Thursday, May 04, 2017

WAZIRI LUKUVI AMTUMBUA AFISA MIPANGO MIJI LINDI



 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza kuhusu utaratibu za upangaji miji  na umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
 Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi akijieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mafaili katika masijala ya ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini mapungufu ya kutokuwa na usahihi wa uwekaji kumbukumbu za ardhi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi mkoani Lindi
Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Lindi
Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa  na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.
Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji. 
 “Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo” .
katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.
Pia alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.

Wednesday, May 03, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA , ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI (TPC)

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo Kutoka  kwa,  Afisa Utawala wa TPC aliyeshika kofia  Bwana Jafari Ally  kuhusiana  na Shughuli zinazo endelea katika kiwanda cha Kutengeneza  Sukari  cha TPC  , Kushoto kwa Waziri Mkuu  aliyevaa shasti jeupe ni Meneja wa kiwanda  Bwana  Pascal Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni.
 Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa, akipata maelezo  Kutuko  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha (TPC) Bwana Robert  Baissac,  kuhusu mbegu za kisasa za Miwa zinazozalishwa  kitika  Shamba Darasa  la Kiwanda cha Sukari cha TPC Kilichopo  Mkoani Kilimanjaro Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo  kutoka kwa  Meneja wa Kiwanda cha Sukari (TPC) Bwana  Pascal Petiot  kuhusiana na Mitambo Mipya ya Kompyuta ambazo zimefungwa  ili kuongeza Ufanisi Katika Kiwanda  cha TPC Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
 Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa,  akiangalia Mitambo  mipya   inayofungwa  katika Kiwanda cha   kutengeneza  Sukari  cha  TPC, Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisalimiana na kiongozi wa Chama  cha Wafanyakzi  wa kiwanda cha Sukari  TPC (TASIWU)  Bwana Bilali Omari, waliopo katikati aliyeva  Tisheti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPC  Bwana  Robert  Baissac na Meneja wa Kiwanda hicho Bwana  Pascal  Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni. PICHA NA PMO

MKUU WA MKOA WA MWANZA AHITIMISHA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.
Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
#BMGHabari
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.

WAANDISHI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI


Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja,mshikamano na maendeleo na siyo uchochezi ili kujenga jamii bora.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison George Mwakyembe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Dkt. Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo siku hiyo huwa maalum kwa wadau wa tasnia hiyo kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni njia ya kujenga jukwaa la ushirikiano.

“Uhuru wa habari una ukomo wake hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari hapa nchini kuajiri watu wenye taaluma hiyo kwa kuachana na makanjanja ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Alizidi kufafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.

Aidha aliitaka Idara ya Habari (MAELEZO) kuwa na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia nzima ya habari nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi alisema uandishi wa habari si biashara ya kawaida bali ni kazi yenye kuhitaji uweledi mkubwa hivyo waandishi wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uandishi.

WAZIRI LUKUVI AZINDUA MPANGO KABAMBE MTWARA

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa ukamilifu.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri ili kuepusha migogoro ya ardhi..
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa Mpango Kabambe Mkoani hapo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego (wakwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza kulia), Mwenyekiti wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa katika uznduzi huo.
 Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . Katika shughuli hiyo Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda.

Katika ziara hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara  na watanzania kwa ujumla.

Katika uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi. Imaculate Senje ameeleza kuwa uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au koundoa kabisa tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara, na kuchochoea fursa za uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara kufuata mpango huo kwa maendeleo ya taifa.

Pia Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza kuwa dira ya mpango kabambe huo ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa mafanikio ambao hutoa kazi na fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.

Afisa huyo ameeleza mpango huo umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe na Ziwani ukigusa huduma zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na shughuli za kiuchumi yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya kuwasili mkoani humo.

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...