Anna Makinda
Anna Abdallah
Kate Kamba
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.
Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.
"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
4 comments:
Haya, akina mama msilale,lale lale akina mama msilale sasa kumekucha!
Yahaya Charahani
Haya siyo mapinduzi..ni kulindana...Nafikiri wajua mi ni nani..Tabora..then MCL IT
Hivi huyu mama Kate ni nani maana amekaa kifisadi kabisa hata hana mvuto...mpango wa kulindana ccm umekamilika
hawa wote wanafanyia kazi mafisadi, hasa huyu anna abdallah ametoka mbali alikuwa fisadi toka miaka ya sabini. cha ajabu yule fisadi wakisasa ambaye alikuwa mfungwa wa tuhuma za TFF leo mbunge wa taifa it only happens in TZ!!! msomali wa dom
Post a Comment