Friday, May 18, 2018

WAZIRI LUKUVI, MWENYEKITI WA KAMATI NAPE WAMWAGA SIFA UTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. Katika Ziara hiyo Waziri Lukuvi amesifia kasi ya utendaji wa Shirika la Nyumba la TAifa huku Mwenyekiti wa Kamati wa Ardhi, Maliasili na Utalii akisema Shirika hilo ni mfano wa kuigwa kwa utendaji wenye viwango ikilinganishwa na mashirika mengi nchini.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi  akizungumza na Arden Kitomari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Margreth Ezekiel akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, maendeleo ya ujenzi wa jengo la biashara na makazi la Morocco Square linalojengwa na NHC Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
Msanifu wa Majengo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Robert Kintu akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, maendeleo ya ujenzi wa jengo la biashara na makazi la Victoria linalojengwa na NHC Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akielezea mbele ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii juu ya utendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa. Kamat hiyo ilifanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika.


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akiwaelekeza wajumbe wa kamati kuelekea kwenye mradi wa Morocco Square NHC jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Ardhi, Maliasili na Maliasili wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku moja ya miradi mbalimbali ya Shirika. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio katika ziara iliyofanyika leo mchana katika miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi  akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio katika ziara iliyofanyika leo mchana katika miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Manyama Maagi akiweleza maendeleo ya mradi wa Morocco Square jijini Dar es Salaam leo.
Jengo la Morocco Square linavyoonekana kwa sasa

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikagua miundombinu ndani ya jengo la Morocco.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...