Saturday, July 28, 2018

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA RASMI NYUMBA 14 ZA MAKAZI ZA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makalla, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Nyumba hizo 14 zimejengwa katika Kata ya Lwangwa. Mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.1 ikiwa ni wastani wa sh. milioni 79 kwa kila nyumba. mradi huu wa Busokelo ulianza rasmi mwaka 2014 na na ulikakamilika mwaka 2015 kisha kukabidhiwa Machi 24, 2017. Hadi kukamilika mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na pesa hii imelipwa kwa awamu tatu zikiwemo baada ya kuweka sahihi katika mkataba, mwaka mmoja baada ya malipo ya awali na malipo ya mwisho ndani ya miaka minne. Makamu wa Rais amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya pamoja na Mkuu wa Wilaya kuharakisha mazungumzo ili maombi ya kujengewa nyumba 11 za watumishi wa Halmashauri hiyo yatimie.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makala na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Freddy Mwakibete wakishuhudia uzinduzi huo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi wakati akimpa maelezo kuhusu mradi huo wakati Makamu wa Rais alipokuwa akizindua nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni
Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.

 Umati wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni. Wengine ni Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Amos Makala na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Challya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Freddy Mwakibete wakishuhudia uzinduzi huo.
 Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.
Jiwe la msingi mbele ya Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo jioni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri ya Busokelo kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan

  Umati wa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika uzinduzi huo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akisalimiana na mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi huo leo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akisalimiana na Profesa Mark James Mwandosya mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi huo leo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...