misururu ya magari mbali mbali iliyoleta wagonjwa na wasio wagonjwa kwenda kunywa dawa dawa ya Mugariga katika kijiji cha Samunge wilayani Loliondo, aliyooteshwa na Mzee Mwasapile mwaka 1991.
Mchungaji Ambikile Mwasapile akifuata dawa katika nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Samunge.Dawa hiyo ikishachemshwa huingizwa ndani na kuiombe kisha kuwanywesha wgonjwa.
Gari inayoonyesha namba za usajili SM, ni mali ya Manispaa ya Arusha. Gari hili ni moja ya magari ya Serikali yakiwa nayo yanasonga mbele kwenye foleni ya kunywa dawa inayogawiwa na mchungaji Mwasapile kwa kikombe abiria wakiwa humohumo ndani ya gari.
watu wakiwamo waasia mbalimbali kutoka Mkoa wa Arusha, Manyara na sehemu kadhaa za Tanzania na nje ya Nchi wakisubiri dawa ya Mugariga kwa ajili ya kujitibu.
*NI KWA MCHUNGAJI ANATIBU KISUKARI, PUMU, SARATANI NA UKIMWI
MAELFU ya watu, wakiwemo vigogo wa serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa nchini, wamefurika katika Kijiji cha Samunge Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata 'dawa ya maajabu ya Mungu' inayodaiwa kutibu magonjwa mengi sugu ikiwamo Ukimwi.
Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1,000 yakiwamo magari ya serikali, binafsi na mashirika ya kimataifa ikiwamo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, yamefurika katika kijiji hicho kilichopo umbali ya takriban kilometa 400 kutoka Jiji la Arusha.
Dawa hiyo, inatolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76), ambaye anasema alioteshwa na Mungu kuitumia kutibu tangu mwaka 1991.
Mchungaji Mwasapile ambaye alifanya mahojiano na Mwananchi Jumapili nyumbani kwake wakati akiendendelea kutoa dawa kwa wagonjwa wake, anasema ndoto hiyo aliendelea kuota mara kadhaa hadi Agosti 26 mwaka jana alipoanza rasmi kutibu.
Anasema dawa hiyo inatokana na mti aina ya mugariga na yeye pekee ndiye anaweza kukupatia na kunywa kikombe kimoja pekee na ukinywa tu inaanza kazi ya kutibu maradhi sugu ya ukimwi, kisukari, pumu na saratani.
Mchungaji Mwasapile anasema gharama za dawa hiyo ni Sh500 tu na dozi yake ni kikombe kimoja tu na hairuhusiwi kurudia kuinywa. Kabla ya kukamilika mchungaji huyo huiombea dawa hiyo na kuichemsha katika majisafi.
“Mungu ameniotesha kutoa dawa hii kwa Sh 500 aliponiambia hata mimi nilishangaa. Kwanza aliniambia niwape watu wapone saratani, kisukari, pumu na magonjwa mengine na baadaye akanionyesha kuwa dawa hii niwape hata wagonjwa wa ukimwi na watapona,“ anasema Mwasapile. Habari hii imeandikwa Mussa Juma na Daniel Sabuni, Loliondo.
Habari zaidi waweza kubonya hapaUpate tukio hilo kwa kina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
4 comments:
Jina la kisayansi la huo mmea ni lipi? Je watu wa utafiti wameshaanza utafiti?
mchungaji anajua kuchunga siri ya dawa yake, maana unakunywa hapohapo hakuna kuondoka na sampuli mkatengeneze 'patent= trade mark ' ulaya mvune mamilioni.
Duh, ama kweli angekuwa mroho angeshatajirika!
uongo mtupu
Post a Comment