Saturday, October 27, 2018

WAZIRI LUKUVI ALITAKA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC KUWA MFANO KATIKA KUSIMAMIA NYUMBA ZAKE

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akitia saini kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi ya NHC mkoa wa Kilimanjaro huku Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akishuhudia.
Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akisoma taarifa ya utekelezaji wa NHC mkoa wa Kilimanjaro mbele ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa na wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro.
wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.

Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akisoma taarifa ya utekelezaji wa NHC mkoa wa Kilimanjaro mbele ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na wafanyakazi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi amelitaka shirika la nyumba la Taifa (NHC) liwe mfano katika ujenzi, kuhifadhi na kutunza nyumba zake pamoja na kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wananchi.

Waziri Lukuvi  alisema hayo leo alipotembelea ofisi za shirika hilo katika mkoa wa Kilimanjaro akiwa katika ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same.

Alisema NHC lazima iwe mfano kwa taasisi nyingine katika ujenzi  wa nyumba bora na kuwapangisha wapangaji  kwa kipindi cha mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha watu kwa kipindi cha miezi sita au mwaka mmoja sambamba na kuepuka vishoka katika upangishaji nyumba zake.

Aidha, amelitaka shirika la NHC kuwa na mkakati maalum wa kukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika vitovu vya miji lakini zikiwa  zimechoka na kusisitiza kuwa asingependa kusikia shirika hilo linakuwa na nyumba mbovu.

Amelitaka shirika la nyumba la taifa kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana na halmashauri  zote nchini  kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi  pamoja na kujitangaza katika shughuli zake kwa kuwa  lina kampuni imara ya ujenzi yenye wataalanu na inayoweza kujenga majengo mbalimbali kama vile  shule,hospitali, vituo vya afya, vituo vya afya, vyuo na majengo ya watu binafsi.

Lukuvi amelitaka shirika kuimarisha kitengo cha huduma kwa wateja na kutembelea wateja kwa lengo la kujua matatizo ya wapangaji katika nyumba zao ili kutatua kero zao.

Kwa upande wake Meneja wa NHC mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba alimueleza Lukuvi kuwa Shirika lake limekuwa na ushirikiano na halmashauri katika mkoa huo na tayari wameshaanza majadiliano kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika halmashauri ya Manispaa ya Moshi kujenga jumla ya nyumba ishirini na tano.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...