Tuesday, January 11, 2011
Ninaugua kuongezeka uzito, nina kilo 300 sasa
UKISTAAJABU ya Musa, utayaona ya Firauni. Mambo mengine ni kama hadithi, lakini hii ni habari ya kweli, kwamba yupo mtu mwenye uzito wa Kilo 300 na zaidi, uzito unaoongezeka kila kukicha na kusababishi maumivu makali kwa mtu huyo.
Ni Tabu Kasidi mama wa makamo, mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa Tabata ambaye amejikuta akiongezeka uzito hadi kufikia hatua hiyo bila kujua chanzo cha hali hiyo. Mbaya zaidi ni kuwa uzito huo unaambatana na maumivu makali yanayotishia kukatisha maisha yake.
“Nikisikia maadhimisho ya kifo cha Nyerere na mimi nahesabu mwaka mwingine wa kukaa chini na maumivu makali, imekuwa sehemu ya maisha yangu kwani miaka 11 sasa nimeshindwa kupata ufumbuzi wa tatizo hili” anasema mama huyu akimaanisha kuwa ameanza kupata matatizo hayo kipindi kile Nyerere alipokufa.
Kasidi anasema tatizo hilo lilianza kama jambo la kawaida ambapo alianza kupata maumivu makali sehemu za kiuno na alikuwa akihisi kuvutwa na kitu kiasi cha kulazimika kukaa chini au hata kulala bila kujali mahali alipokuwa.
“Nakumbuka siku moja maumivu yalinipata nikiwa eneo la tabata relini, ambapo nililazimika kukaa chini katikati ya reli hali iliyosababisha wasamaria wema waje kunisogeza pembeni na kuniuliza sababu, lakini niliwaambia waniache kwa muda maumivu yatapungua na nitaweza kuendelea na safari yangu” anasema.
Anasema, wakati huo uzito haukuwa mkubwa sana Alikuwa na kilo 80 tu hali iliyomuwezesha kutembea kwa miguu yake na kuzunguka sehemu mbalimbali, huku akiendelea na biashara zake ndogondogo za kupika chapati, maandazi ili kuweza kujipatia riziki. Imeandikwa na Joyce Mmasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
3 comments:
Kuna vyakula vya aina nyingi vya kupuza uzito, Mshaurini kuvitumia ninyi mnao weza kuonana nae ana kwa ana! mfano,
Cabbage Soup Diet.
It is a radical weight loss diet involving consumption of low-calorie cabbage soup for seven days. Usually considered a fad diet, Cabbage soup diet is meant for short-term weight-loss. The typical diet is said to reduce 4.5 kg of weight in a week's time, however, nutritional experts claim that it is almost impossible to lose that much fat within a week. Thus, the weight lost is generally water.
Maziwa, grep fruits, kunywa maji na fresh juices! atembee tembee nk!
What's up all, here every person is sharing these kinds of knowledge, thus it's nice
to read this website, and I used to pay a quick visit this website
everyday.
Here is my webpage :: diet before and after
Hi, i believe that i saw you visited my blog thus i got here to go back the prefer?
.I'm attempting to find things to enhance my web site!I assume its ok to make use of some of your concepts!!
Here is my blog :: Neil Marcus
Post a Comment