Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ambaye alikuwa Mwenyekiti akiwa na wenyeviti wenza wa Mkutano wa 37 wa Shelter Afrique wakiongoza ajenda
mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika
Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi ambaye alikuwa Mwenyekiti akiwa na wenyeviti wenza wa Mkutano wa 37 wa Shelter Afrique wakiongoza ajenda
mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika
Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Pius Tesha, akipitia
na kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa na Wajumbe kutoka
nchi 44 za Afrika waliohudhuria Mkutano huo uliofanyika katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi, akifuatilia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Windsor jijini Nairobi Kenya.
Tanzania
imeteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wa Mkutano wa 37 wa Makazi Afrika
(Shelter Afrique) kuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa 37 wadhifa ambao atautumikia kwa mwaka mmoja na kukabidhi madaraka katika mkutano utakaofanyika mwezi
Julai 2019 Jijini Rabat, Morocco. Mkutano huo ambao una wanachama kutoka
nchi 44 za Afrika walikutana katika jiji la Nairobi nchini Kenya ili kujadili changamoto za hali ya makazi kwa watu wa
nchi hizo ili kuona namna ya kutatua changamoto hizo kwa kutumia uzoefu
wa kila nchi mwanachama.
Aidha, katika Mkutano huo ambapo Tanzania
iliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa
William Lukuvi, iliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa 37.
Tanzania
ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32 wa Shelter -
Afrique uliofanyika N’djamena, Chad mwaka 2013 ulipitisha Azimio Namba
GM/2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la
kukuza mtaji wa kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika
masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika.
Shirika la Nyumba
la Taifa limenufaika na mtaji huo ambapo mwaka 2002 lilikopeshwa Dola za
Kimarekani 1.5 milioni na kuzitumia kujenga nyumba 212 eneo la Boko
Jijini Dar es Salaam na mwaka 2011 lilikopeshwa fedha kiasi cha Dola za
Kimarekani 14.5 milioni mkopo uliotakiwa kurejeshwa katika kipindi cha
miaka 10 na mkopo huo ulitumika kujenga nyumba za gharama nafuu zipatazo
558 katika maeneo mbalimbali nchini. Pamoja na kuikopesha NHC, Shelter
Afrique imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani 27,500,000/= katika
miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba nchini Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment