MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA ARUSHA (AUWSA) WAANZA KUCHIMBA VISIMA NA KUSAMBAZA MAJI MJI WA SAFARI CITY
Meneja wa Mradi, Ndugu James Kisarika akielekezwa jinsi mtambo unavyofanya kazi na baadaye kuuendesha mwenyewe. Kama unavyoona eneo ni maji maji sana kwa sababu ya mvua nyingi. Hata hivyo, kitaalamu, hayo ndio mazingira yatakayotoa ukweli wa mazingira ya jengo litakalojengwa.
Meneja wa Mradi, Ndugu James Kisarika akielekezwa jinsi mtambo unavyofanya kazi na baadae kuuendesha mwenyewe. Kama unavyoona eneo ni maji maji sana kwa sababu ya mvua nyingi. Hata hivyo, kitaalamu, hayo ndio mazingira yatakayotoa ukweli wa mazingira ya jengo litakalojengwa.
Kikao cha makubaliano kiliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara, Ndugu William Genya, ambaye alitoa nafasi kwa pande zote mbili kutoa mawazo ya kuboresha maafikiano hayo muhimu kwa maendeleo ya Mji wa Safari City. Katika makubaliano hayo, Shirika la nyumba la Taifa litakabidhi kwa AUWSA visima vyake vitatu vya maji vilivyoko umbali wa Kilometa 3.8 hivi kutoka Safari City na AUWSA itaviendeleza kwa gharama zake na kuvuta maji ya visima hivyo kwa ajili ya kusambaza kwa wateja wa viwanja vya Safari City. Safari City itakuwa na wateja wa maji wa uhakika 4,500. Hiyo ni biashara kubwa kwa AUWSA. Aidha, AUWSA pia iliamua kujenga Makao Makuu yao ya Kanda yenye ghorofa 4 katika Mji wa Safari City, jambo ambalo tayari hatua za awali zimeshachukuliwa. Kwa upande wa NHC, makubaliano haya, yanatuhakikishia kwamba uendelezaji wa Safari City sasa ni mbele kwa mbele. Maji ni miundombinu muhimu kuliko vyote katika ujenzi na makazi ya watu.
Meneja wa Mradi, Ndugu James Kisarika, akitoa maelezo ya
kina kuhusu mradi wa Safari City kwa timu ya Wahandisi na Washauri(Consultants)
wa AUWSA
Wahandisi wa AUWSA na Washauri wanaoshughulikia ujenzi wa jengo la Makao yao ya Kanda. Pamoja Tunajenga Taifa Letu.
Mamlaka ya maji safi na majitaka, Mkoa wa Arusha, waanza kutekeleza makubaliano yaliofikiwa kati yake na Shirika la Nyumba la Taifa, kuhusu uvutaji na usambazaji wa maji katika Mji wa Safari City. Inayoonekana hapo juu na hapa chini ni mitambo yao ya kuchukulia sampuli za udongo ili kuweza kujua kama utaweza kubeba jengo kubwa la Makao Makuu yao ya Kanda
Comments