Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akimkabidhi cheti cha shukurani ya udhamini Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Mwanza, Joseph John kwenye ufunguzi wa maonyesho wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu. NHC lilidhamini kiasi cha shilingi milioni tano.
Cheti cha udhamini kilichokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo yaliyofanyika viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho
ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda
mti mara baada ya kufungua Maonesho ya
Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akijadiliana jambo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mkakaro wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, akijadiliana jambo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Rhobi Wambura wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, akijadiliana jambo na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mwanza, Joseph John na Afisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mkakaro wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO kuweka mikakati ya kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuanzisha vituo katika ngazi ya halmashauri za wilaya ili kuwafikia wajasiliamali wengi zaidi, kuwajengea uwezo, kuwapa miongozo bora ya namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija na kuwaunganisha na taasisi za fedha waweze kupata mikopo.
Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo amesema umefika wakati kwa SIDO kutilia mkazo sekta ya viwanda na hivyo kuifanya jukwaa la kuwakutanisha wabunifu pia kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika matumizi ya teknolojia rafiki na rahisi zitakazoharakisha maendeleo ya viwanda nchini.
Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema SIDO inapaswa kujielekeza katika kubuni mashine , mitambo na teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza thamani ya bidhaa na kusisitiza kuwa kutokana na umuhimu wa sekta ya viwanda nchini katika kukuza ajira na kuongeza pato la taifa serikali itaendelea kuweka miundombinu wezeshi itakayoharakisha kasi ya ukuaji wa viwanda.
No comments:
Post a Comment