Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk
Khamisa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa
Christian Omolo na ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa
Kongani ya Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu
fursa za ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.
Na.Mwandishi Wetu-ETHIOPIA
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali ya
Tanzania inaendelea kuweka Mazingira bora na wezeshi yanayovutia
wafanyabiashara kuja kuwekeza nchini hususani katika kuanzisha viwanda
ili kutiumiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayolenga kujenga
uchumi shindani na jumuishi wa viwand kwa lengo la kuongeza ajira na
pato la Taifa .
Waziri
jafo ameeasema hayo Novemba alipotembelea na kuzungumza na uongozi wa
Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern Industry Park) iliyopo Addis
Ababa, Ethiopia yenye jumla ya viwanda takribani 257 ikiwemo viwanda vya
chuma, nguo, na dawa na yenye nia ya kuja kuwekeza Tanzania kwa kujenga
Kongani kubwa ya Viwanda.
Waziri
Jafo akiwa ameambatana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango – Hazina, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia pamoja na wataalamu
kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara
katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) utakaofanyika Novemba 9-10,
2024, mjini humo ameikaribisha kampuni hiyo na kuahidi kuwa Wizara yake
kwa kushirikiana na Taasisi husika itaipa ushirikiano wa katika
kuanzisha kongani hiyo.
Naye
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kongani ya Viwanda ya Mashariki (Eastern
Industry Park) Bi Ma Futao amesema Kampuni yake iko tayari kuwekeza
Tanzania kwa kuwa mazingira ya ufanyaji biashara yanavutia ikiwemo Sera
nzuri za biashara, bandari na miundombinu ya barabara na reli ya kisasa
inayoinganisha na nchi jirani zisizo na bahari
Naye
Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amebainisha kuwa
Kongani ya Viwanda ya Eastern ikijengwa Tanzania itaongeza ajira
hususani kwa makundi maalum kama wananwake na vijana, pato la Taifa na
hatimaye kukuza biashara na uchumi kwa ujumla.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe
Dkt. Selemani Jafo (Mb) wakipeana mkono wa heri na Mmiki wa Kongani ya
Viwanda ya Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia Bw Bw.Lu Qixin mwenye
nia ya kuwekeza Tanzania baada ya kutembelea Kongani hiyo ambapo
amemkaribisha mwekezaji huyo kuja kuwekeza nchini ili kuongeza ujenzi wa
Viwanda ambavyo vitatoa ajira nyingi kwa watanzania na kujenga uchumi
wa nchi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe
Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na
ujumbe wa Tanzania wakitembelea viwanda katika Kongani ya Eastern
Industry iliyopo Addis Ababa, Ethiopia kujionea shughuli za uzalishaji
kwa Mwekezajih uyo mwenye nia ya kuwekeza Tanzania.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe
Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamisa, Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango – Hazina Bi Jenifa Christian Omolo na
ujumbe wa Tanzania wakijadiliana na Uongozi wa Kongani ya Viwanda ya
Mashariki iliyopo Addis Ababa, Ethiopia, kuhusu fursa za ufanyaji
biashara zilizopo Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini
Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi
Mwenza wa Kampuni ya Tirita General Trading ya Djibouti Bw. Abiy Araya
kuhusu fursa za ufanyaji biashara Tanzania katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania Addis Ababa, Ethiopia ambapo Dkt. Abdallah amemukaribisha
Mfanyabiashara huyo kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.