Thursday, April 19, 2007

Nini kisa cha kutumia fedha nyingi kujadili ubadhirifu?

POTELEA mbali, wakati mwingine ukweli inabidi uzungumzwe na hata kama unauma kiasi gani. Si bora hata kidogo kukaa kimya na kuchekacheka wakati mambo tukiyaona hayaendi sawa.

Hayaendi sawa sababu, kadiri siku zinavyoenda tunayaona yanajirundika, yanaongezeka, na kisha yanakuwa kama vile mazoea. Yanakuwa kama mambo ya kawaida kabisa kufanywa na wakuu wetu hawa wa nchi.

Tunawaheshimu sana na wakati mwingine tunawaonea huruma, kwa namna ambavyo wanakabiliana na maamuzi magumu kupita kiasi na mengine yanayokuwa yanazidi uwezo wa kibinadamu. Katika hayo tuko pamoja nao.

Lakini jamani hebu tufikirie, hivi wale wazazi wetu waliopo kule Nanyamba au Nachunyu au Nakasahenge na kwingineko wanavyotaabika ili kuhakikisha wanaendelea kuwapo katika dunia hii, wanaposikia haya yanayofanyika sasa wanajisikiaje! Bonyeza hapa

2 comments:

Mikundu Matako Makalio Manundu said...

Mzee wa Mshitu na wengineo, baada ya siasa piteni kwa Mzee wa Mikundu, mjifarij kidogo, nyeto ruksa:

http://mikundu.blogspot.com/

mloyi said...

Mtoa maoni hapo juu simuelewi analengo gani kuchukua jina hilo.
tuendelee,
Sijui kama wakati mwingine watu hawa kama wanabusara, baada ya kutumia TShs millioni 100. spika anatoa uamuzi usioeleweka kwa wabunge, nao wanaafiki, sijui kwanini alikubali jambo hilo kujadiliwa na baadae analifuta baada ya kuingia gharama ya kujenga madarasa kumi ya kisasa! sijui ni nini kilichomfanya afikie uamuzi huo, halafu hatuambiwi hizo pesa zilitumika vipi? ni pesa nyingi sana kwa nchi inayojiita "masikini" kama Tanzania. ni kashfa nzito sana, inafaa ajiuzuru kwa kushindwa kusimamia pesa za walipa kodi vizuri.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...