Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitiliana saini mkataba wa ujenzi wa jengo la Utawala na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata huku wakishuhudiwa Mkuu wa Huduma za Sheria wa Shirika la Nyumba laTaifa, Martin Mdoe Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akipeana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata baada ya kusaini mkataba huo.
Picha ya pamoja ya viongozi hao.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) leo limesaini mkataba na
Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Wangingómbe iliyopo Mkoani Njombe ya Ujenzi wa
Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.
Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo asubuhi katika Ofisi
za Halmauri hiyo na kuhudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Emmanuel Kirundo na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata na
watumishi waandamizi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi alisema ujenzi wa jengo hilo
unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja utaanza ndani ya wiki mbili
kuanzia sasa.
“Ni jengo litakalokuwa na ofisi nyingi za viongozi na
wataalamu wa Halmashauri na pande zote mbili tuko tayari kutekeleza majukumu ya
kimkataba,”alisema.
Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Emmanuel Kirundo alisema wameamua kulikabidhi Shirika hilo
dhamana ya ujenzi wa jengo hilo kubwa lenye nafasi ya kutosha kutokana na uwezo
lililo nao Shirika hilo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Athony Emmanuel Mawata
alisema wamepitia michakato mingi katika kumtafuta mkandarasi bora atakayejenga
jengo hilo na hatimaye wakafikia hatua ya kukabidhi ujenzi wa jengo hilo kwa
NHC kutokana na ubora wa kazi zilizokwishawahi kufanywa na Shirika hilo.
No comments:
Post a Comment