Tuesday, May 08, 2007

Soma interview ya Flaviana Matata Mexico

Flaviana Matata akiwa Mexico













Hii ni sehemu ya interview hiyo iliyotafsiriwa

Miss Universe: Ni kipi unachokipendelea na kipi kinakuvutia zaidi?

Flaviana: Napenda sana mitindo. Mitindo ndiyo kitu kikubwa kwangu. Muziki pia ni kitu kinachonivutia pia.

Miss Universe: Unatarajia kuwa nani maishani mwako?

Flaviana Matata: Matarajio yangu ni kuwa Mhandisi na pia kuwa mwanamitindo wa kimataifa na mbunifu wa mitindo.

Miss Universe: Elezea umezaliwa na kukulia wapi na maisha yako utotoni yalikuwaje.

Flaviana Matata: Nilizaliwa mjini Shinyanga katika familia ya kawaida . Shinyanga ni mkoa unaofahamika nchini kwetu kwa utajiri wa madini hasa almasi na pia mengine mengi kama dhahabu na kadhalika.

Maisha ya utotoni mwangu yalijaa furaha na vicheko na nilipenda sana kuthubutu kujifunza vitu vipya kila siku iendayo kwa Mwenyezi Mungu. Na mara nyingi nilitembelea migodi nikiwa mimi na familia yangu na hata na marafiki.

Miss Universe: Unataka kipi majaji wa mashindano haya wakifahamu kutoka kwako?

Flaviana Matata: Mimi ni mtaalamu wa masuala ya umeme kitaaluma na pia ni mwanamitindo nchini mwangu. Sipendi watu wanielezee vingine aidha kwa mavazi yangu au kwa nywele kwa kuwa naamini Mungu hakukosea kuniumba kama mwanamke wa kiafrika. Picha ni za mtandao wa miss universe kwa maelezo zaidi Bonyeza hapa au hapa hapa

1 comment:

mwandani said...

Nimeipenda hiyo picha aliyopaka mafuta mengi.

UJUMBE WA MAAFISA KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA MISRI WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA TANZANIA

Leo, tarehe 23/04/2026 Makumbusho ya Taifa la Tanzania imepokea ugeni maalum kutoka Chuo cha Kijeshi Misri (Egypt War College) walioko katik...