Friday, May 05, 2006

Hongera sana Waziri MK

JAMANI msishangae hii templeti ya blogu yangu nimeipata wapi, siyo ufundi wangu ni utundu, ugunduzi, kipaji na sijui tuseme nini cha ndugu yangu MK ambaye kupitia rafiki yangu Makene, ameweza kufanya mamboz bureeeee! Sikununua mimi, nilichofanya nilipokutana na Waziri MK nilizungumza naye mtandaoni na kisha baada ya muda nikaona kama miujiza vile mambo yakabadilika!
Nakupa pongezi ndugu yangu MK, Mungu akujaalie ujasiri huu huu wa kutuinua wabongo wenzako hivi sasa. Blogu zetu zina touch ya kibongo zaidi. Nilitamani sana blogu zetu ziwe zinalenga lenga maisha yetu kule bushi kwani hayo ndiyo maisha yetu hayo. Nirudie tena hongera saana ndugu yangu MK sijui tukupe nini!

5 comments:

boniphace said...

Charahani huyu MK ni kiboko na wale watoto wanaoiga mambo ya utaalamu wa kompyuta nimegundua kuwa wachanga sana. Sasa haya mavipaji kama ya akina MK ni lini tutayarejesha home na kuyapa uwezo wa kufungua makampuni ya kutengeneza software au kompytuta kabisa ikiwezekana na magari hapo Tanzania? Tunapaswa kutazama upya.

Mija Shija Sayi said...

Yaani anajenga halafu anagawa bure, anajenga anagawa bure...!! huyu jamaa ana roho nzuri sana.

Ndesanjo Macha said...

Mzee, hongera sana kwa nyumba mpya. Nataka kuona "document" za kihamba chako!!! (natania).

Vempin Media Tanzania said...

Makene, Mija na Ndesanjo nashukuruni sana kwa kunitembelea katika hiki kibanda changu, japo mmeishia sebuleni tu, (natania) nashukuru sana, lakini wa kumshukuru zaidi ni bwana MK, huyu bwana siwezi kumsahau kwa uwezo, ukarimu na sijui niseme nini!

Reggy's said...

Acha MK aitwe Waziri wa teknolojia. Anafaa sana. Ana moyo mzuri ajabu, mimi alinipigia hata simu, tukaongeza zaidi ya dakika tano,wakati anafafanua jinsi gani anaweza kuboresha jumba langu. Naamini limekuwa bora zaidi, ingawa sikutaka kupoteza 'originality.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...