Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wauguzi wa zamu wa Wadi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine’s Day) ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. Taasisi ya Doris Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha, wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo, lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid (Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
Muwakiliwa wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Wakinamama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment