Saturday, November 26, 2011

Amavubi yawang'ata Kilimanjaro Stars bao moja bila

Kilimanjaro Stars
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwapungia mikoni mashabiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Mara baada ya kuzindua rasmi michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 ambapo leo michuano hiyo imekutanisha timu za Tanzania Kilimanjaro Stars na Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi, mpira umekwisha na timu ya Rwanda imeifunga Kilimanjaro Stars goli 1-0 , katika picha kulia anayecheka ni Rais wa TFF na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CACAFA Leodger Tenga.
Kikundi cha ngoma cha Mama Africa kikitumbuiza jioni ya leo kwenye uwanja wa taifa wakati timu ya Taifa Kilimanjaro Stars ilipopambana na Amavubi ya Rwanda na kuambulia kipigo cha bao moja bila.


Mashabiki wakifuatilia kwa karibu mpambano huo kati ya Kilimanjaro Stars na Timu ya taifa ya Rwanda wakati wa mchezo wao wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.

1 comment:

Anonymous said...

mimi binafsi namwona Leodgar Tenga kushoto ndio relevant zaidi ya huyu waziri mkuu ambae hatujui katoke wapi? Leodgar Tenga was one of best defensive player in bongo, people likr Hassan Gobos, mohd Bakari Tall,Jella Mtagwa ndio wangestahili kuwa viongozi sio takataka kama Ismail Aden, bongo bwana majasusi watupu. msomali wa dom

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...