Tuesday, July 18, 2006


Waweza kujenga nyumba rahisi kama hii ingawa tatizo ni moto hebu tafadhalini naombeni kapsheni.


Mfanyakazi wa kujitolea raia wa Ujerumani, Scarlet Stirieber akimnywesha uji mtoto yatima, Athman katika kituo cha watoto yatima cha Ipamba kilichopo Tosamaganga Iringa hivi karibuni. Kituo hicho kina yatima 200. (Picha na Yahya Charahani)

4 comments:

mwandani said...

Charahani ndugu yangu uko kila mahala, tosamaganga mara sijui wapi... mara...

Hiyo nyumba hata mimi nimevutiwa sana, tabu ukikasirikiana na mtu hachelewi kutia kiberiti.

umezungumzia kituo cha yatima, nakumbuka kuwa ughaibuni sehemu nyingi kuna nyumba za watoto watukutu tu, nyumba za yatima nyingi zimetiwa kufuli.

Vile utoaji mimba ruksa, yatima atoke wapi. Wazazi wasioweza kupata watoto wanaenda kununua watoto sijui China, Ethiopia, Romania...

Usichoke kutupasha ya safarini.

Vempin Media Tanzania said...

Ni kweli ndugu yangu Tungaraza nyumba za watoto yatima ziko huku kwetu tu ambako wazazi ni irresponsible kupita kiasi wengi wanajua kuzaa tu lakini kulea wanakwepa ni ngumu sana hiyo.

Nafurahi sana kuliona hili la kutoka kila kona ninajaribu kubandika kila nachoona kina manufaa.

Ciao

Rashid Mkwinda said...

Ni nyumba rahisi kujenga lakini kama ulivyosema tatizo iwapo umekwaruzana na jirani ni hatari ya kugeuka majivu kwa kuunguzwa moto.

Halafu unajua kuzagaa kwa watoto hususana yatima na wa mitaani kunaweza kusababishwa na miundo mbinu hafifu ya fikra mbadala za serikali yetu ya Kidanganyika.

Hivi ni kweli tunashindwa kukabiliana na tatizo la watoto yatima ilhali tunazo rasilimali za kutosheleza, madini aina ya dhahabu, mito, maziwa na bahari ardhi panma yenye rutuba nk.

Mi nadhani kwa kuwa tumelalia masikio nnndio maana hakuna tulijualo, angalia sasa hadi watoto wetu wanageuzwa kuwa ni vivutio va kitalii hadi mzungu anakuja kutukebehi eti kwa kumlisha mmtoto yatima uji.

Sijui!!! lakini huu ndio ukweli wenyewe watoto yatima Wakidanganyika ni vivutyio vya utalii, waatu hufunga safari waatokako kuja kutembelea vituo vya yatima na kuangalia watoto wanaozagaa mitaani.

Hebu tumuulize Makene,MK,Ndesanjo, Fred Macha na wengineo walioko ughaibuni hivi huko hakuna vivutio vya utalii kama hivyo vya watoto yatima? mie ningefurahi siku moja nimuone Makene au Ndesanjo akiwa amepiga picha na mtoto wa mitaani aau yatima wa Kizungu halafu watupandishie katika Blogu tuichangie.

Anonymous said...

YATIMA NI MTOTO ALIYEFIWA NA WAZAZI AMA WOTE AU MAMA YAKE, HII NI TAFSIRI YA KISOMI, KWANI MTOTO AKIFIWA NA BABA TU HUWA HAITWI YATIMA KWA SABABU MAMA BADO YUPO, NA NI MAMA TU NDIYE ANAYEJUWA BABA WA MTOTO, NDO MAANA AKIFIWA NA ABA HUWA SI YATIMA, NI PALE TU ANAPOFIWA NA MAMA AU WOTE WAWILI NDIPO ATAITWA YATIMA, NA KWA LOGIC HIYO HUWEZI KUSEMA WAZAZI NI IRRESPONSIBLE KWANI HAWAKUPENDA KUFA, NI WALE TU AMBAO WANATELEKEZA WATOTO WAO WENYEWE WAKIWA HAI UNAWEZA KUSEMA WAKO IRRESPONSIBLE.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...