndullu akabidhi fedha mpya kwa JK



The Governor of Bank of Tanzania Prof. Benno Ndulu, today presented the new Tanzanian shilling currency note to President Dr. Jakaya Kikwete at Dar es Salaam State House this evening. The New Currency Note will be in circulation from January next year and they will be used alongside with the current bank notes. In the Picture The Central Bank Governor Prof. Ndulu (left) presents a special album with new Tanzanian shilling currency notes to President Dr. Kikwete while the Minister for Finance Mustafa Mkullo,(right) looks on.

Wednesday, December 22, 2010

Michuano ya Netball

Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu akimiliki mpira dhidi ya wachezaji wa Mwanza wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la Taifa la netiboli iliyofanyika viwanja vya shule ya sekondari Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani jana. Picha na Silvan Kiwale

Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu akiwa kwenye hekaheka ya kufunga huku akiwa kwenye ulinzi wa wachezaji wa Mwanza. Mfungaji wa Morogoro Zuhura Twalibu (kulia) akifunga goli wakati wa mechi
ya nusu fainali ya kombe la taifa la netball dhidi ya Mwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani jana. Picha zote za Silvan Kiwale.

Tuesday, December 21, 2010

Mary apata shahada ya uzamivu




Mkuu wa United Graduate College and Seminary, Clyde Rivers,(kulia) akimkabidhi Shahada ya Uzamivu ya Masuala ya Jamii katika Kuthamini Utu, Mary Mwanjelwa, (wapili kushoto) kutoka kushoto ni askofu,Dkt,Arthun Kitongo wa Association of Evangelicals in Africa, Joe Mzunda na Prof Nathan Kabara.

Saturday, December 18, 2010

Mariam Mohammed ndiye mshindi Bongo Star Search



Mwanadada Mariam, aliyejipatia umaarufu katika BSS 2010 kwa umahiri wake wa kuimba miondoko ya Taarabu, usiku wa kuamkia leo ametangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo liliofanyika katika ukumbi wa Mlinami City jijini Dar es salaam na kushudiwa na Waziri wa habari, Michezo na Vijana, Emmanuel Nchimbi.
Pichani, Mariam akishangilia ushindi wake baada ya kukabidhiwa zawadi yake ambayo ni shilingi za bongo milioni 30 na zawadi nyingini kibao! kwa taarifa zaidi ingia http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/marim-ndiye-mshindi-bss-2010

Monday, December 13, 2010

Kifo hakina huruma kimemchukua Dk Remmy




Mwanamuziki mkongwe na kipenzi cha watu wengi nchini, Ramazani Mtoro Ongala au maarufu kama Dokta Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi.

Habari zilizopatikana katika eneo la msiba leo asubuhi zinasema msiba wa mwanamuziki huyo utakuwapo nyumbani kwake Sinza kwa Remmy jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi za mipango za mazishi tutawaleteeni baadaye.

Dk Remmy Ongala ni mmoja wa wanamuziki waliojipatia umaarufu nchini Tanzana tangu miaka ya 1980 kutokana na umahiri wake katika masuala ya muziki.

Ongala, mwanamuziki mwenye asili ya Kikongo, alizaliwa mwaka 1947 Kisangani huko Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (DRC), wakati huo ikijulikana kama Zaire, na ndiko alikoanza kujihusisha na muziki wa dansi.

Alisema kwamba alianza kuupenda muziki tangu akiwa mtoto kwa sababu ni moja ya fani iliyokuwa damuni, pia anaamini Mungu ndiye aliyempatia kipaji mpaka kufikia kupendwa na wapenzi wengi wa muziki.

Mnamo mwaka 1964 ndio alianza rasmi masuala ya muziki akiwa DRC na bendi ya Grandmike.

Mwaka 1967 alijiunga na kundi lingine lililojulikana kama Sakses Bantu ambalo pia lipo hukohuko DRC.

Ongala alikuja nchini katika miaka ya 1970 na kufanikiwa kuendelea na muziki ambapo alianzisha bendi yake ya Super Matimila na kutoa albamu kadhaa kama "Kilio cha Samaki" na nyinginezo.

Mkongwe huyu anakumbukwa na nyimbo zake zilizotikisa ulimwengu wa muziki wa dansi kama 'Mambo kwa Soksi', 'Kifo Hakina huruma', 'Mambo Mbele kwa mbele' na nyinginezo nyingi zilizomfanya ajipatie umaarufu nchini na nje ya nchi.

Sunday, December 12, 2010

KILIMANJARO STARS MABINGWA WAPYA WA CECAFA


Timu ya Taifa Stars imenyakua ubingwa wa kombe la Tusker Cecafa, Challenge Cup baada ya kuibwaga Ivory Coast kwa bao moja kwa bila katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo iliyomalizika muda mfupi uliopita katika uwanja wa taifa.

Mfungaji wa bao hilo alikuwa nahodha wa timu hiyo ya taifa Shadrack Nsajigwa kwa njia ya penati ambapo alikung’uta mkwaju mkali ulioingia wavuni na kumwacha kipa wa timu ya Ivory Coast akigaragara, hiyo ilikuwa dakika ya 31.

Mara baada ya kufunga bao hilo uwanja uliripuka kwa furaha na vifijo, Ushindi huo umekuwa zawadi kuu kwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seifa Shariff Hamad. Mshindi wa tatu ni timu ya Uganda ambayo imemrambisha Ethiopia bao 4-3.

Saturday, December 11, 2010

DONDOO KUHUSU MATONYA



Jina lake halisi ni Paulo Mawezi

Jina Matonya ni la utotoni

Ni mume wa wake watatu

Ni baba wa watoto wawili, Elizabeth na Ernest

Aliishi Kilimatinde, Singida miaka 30 iliyopita

Sasa ni mkazi wa Bahi Sokoni, Dodoma

Alianza 'kazi' ya ombaomba kabla ya uhuru

Hukusanya kati ya sh 4000 na 7000 kwa siku

Alitoroka kambini Moro, akapandishwa kizimbani

Kuila Krisimas 2010 jijini Dar es Salaam

Friday, December 10, 2010

Mkutano wa kukabili uharamia


Waziri ya Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP , Saidi Ali Mwema leo asubuhi katika hoteli ya Moven Pick Hotel wakati wa ufunguzi wa programu ya mkutano wa kanda wa wakuu wa polisi kuzungumzia suala la uharamia. kulia ni Kamishna wa Polisi , Paul Chagonja. (picha na Hassan Mndeme- Police Force).



Wednesday, December 08, 2010

Bambaga kuzikwa Musoma kesho



MAZISHI ya aliyekuwa mchezaji wa zamani soka wa Tanzania, Nico Bambaga yanatarajia kufanyika kesho nyumbani kwao Musoma mkoani Mara.

Bambaga alifariki dunia usiku wa Jumatatu katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu.

Msemaji wa familia ya marehemu alisema jijini Dar es Salaam leo kuwa utaratibu wa mazishi ya mwanasoka huyo yalikuwa yakiendelea vizuri na mwili wake ulitarajiwa kusafirishwa jana kwa maziko ambayo yatafanyika kwa taratibu maalumu nyumbani kwao mjini Musoma.

"Kifo cha mpendwa wetu kwa kweli kimetushtua sana sisi kama wanafamilia na alikua na mchango mkubwa hivyo ameacha pengo kubwa kwetu ambalo si rahisi kuzibika kwa sasa.

Msiba huu si pengo kwetu tu bali kwa wanafamilia wote wa soka nchini kwani Nico alikuwa mchezaji wa kutumainiwa na ambaye aliweza kuichezea pia na timu ya taifa,"alisema.

Wakati wa uhai wake, Bambaga alizichezea Pamba ya Mwanza kabla ya kuhamia Yanga na baadaye Simba, Malindi ya Zanzibar, wakati huo akiichezea pia Taifa Stars. Imeandikwa na Jessca Nangawe.

Tuesday, December 07, 2010

Mshindi wa pili wa Shindano la Tusker Project Fame awasili






LICHA ya Mganda Davis Ntare kutwaa taji la Tusker Project Fame 2010, jopo la majaji kwa pamoja na uongozi wa chuo cha mafunzo cha shindano hilo wamekiri kwamba mshiriki wa Tanzania, Peter Msechu, ana kila sababu ya kuwa ndiye mshindi wa shindano.

Kila mtu kwa wakati wake, majaji Ian, Hermes Joachim na Juliana Kanyomozi, walimtaja Msechu kuwa ni mwanamuzikii maarufu anayejiamini sana na kujiweza jukwaani, na pia mbunifu.

Sifa hizo ndizo zinazotakiwa kwa mwanamuziki wa karne hii iliyojaa utandawazi, walieleza majaji.

Msechu ambaye kete yake ya mwisho aliitupa kwa kutumia kwa kibao cha Kilwa Jazz aliudhihirishia tena umma wa wengi katika Afrika Mashariki kwamba anaweza kuwainua kwenye viti na kuwaimbisha muda wowote anaotaka.

Msechu, huku akionyesha kujiamini kwamba muziki ni njia pekee ya kueleza hisia zake kwa jaji huyu kwani, angepata wapi nafasi nyingine ya kumwambia.

"Ningemuita nikamwambia nina maongezi naye angekuja?", alisema Msechu katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya onyesho hilo kwisha na washindi kutajwa katika maeneo ya Ruaraka, jijini Nairobi, eneo ambapopia yapo makao makuu ya East African Breweries, watengenezaji wa bia ya Tusker.

Akizungumza na Mwananchi, Msechu ambaye ameshinda mkataba wa mwaka mmoja wa wa kurekodi na Kampuni ya Africa Sound yenye makao makuu nchini Kenya alisema anaamini kuwa yeye ni mshindi, ila zawadi kubwa amechukua Davis, na atalithibitisha hilo atakapoanza rasmi kazi yake ya muziki, mashabiki wataendelea kufurahi kumsikiliza na kumuona jukwaani.

Monday, December 06, 2010

Teknolojia ya digitali yatinga mahakamani



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizinduwa mfumo wa kurekodi mashauri mahakamani kwa kompyuta na Tovuti ya Mahakama katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo.

******************************************************



HATIMAYE Mahakama ya Tanzania imeanza rasmi kutumia teknolojia ya kisasa katika kuendesha shughuli zake, baada ya kuzindua mfumo mpya wa kuweka kumbukumbu za mashauri mbalimbali kwa kutumia kompyuta.
Mfumo huo wa digitali ulizunduliwa jana na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal kwenye ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Sambamba na mfumo huo, mahakama pia imezindua tovuti yake ambayo itakuwa na taarifa mbalimbali kuhusu sheria zinazotumika nchini, hukumu za kesi za kuanzia mwaka 1979 na taarifa nyingine kuhusu kesi zinazoendelea mahakamani.
Kutokana na kuzinduliwa kwa mfumo huo sasa majaji wa Mahakama Kuu na wa Mahakama ya Rufani hawatalazimika kuchukua kumbukumbu za mwenendo wa kesi mbalimbali kwa kuandika kwa mikono na badala yake kazi hiyo itafanyika kwa kutumia kompyuta maalum.
Katika mfumo huo mwenendo wa kesi utakuwa unaingia kwenye kifaa maalumu cha kuhifadhia sauti kwenye kompyuta na baada ya dakika tatu sauti hizo huanza kuchapwa na wataalumu na kuwekwa katika maandishi.
Kwa kuanzia, mfumo huo utaanza kutumiwa na majaji wa Mahakama ya Rufani na wa Mahakama Kuu Dar es Salaam kabla ya kuziunganisha kanda nyingine 14 ikiwa ni pamoja na mahakama za chini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Dk Bilal alisema matumizi ya teknolojia hiyo yataharakisha usikilizaji wa kesi, lakini yatajenga mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.
Dk Bilal alisema ni matakwa ya haki na katiba ya nchi kuwa kesi zimalizike katika muda muafaka, lakini zimekuwa hazimaliziki mapema na kusababisha mahakama kulalamikiwa kwa kuchelewesha kumaliza kesi mbalimbali.
Aliitaka mahakama kutumia sheria kwa ufanisi na kwamba kasi katika kuhitimisha kesi imaanishe upatikanaji wa haki badala ya kuzua mashaka.
Badala ya kuahirisha kesi mara kwa mara, Dk. Bilal aliitaka mahakama kuhakikisha kuwa kesi zinaeneshwa kwa kasi, kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuhitimishwa kwa haki na usawa.
“Wafanyabiashara na wawekezaji wanavutiwa kuwekeza katika nchi ambazo utekelezaji wa mikataba ni rahisi kwa maana kwamba gharama za kufungua mashauri ni za chini na kesi kuendeshwa kwa haraka,” alisema Dk. Bilal .
Alisema matarajio ni kwamba kampuni ambazo zina matatizo ya kisheria katika shughuli zake za kibiashara, lazima yaweze kutatuliwa haraka ili kuwezesha uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma wa kampuni hizo.
Dk. Bilal alisisitiza kwamba haki za binadamu na katiba yetu zimejenga mazingira ya haki na usawa katika usikilizwaji wa mashauri na kwamba mahakama ndio yenye jukumu hilo.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Jaji Mkuu Agustino Ramadhani alisema mahakama imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchelewa kumaliza mashauri kutokana na kutumia zaidi mfumo wa uchukuaji wa kumbukumbu unaotegemea kuandika kwa mkono tu.
Alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo mpya wa kiteknolojia kutawawezesha majaji kuepukana na mfumo wa kizamani na hivyo kuharakisha uhitimishwaji wa kesi.
Jaji Ramadhani alisema faida kubwa ya mfumo huo ni kumwezesha Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kujua kila kinachofanywa na kila jaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu.
Imeandikwa na James Magai wa Mwananchi

Wednesday, December 01, 2010

Happy Birthday Dear First Lady Salma Kikwete



Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akilicharaza gitaa wakati alipowaongoza wanafamilia nyumbani kwake kumpongeza mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka 47 jana.

Kumbe mgomo wa Ustawi wa jamii ni kanyaboya


SERIKALI ya wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii imesitisha mgomo wao mara tu baada ya raisi wa chuo hicho kuitwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ofisini kwake na kumuahidi kushughulikia matatizo ya chuo hicho ndani ya wiki moja.

Hata hivyo habari tulizozipata kutoka katika chanzo chetu cha habari zinaeleza kuwa tatizo la chuo hicho linasabababishwa na mpasuko uliopo ndani ya uongozi wa chuo kwa kudai kuwa na makundi mawili mbayo yanavutana ili kuharibiana sifa.

“Hapa chanzo cha tatizo ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Ufundi ya kati(NACTE) ambayo ilileta muongozo na sifa zinazotakiwa kwa baadhi ya watu wanaotakiwa kuwa ndani ya uongozi wa chuo,” kilisema chanzo hicho.
Kilisema kuna watu ambao wapo katika nafasi nyeti za uongozi wa chuo na hawana sifa zilizotajwa na NACTE ivyo basi wameamua kutumia wanafunzi ili waweze kukamilisha lengo lao.
“Wanafunzi wanatumiwa kama chambo tu lakini wao hawajui chuki imejengwa na watu kutoka juu na mtu huwezi kulazimisha kukaa mahali wakati huna sifa za kuwa na cheo kuwa na mdaraka serikalini sio sababu ya kuweka mizigo katika sekta muhimu kama hizi,” kilisema chanzo hicho.
Hata ivyo raisi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho jana aliitwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ili kuweza kupata ufumbuzi wa tatizo lao.

Sunday, November 28, 2010

Mke wa Mzee wa Mshitu apata nondooz


Mdau Eric Anthony ambaye ni Mhariri wa Habari wa HABARILEO (Jumamosi na Jumapili) akipozi na Mzee wa Mshitu, Yahya Charahani,kwenye ukumbi wa Mlimani City ambako Eric alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Taaluma za Maendeleo (Mipango na Utawala) wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.Picha ya John Bukuku.


Mzee wa Mshitu au Yahya Charahani wa Blogu hii akimvisha mkewe shada la maua baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika sanaa na elimu muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada hiyo na mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Balozi Fulgence Kazaura mahafari hayo alifanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana /Picha na Jackson odoyo

Wednesday, November 24, 2010

Baraza jipya la mawaziri

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI



OFISI/WIZARA
WAZIRI

NAIBU WAZIRI

1.Ofisi ya Rais



1. WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe

2. WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira


2.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

Hawa Ghasia

3.Ofisi ya Makamu wa Rais


1.Muungano

Samia Suluhu

2.Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa


4.Ofisi ya Waziri Mkuu


1.Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi

2.Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu


5.Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)


George Huruma Mkuchika

1.Aggrey Mwanri

2.Kassim Majaliwa


6.Wizara ya Fedha

Waziri

Mustapha Mkulo

Manaibu

1. Gregory Teu

2. Pereira Ame Silima

7.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Shamsi Vuai Nahodha

NAIBU
1.Balozi Khamis Suedi Kagasheki

8.Wizara ya Katiba na Sheria

Celina Kombani


9.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Bernard K. Membe

NAIBU

Mahadhi Juma Mahadhi

10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11.Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. Mathayo David Mathayo

NAIBU

1. Benedict Ole Nangoro

12.Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

NAIBU

1. Charles Kitwanga

13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna Tibaijuka
Goodluck Ole Madeye

14.Wizara ya Maliasili na Utalii

Ezekiel Maige

15. Wizara ya Nishati na Madini

William Mganga Ngeleja

NAIBU

1. Adam Kigoma Malima

16. Wizara ya Ujenzi

Dr. John Pombe Magufuli

NAIBU

Dr. Harrison Mwakyembe

17. Wizara ya Uchukuzi

Omari Nundu

NAIBU

Athumani Mfutakamba

18. Wizara ya Viwanda na Biashara

Dr. Cyril Chami

NAIBU

Lazaro Nyalandu

19.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru Kawambwa

NAIBU

Philipo Mulugo

20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Haji Hussein Mpanda

NAIBU
Dr. Lucy Nkya

21.Wizara ya Kazi na Ajira

Gaudensia Kabaka

NAIBU
Makongoro Mahanga

22.Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Sophia Simba

NAIBU

Umi Ali Mwalimu

23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo

Emmanuel John Nchimbi

NAIBU

1. Dr. Fenella Mukangara

24.Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Samuel John Sitta

NAIBU

1. Dr. Abdallah Juma Abdallah

25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

Prof. Jumanne Maghembe

NAIBU
1. Christopher Chiza

26. Wizara ya Maji

Prof. Mark James Mwandosya

NAIBU
Eng. Gerson Lwinge

Sunday, November 21, 2010

Choo cha kwetu uswazi


Kwa wale wenzangu na mimi ambao ama wamewahi au wanaendelea kuishi katika vyumba vya kupanga katika maeneo yetu ya uswahilini, bila shaka wanazielewa ipasavyo adha wanazozipata na hususan pale unapowadia muda wa kwenda msalani.

Lakini kwa wale waliobahatika kuzaliwa katika familia zilizoneemeka hapa duniani, watakuwa hawanielewi ninapozungumzia adha ya vyoo vya uswahilini. Kwao vyoo ni vya kutumia maji ambayo husukuma uchafu kwa ustaarabu wa hali ya juu. Hakuna bughudha wala kinyaa chochote kwa watu hawa pindi waingiapo msalani. Hebu cheki choo hiki kilichopo karibu kabisa na katikati ya jiji Magomeni hapa halafu unambie.

Mzee Boziboziana mchawi wa Nzawisa ndani ya Bongo



Mwanamuziki kutoka nchini Congo, Bozoboziana (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Meneja wa Bendi ya African Stars Twanga Pepeta,Asha Baraka (wa pili kulia) walipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.Boziboziana yupo nchini kwa mafunzo maalumu kwa bendi ya Twanga katika kujitayarisha na soko la kimataifa.Picha na Venance Nestory.

Saturday, November 20, 2010

Dk Muterea afariki dunia



DK Absalom Mutere amezikwa leo mchana katika makaburi ya huko Musanda, Mumias, Kakamega Kenya. Alifariki ghafla akiwa safarini nchini Zambia ambako alikwenda kwaajili ya masuala yake ya kitaaluma. Dk ay Profesa Mutere ninamkumbuka sana kwa staili yake ya ufundishaji na kwa nondo zake alizotupatia katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino hasa darasa la Masters 2009.
Hakika fani ya mawasiliano ya Umma imepoteza gwiji lake ambaye alikuwa ni mtu asiyekuwa na mikwara na wala kinyongo hata kidogo, kufundisha kwake ilikuwa kama ni maji asipokunywa anakuwa na kiu.
***************************************


Mutere was educated in the UK, Uganda, Kenya and the USA. He held a BA in Political Science, MA in Journalism (Kent State University, USA), and a PhD from the University of Amsterdam.

He passed away on Tuesday 9 November in Lusaka, aged just 54. He leaves behind a wife, Chalwa Mutere, and two daughters, Ayanda and Julia, from a previous marriage.

He also leaves behind a rugby fraternity that will mourn his departure while celebrating his enormous contribution to the sport.

----------------------------------------------------------------------------
It is with humble acceptance of God’s will that we announce the passing away of Dr Absalom “Bimbo” Mutere in Lusaka, Zambia.

Loving husband of Chalwa Mutere. Father of Ayanda and Julia Mutere. Son of the late Prof Festo Abby Mutere and Mrs Melcah Ephalinah Mutere. Brother of Matilda Mutere, the late Anna Mutere, the late Jacqueline Mutere, Gillian Mutere and Flora Okuku. Brother-in-law of Greg Pirio and Tony Okuku, and uncle to several.


Body arrived in Nairobi on Wednesday, Nov 17, 2010. Friends, relatives and professional colleagues meet daily at Nairobi Railway Club.



Fundraiser took place on Tuesday, Nov 16, 2010 at same venue at 6pm. Burial on Saturday, Nov 20, 2010 at Musanda, Mumias, Kakamega County.



We will miss you terribly.

“A good name is better than precious ointment; and the dayof death than the day of one’s birth.” - Ecclesiastes 7:1.

Tuesday, November 16, 2010

Vodacom gets US $4.8 million to expand M-Pesa services


Vodacom Tanzania is to receive a 4.8 million US dollars grant from the Bill & Melinda Gates Foundation to augment financial inclusion in Tanzania through increased usage of its mobile money service, Vodafone M-PESA.
Vodacom Managing Director, Dietlof Mare, said that the grant aims to and will improve the lives of Tanzanians as Vodacom believes that financial inclusion is possible through the use of Vodafone M-PESA.
The grant, about 7.2 billion Tanzanian shillings, will be used to enhance and improve Vodafone M-Pesa services that a customer receives from an agent, Mare said.
“Vodacom will use the money to increase the awareness and service benefits of Vodafone M-Pesa specifically to those living in remote parts of the country”, he noted.
“Tanzania has a highly dispersed population of around 40 million, which severely restricts access to financial services. Today only two million Tanzanians have access to a bank account while over 18 million are mobile phone users,” he said.
Research in Kenya and Tanzania shows that many people find M-PESA provides a safe and affordable way to store and send money to friends, family and business associates.
According to Mare, Vodacom has been singled out to receive the grant because the company laid the groundwork for the uptake of mobile money transfer services in the country and has invested greatly in the technology.
To date over 5.3 million people have already registered to use Vodafone M-PESA in Tanzania.
Although it is ideally suited for those without access to financial services, it is the banked community that has been the quickest to take advantage of the convenience, security and efficiency it offers.
With funding from the Bill & Melinda Gates Foundation through the Financial Services for the Poor initiative, Vodacom will extend this service to reach the wider “unbanked” community.
This grant was announced on November 16 by Melinda French Gates at the Global Savings Forum in Seattle, Washington, as a part of the foundation’s $500 million pledge to expand access to savings accounts and help the world’s poor build financial security.
The pledge included a package of six grants, totaling $40 million, from the foundation’s Financial Services for the Poor initiative, to support projects and partnerships that will bring quality, affordable savings accounts and other financial services to the doorsteps of the poor in the developing world.
“Savings doesn’t just help people mitigate the risks posed by a medical emergency or a bad crop,” said Gates at the foundation-hosted event.
“It also gives them the ability to marshal their resources to build something better for themselves and their children. It allows them to fund their own businesses, to look ahead with confidence. Savings helps families to take the giant leap from reacting to events to planning for a healthier, happier future.”

Mbunge wetu Mary Mwanjelwa akiapa bungeni


Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa akiapa, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 13, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, November 15, 2010

Pinda umechakachuaa hahahahaha


Waziri Mkuu aliyemaliza muda wake, Mizengo Pinda akifurahia jambo na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa walipokutana nje ya ukumbi wa Pius Msekwa bungeni jana mjini Dodoma. Pinda alikwenda kujumuika na wabunge wenzake wa CCM waliokuwa na kikao cha kumteua mgombea wa Naibu Spika kwa tiketi ya chama chao. Picha na Edwin Mjwahuzi

Saturday, November 13, 2010

Spika mpya mama Makinda


MHESHIMIWA ANNE MAKINDA NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE BAADA YA KUMSHINDA MH. MGOMBEA MABERE NYAUCHO MARANDO KATIKA UCHAGUZI WA KUMPATA SPIKA MPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.


Idadi ya kura zilizopigwa = 327
Idadi ya kura zilizoharibika = 9

Mabere Marando amepata kura 53
Anna Makinda amepata kura 265

Wednesday, November 10, 2010

CCM WAFANYA MAPINDUZI WAWAPITISHA MAKINDA, ANNA ABDALLAH, KATE KAMBA USPIKA

Anna Makinda
Anna Abdallah
Kate Kamba
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.

Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.

Uzinduzi wa TV ya Sony 3D


Mkurugenzi Mkuu wa Sony Osamu Miura (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mauzo Afrika Mashariki Dinakaran Munaswamy (wa pili kulia) wakizindua TV ya Sony 3Djijini Nairobi leo.

Managing Director, Sony Gulf Mr. Osamu Miura(right) accompanied by a Sony model unveil the Sony 3D TV.

Managing Director, Sony Gulf Mr. Osamu Miura (second left) and East Africa Head of sales Mr. Dinakaran Munaswamy (second right) unveil the 3D Sony TV accompanied by Sony models.

Makamu wa Rais



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi Makamu wa Rais (Mazingira), wakati alipofika ofisini hapo kusaini kwa mara ya kwanza na kuanza kazi rasmi Nov 08. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel.( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Sunday, November 07, 2010

Rais Kikwete aapishwa aanza ngwe




RAIS Jakaya Kikwete jana aliapishwa kuiongoza Tanzania kwa kingine cha miaka mitano ijayo na kutoa wito kwa vyama vya upinzani kushirikiana na serikali yake katika kuimarisha demokrasia na kudumisha amani nchini.
Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu Augustino Ramadhan katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete ambaye alipata ushindi wa asilimia 61.17 ambayo ni chini zaidi ya ushindi aliopata mwaka 2005, alisema wapinzani waliifanya CCM kujituma zaidi na mahali pengine kulazimika kufanya kazi ya ziada wakati wa kusaka ushindi.
"Siwezi kuacha kuwatambua wagombea wenzangu sita tuliowania nafasi ya uongozi wa juu kabisa wa nchi yetu, nawashukuru kwa kutuchangamsha wakati wa kampeni, mmetufanya tujitume zaidi na mahali pengine tufanye kazi ya ziada.

Thursday, November 04, 2010

Vodacom yatangaza zawadi za Mwanza Cycle Challenge



Vodacom Tanzania imetangaza zawadi zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki mashindano ya baiskeli ambayo yatafanyika Jijini Mwanza mwezi huu yanayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza naWaandishi wa Habari, Jijini leo, katika makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi.

“Mashindano haya yameboreshwa kwa upande wa zawadi, ubora na viwango,” alisema.

Aidha alifafanua kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa siku mbili yaani Novemba 12 na 13 mwezi huu na kwamba tarehe 12 itakuwa maalumu kwa mashindano ya walemavu ambao watashindana kilometa 15 kwa wanaume na 10 kwa wanawake. Na tarehe 13 Novemba yatafanyika mashindano ya kilomita 196 kwa wanaume, 80 kwa wanawake ambapo kwa upande wa walemavu ni Kilometa 15 kwa walemavu wanaume na Kilomita 10 kwa walemavu wanawake.

Akitangaza zawadi hizo kwa washiriki wa mbio za kilometa 150 Mtingwa alisema mshindi wa kwanza atajipatia shilingi 1,500,000, wa pili kiasi cha 1,000,000, wa tatu 700,000, ambapo mshindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atajipatia shilingi 500,000 kila mmoja. Aidha kwa upande washindi wa 11 hadi 20 kila mmoja atajinyakulia kitita cha 250,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 90,000 kila mmoja.

Kwa upande wa mbio za mita 80 kwa wanawake mshindi wa kwanza pia atajipatia zawadi ya shilingi milioni 1,100,000, wa pili 800,000, mshindi wa tatu 600,000, wakati washindi wa nne hadi wa kumi kila mmoja atazawadia kiasi cha shilingi 350,000 kila mmoja. Vilevile washindi watakaoshika nafasi ya 11 hadi ya 20 katika mbio hizo watapewa jumla ya 130,000 kila mmoja, na kuanzia mshindi wa 21 hadi wa 30 watapatia shilingi 70,000 kila mmoja.

Mbali na hayo Mtingwa alibainisha kwamba kwa upande wa mbio za kilometa 10 ambazo zitawashirikisha watu wenye ulemavu alisema washindi wa kwanza wawili kila mmoja atajipatia jumla ya shilingi 400,000.

Kwa washindi wa pili wawili nao watajishindia kiasi cha shilingi 250,000 kila mmoja, washindi wa tatu wawili kila mmoja atapewa kiasi cha 150,000 kila mmoja wakati washindi wa nne wane hadi wa kumi watajipatia kitita cha 70,000 kila mmoja.

Wednesday, November 03, 2010

TEMCO: Wakuu wa mikoa na wilaya waliisaidia CCM kampeni



Mwenyekiti wa kamati ya uangalizi wa uchaguzi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (TEMCO) Profesa Rwekaza Mukandala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya awali ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambapo ripoti hiyo inaeleza kuwepo kwa mapungufu kwa baadhi ya maeneo ingawa inaeleza ulikuwa huru, kulia ni makamu mwenyekiti Temco Maryam Abubakar. Picha na Said Powa

*********************************************************************************

TIMU ya Waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu (Temco) imetoa tathmini yake ya awali kuhusu uchaguzi huo uliofanyika Oktoba31, ikionyesha kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya walikisaidia chama tawala katika kampeni zake.
Temco pia imeonyesha kuwepo kwa dalili za kuvunjwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi kutokana na baadhi ya vyama kutoa mabango mengi na vifaa vingine vya kampeni hizo vyenye gharama kubwa.
Katika taarifa yake hiyo ya awali mbele ya wanahabari jana Temco kupitia mkwenyekiti wake, Profesa Rwekaza Mukandala imetaja kuwepo kwa vitendo vilivyotishia uvunjifu wa amani na vurugu ikibainisha kuwa vyama vya CCM, Chadema na Cuf kuhusika.
“Mambo yasiyofaa yaliyobainishwa na timu ya waangalizi wa Temco si mageni, lakini yameonekana kuchukua nafasi kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu,”alisema Profesa Mukandala na kufafanua:
Wakuu wa mikoa na wilaya walitumia rasilimali za taifa kama magari katika kampeni za urais kumsaidia mgombea anayetetea nafasi yake.”
Mwenyekiti huyo wa Temco aliongeza kuwa mara kadhaa katika kampeni zake mgombea urais huyo alitumia nafasi yake kama kiongozi wa nchi kutoa au kubadili uamuzi wa serikali kama ahadi kwa wapiga kura ili kujipatia wapiga kura jambo ambalo wagombea wengine hawakuweza kulifanya.
Temko ilitembelea majimbo 135 kati ya 223 ikiacha majimbo ya uchaguzi ambayo wagombea wake walipita bila kupingwa na kutoa alama A mpaka E kwa majimbo.
Mukandala alisema kuwa mgombea kutoa ahadi si jambo baya lakini kutoa ahadi au uamuzi kutumia madaraka aliyonayo mtu ili kuvuna wapiga kura syo jambo sahihi.
Wakati wa kampeni za kuwania urais, ubunge na udiwani kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumapili iliyopita, vyama vya upinzani vililalamikia baadhi ya wagombea nafasi hizo kutumia nyadhifa zao kutoa ahadi kwa lengo la kuvuna wapigakura.
Akizungumzia uvunjaji sheria ya gharama za uchaguzi, mwenyekiti huyo wa Temco alisema kuwa, “Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kwanza kufanyika chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi uliolenga kudhibiti matumizi makubwa ya fedha, lakini kumekuwepo na vifaa vingi vya gharama kubwa kwa vyama vikubwa hasa chama tawala CCM.”...
Imeandikwa na Exuper Kachenje: SOURCE: MWANANCHI

Nyalandu aibuka na ushindi mnono



MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweza tena kurejea madarakani baada ya kuibuka na jumla ya kura 46,869 ikiwa ni asilimia 91 ya kura zote.

Nyalandu ambaye amekuwa mgombea ubunge wakwanza nchini kutumia helkopta katika kampeni aliwabwaga wapinzani wake Msaghaa Kimia kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipata kura 3,544 wakati Sizimwe Kanyota wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyepata kura 550.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa jana, Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Iliminata Mwenda alisema jumla ya wapigakura waliojiandikisha walikuwa 90,045 wakati waliopiga kura ni 46,869 katika jimbo hilo.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nyalandu alisema kuwa wananchi wa Singida Kaskazini wamempa heshima kubwa kwa kuonyesha kumwamini na kuwa yuko tayari kuendeleza mambo aliyoyafanya kipindi kilichopita na kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...