Thursday, May 31, 2007

Breaking Newsss Flaviana





MWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya Miss Universe, Flaviana Matata amewasili nchini leo na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa nderemo, burudani kutoka kwa kikundi cha ngoma za asili cha Makumbusho Dancing Group.

Katika mashindano hayo, Flaviana alishika nafasi ya sita kati ya washiriki 77 kutoka nchi mbali mbali duniani.

Mratibu wa mashindano ya Miss Universe nchini, Maria Sarungi alikiri mashindano ya urembo ni bahati na kwamba pamoja na Flaviana kushika nafasi ya sita hakuwa na bahati ya kutwaa taji la dunia katika mashindano hayo.

Kutokana na kuingia 10 bora katika mashindano hayo, Flaviana ametwaa dola 500 za Marekani na kombe kutoka Kampuni ya Rogaska Crystal. Nachukua fursa hii kumpongeza Flavi huraaaaaa Mungu akujaalie usonge mbele zaidi na zaidi.

Mlimbwende wa Japan, Riyo Mori aliibuka kidedea katika mashindano hayo ambayo yalimalizika Jumatatu usiku mjini Mexico City, Mexico. PICHA IMEPIGWA FIDELIS FELIX

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...