Thursday, April 26, 2007

Muungano oyeeeee!!!


Katika hali ya kawaida na hasa kwa vijitaifa vyetu hivi vichanga vya dunia ya tatu ni nadra sana kwa waheshimiwa walioshika mipini ya visu kama hawa kukaa na kucheka hivi, hebu mtizame Maalima Seif, Lipumba na kisha mzee mkali na kina Saleh Pamba walivyokenua meno, hapa ni katika sherehe za sikukuu ya muungano. Picha ya Deus Mhagale.

Thursday, April 19, 2007

Nini kisa cha kutumia fedha nyingi kujadili ubadhirifu?

POTELEA mbali, wakati mwingine ukweli inabidi uzungumzwe na hata kama unauma kiasi gani. Si bora hata kidogo kukaa kimya na kuchekacheka wakati mambo tukiyaona hayaendi sawa.

Hayaendi sawa sababu, kadiri siku zinavyoenda tunayaona yanajirundika, yanaongezeka, na kisha yanakuwa kama vile mazoea. Yanakuwa kama mambo ya kawaida kabisa kufanywa na wakuu wetu hawa wa nchi.

Tunawaheshimu sana na wakati mwingine tunawaonea huruma, kwa namna ambavyo wanakabiliana na maamuzi magumu kupita kiasi na mengine yanayokuwa yanazidi uwezo wa kibinadamu. Katika hayo tuko pamoja nao.

Lakini jamani hebu tufikirie, hivi wale wazazi wetu waliopo kule Nanyamba au Nachunyu au Nakasahenge na kwingineko wanavyotaabika ili kuhakikisha wanaendelea kuwapo katika dunia hii, wanaposikia haya yanayofanyika sasa wanajisikiaje! Bonyeza hapa

Monday, April 16, 2007

Miss Universe Tanzania


Miss Universe Tanzania, Flaviana Francis Matata, katika pozi baada ya kuvishwa taji hilo juzi kwenye Hoteli ya Movenpick Dar es Salaam. Hongera kwa ushindi huu mdogo wangu.

Thursday, April 12, 2007

Shule

Shule yetu nzuri.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kibogwa, tarafa ya matombo mkoani Morogoro wakiwa darasani. Mazingira duni ya kusomea kama haya, yatasababisha taifa kushindwa kutimia kwa malengo ya usawa katika elimu. Picha hii ni kwa hisani ya ndugu yangu Mathew Kwembe.

Wednesday, April 11, 2007

Mchikichini

Sokoni Mchikichini mambo sasa shwari ni kwa wale wafanyabiashara waliohamishwa Mitaa ya Kongo,Swahili, Aggrey na kadhalika.

Friday, April 06, 2007

Mbadala wa RVF



Kutokana na ongezeko la ugongwa wa homa ya bonde la ufa hivi sasa kuku ay vyuku vinalika ile mbaya, hapa lori lililojaa vyuku likiingia mjini. Picha ya Fredrick Felix.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...