Monday, June 02, 2014

Marehemu Amina-Zahara Shabani Mtengeti azikwa Kisutu, Dar es salaam


 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilali, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine na waombolezaji wakiwa katika mazishi ya marehemu Amina-Zahara Shabani Mtengeti katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam jioni hii. Marehemu, ambaye ni mdogo wa Hajat Mwantumu Malale, Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi Radhia Msuya, alifariki jana
 Shughuli za mazishi zikiendelea
 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib Bilali akiweka udongo kaburini
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiweka udongo kaburini
 Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman akiweka mchanga kaburini
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Mecky Sadick akiweka mchanga kaburini
 Viongozi, ndugu, jamaa na marafiki wakiweka udongo kaburini
 Balozi Juma Mwapachu akiweka udongo kaburini
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Philip Mangula akiweka udongo kaburini
Ndugu, jamaa na marafiki wakiweka udongo kaburini.
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

WAHARIRI NA WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA KISIWA CHA SAANANE JIJINI MWANZA


Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakitoka katika lango la ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane tayari kuelekea kisiwani
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habariwakiwa katika boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha  TBC 1,Ben Mwaipaja akiwa ameshika jembe lake tayari kwa ajili ya kuchukua matukio.
Safari ilikuwa ni ya takribani dakika 15 hadi 20.
Hatimaye Watalii hao wa ndani wakafika katika Kisiwa cha Saanane.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakikaribishwa na Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saanane Patricia Mtenga.
Safari ya kuelekea katika eneo la kuanzia ziara ya kitalii katika Hifadhi hiyo ikaanza.
Baadae Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakapata historia ya Hifadhi hiyo kutoka kwa Muongoza Watalii Fua Hamis.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo ya mhifadhi Fua Hamis(Hayupo Pichani)
Safar ya kutembelea maeneo mbalimbali katika hifadhi hiyo ikaanza.
Moja ya eneo ambalo liliwavutia Wahariri hao ni eneo hili ambalo unatazama Taswira ya Ziwa Victoria vyema.
Safari iliendelea.
Eneo hili linajulikana kama Jiwe la Kuruka na hapa Mkuu wa Idara ya Ikolojia na Ulinzi katika HIfadhi hiyo Donates Bayona namna ambavyo watalii wa ndani wamekuwa wakifurahia kupata Taswira za Mawinguni wakiwa katika Jiwe hilo.
Baada ya kupita katika maeneo mbalimbali Safari ya Kurudi ikaanza.
Wakati Safari ya kurudi ikiendelea bahati mbaya Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA ,Ibrahim Mussa aliteguka mguu baada ya kukanyaga vibaya jiwe hali iliyopelekea kupatiwa huduma ya kwanza.
Baada ya kufikishwa katika eneo la Mapumziko ndiko kukafanyika taratibu za kupelekwa Hosptali kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hatimaye akapelekwa Hosptali.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa jijini Mwanza.

MWILI WA MAMA YAKE MBUNGE WA KIGOMA ZITTO KABWE WASAFIRISHWA KWENDA KIGOMA


Zitto Kabwe akiwa na Prof  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki jana kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi

Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe

Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi
Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko
Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport
alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe
PICHA NA Dj Sek Blog

MAKAMU WA RAIS DKT. BILA AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA NCHI MAJIRANI ZA UMOJA WA KUDHIBITI SILAHA NDOGO (RECSA)

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima, akizungumza wakati wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Maalum wa tatu wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Nchi Majirani zinazounda Umoja wa kudhibiti Silaha ndogo (RECSA), uliofanyika mchana kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Umoja huo unaundwa na nchi 15 ambazo  ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Shelisheli, ElitreaAfrika ya Kusini, Jibuti na Afrika ya Kati.
  Baadhi ya wadau na washiriki wa mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano huo  kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Aung'uruma Mbulu,Maelfu Wajitokeza

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali. Katibu Mkuu alisisitiza serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote waliojichukulia mali ya serikali bila utaratibu hasa nyumba za madaktari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakijiji cha Bashei ambao walimueleza kuwa wanalima sana kitunguu saumu lakini soko si zuri na kumuomba awasaidie kutafuta soko la kdumu, tatizo jingine ni ucheleweshaji wa kujenga bwawa la maji, Katika ziara hizi za Katibu Mkuu wananchi wamekuwa na imani kubwa na CCM kwa ushirikiano wanaoupata kwani majibu ya maswali yao yanakuwa ya kuridhisha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji ,pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini.

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...