Friday, May 29, 2026

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Aungana na Waombolezaji Chato Katika Ibada ya Kumuaga Mama wa Hayati Dkt. John Magufuli

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea Marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, inayofanyika leo tarehe 29 Mei 2026.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili katika Viwanja vya Kilimani vilivyopo Wilaya ya Chato mkoani Geita, ambapo ameungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli.

Marehemu Bi. Suzana Magufuli ni mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Ibada hiyo ya kuaga na kumuombea marehemu inafanyika leo tarehe 29 Mei 2026, ikiibua hisia za majonzi na heshima kubwa kutoka kwa viongozi wa Serikali, familia, pamoja na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushiriki tukio hilo la maombolezo.

No comments:

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Aungana na Waombolezaji Chato Katika Ibada ya Kumuaga Mama wa Hayati Dkt. John Magufuli

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumu...