Friday, February 16, 2007

Kasi hii ya sasa haitufai, tutafakari la kufanya

PANGA pangua. Hili huku, lile kule, chukua huyu hamisha peleka kule, yule weka hapa, mwingine fukuza, toa matamshi ya kila aina ya kutia matumaini ya ajabu na kisha mwisho wa siku mambo yanabaki kuwa yale yale na pengine mabaya zaidi.

Hii ndivyo ilivyo Tanzania yetu, kila anayekuja anakuja na lake, anajaribu kufanya majaribio na kisha anastukia muda wake umeisha basi anaondoka na kuiacha nchi ikiwa katika hali iliyo mbaya zaidi.

Serikali yetu ilianza kwa kujiunda Baraza lake la mawaziri ambalo lilikuwa kubwa kuliko yote tangu kupatikana kwa nchi hii, ukatolewa utetezi wa kila aina, lakini baadaye muda kidogo likapanguliwa. soma zaidi hapa kwa kubonya hapa

2 comments:

Ndesanjo Macha said...

Charahani,
mimi huwa napenda kusema kuwa nchi yetu inaongozwa kwa kauli mbiu. Kila anayekuja anakuja na kauli yake, kisha nchi nzima inaipokea na baadaye kuwa ni kama pambio fulani. Tunapumbazwa na kauli mbiu tupu.

Vempin Media Tanzania said...

ni kweli mzee hizi kauli mbiu wao wanadhani zinajenga kumbe zinabomoa hatuzitaki!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...