Monday, March 12, 2007

Kama tumekosa kauli, basi tunyamaze tusijiabishe

KAULI ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu yeyote awaye. Kauli yaweza kuchonganisha. Inaweza pia kufurahisha, kutoa matumaini, kuleta balaa wakati mwingine na hata kuleta madhara makubwa.

Kauli ndizo huweza kumtambulisha mtu na kutambua yukoje mbele ya wenzake. Huweza kuwafanya watu wengine watambue ni kiasi gani mtu wanayezungumza naye kaiva au kukomaa au vinginevyo.

Kwa jumla, kauli humchonganisha au kumkutanisha mtu na watu wengine. Kisiasa, kauli hujenga mtaji kwa mwanasiasa kukubalika na hasa kama anajua namna ya kuzipangilia hoja kimantiki, lakini hasa zikiwa zenye kubeba ukweli na uhalisia wa mambo.

Kwa kawaida, imezoeleka kuwa kauli nyingi zinazotoka midomoni mwa wanasiasa kuwa ni za uongo, huchukuliwa hivyo kwa sababu mara nyingi hutolewa ili kutumika kama chambo cha kuwavuta wananchi kuwachagua na kisha wakishawachagua wanawasahau. Lakini, si kweli wakati mwingine kuna ukweli fulani.Soma kwa urefu zaidi hapa

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...