Maisha ya skuli si mchezo kuna milima na mabonde, kuna miteremko vile vile hebu cheki hivi vijamaa vimejificha sijui vinaogopa nini, bila shaka vimetoroka kabla ya kuruhusiwa na mwalimu
Tuesday, August 12, 2008
Watoto shuleni
Maisha ya skuli si mchezo kuna milima na mabonde, kuna miteremko vile vile hebu cheki hivi vijamaa vimejificha sijui vinaogopa nini, bila shaka vimetoroka kabla ya kuruhusiwa na mwalimu
Sunday, August 10, 2008
Usafiri Dar
MWANANCHI COMMUNICATIONS YAZINDUA SURA MPYA YA GAZETI LA MWANANCHI KWA MBWEMBWE

Katika tukio lililojaa hamasa na uzalendo wa kitaaluma, baadhi ya wafanyakazi walionekana wakigongeana glasi kwa bashasha kama ishara ya kusherehekea mafanikio hayo makubwa ya kimkakati. Tukio hilo liliambatana na furaha ya mafanikio, ubunifu, na dhamira ya kampuni hiyo kuendelea kuwa kioo cha jamii na kinara wa habari za kuaminika nchini.
Sura mpya ya gazeti la Mwananchi inatajwa kuwa ya kisasa zaidi, yenye mvuto wa kimtazamo na urahisi wa kusoma, ikilenga kukidhi mahitaji ya wasomaji wa leo katika enzi ya kidijitali na ushindani mkubwa wa habari.
Katika picha iliyopigwa na Fidelis Felix, wafanyakazi hao walionekana wakiwa na nyuso za furaha – ushahidi tosha wa ari mpya ndani ya taasisi hiyo kongwe ya habari nchini Tanzania.
Thursday, August 07, 2008
msiba wa Kapteni Mazula
MAELFU ya waombolezaji katikati ya wiki hii walijitokeza kwa wingi katika kanisa la katoliki usharika wa St Martha mikocheni kuusindikiza mwili wa marehemu Kapt George Mazula
Miongoni mwa sifa za Marehemu Kapt Mazula ni kutumia muda wa masaa 17,640 kuruka na ndege angani wakati wote wa uhahi wake alioishi hapa duniani.
Mbali na kukumbukwa katika mengi lakini pia Kapt Mazula atakumbukwa kwa tija na ufanisi katika kazi huku akiweka mbele masilahi ya taifa kuliko kutafuta faida zake binafsi.
Katika uhai wake aliweza kutumia masaa 3,300 kuendesha ndege ndogo yenye uwezo wa kubeba watu 19,masaa 7,340 watu wasiozidi 50 na zaidi ya masaa 7,000 ndege za B737.
Marehemu Kapt Mazula alipata matatizo ya mgongo ambayao yalisababisha apelekwe India kwa matibabu ,mnamo julai 8 mwaka huu aliweza kufanyiwa upasuaji na kupata nafuu jambo lililopelekea aweze kurudishwa nchini julai 20.
Hali yake iliendelea vizuri hadi julai 30 mwaka huu alipoanza kupata mtatizo ya pumu kabla ya roho yake kutwaliwa agosti mosi majira ya saa nne asubuhi akiwa nyumbani kwake.
Marehemu Kapt Mazula amewaacha watoto wake wawili Brayan Mazula na George -Junior mazula wanaoishi nchini marekani pamoja na mke wake Hariety Mazula.
Akisoma wasifu wa marehemu Kapt Mazula mtoto wake Georgejunior anasema marehemu alizaliwa mwaka 1949 katika eneo la bwiru mkoani Mwanza,yeye akiwa ni mtoto wa nne kuzaliwa kutoka kwa wazazi wake Arbogasti na Maria Mazula.
Anasema alisoma katika shule ya msingi Tabora, kabla ya kuhamia shule ya Kangululi wilayani ukerewe mkoani mwanza.
anasema katika masomo yake ya sekondari Marehemu Mazula alisoma katika shule ya musoma collegge na baadaye mwaka 1970 alijiunga na shule ya sekondari ya Aga Khan Boys kwa masomo ya kidato cha tano na sita.
Georgemazula anasema mwaka 1973 Kapt Mazula alijiunga na benki ya taifa ya biashara alikofanya kazi kabla ya kujiunga na chuo cha urubani Saroti kilichopo nchini Uganda. Habari hii ya Peter Edson na picha zote ni za Perez Mwangoka wa Mwananchi.
Wednesday, August 06, 2008
Paschal Mayalla apata ajali
Pascal Mayalla akiwa katika chumba cha wagonjwa Daraja la kwanza katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako amelazwa kwa matibabu baada ya kupata ajali ya pikipiki juzi jioni katikati ya Ihumwa na Nzuguni nje kidogo ya mji katika barabara ya iendayo Morogoro. Kwa mujibu wa maelezo yake, amevunjika mkono wa kushoto ambao hauna mawasiliano na mwili uliosababishwa na kushituka kwa uti wa mgongo. Hata hivyo amepewa rufaa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo atapelekwa leo kwa matibabu zaidi. Picha na Jube Tranquilino.
Monday, August 04, 2008
Hafla ya kuzaliwa rasmi Zain
Sunday, August 03, 2008
Nasreem Karim Miss Vodacom
MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...




