Wednesday, April 19, 2006

Huyu sijui ni Nyarubanja au vipi?

Haya tena kumekucha uwanja wa blogu unazidi kuvamiwa tena kwa nguvu ya ajabu, tunaye mwanablogu mpya kutoka hapa katika kijiji chetu cha Mwananchi, huyu si mwingine ni Midraji Ibrahimu, huyu kwa wasiyo mfahamu alishiriki kwa kiasi kikubwa kumpigia debe Mzee wa Standard and speed, lakini bahati mbaya akabwagwa katika kambi yake nyingine ya Mzee Malecela, waweza kumpata kwa kutembelea hapa

2 comments:

boniphace said...

charahani unafanya kazi kubwa sana hapo Tanzania kwa sasa. Unajua kimzaha mzaha tutakapoanza kutoa tuzo za Magazeti Tando Mwananchi itakuwa inabeba kila sekta wewe waache wajanja tujichukulie chati wao watafatia

Vempin Media Tanzania said...

Makene

Hilo umesema kweli huu ni wajibu wetu kwa kweli inabidi tuwachangamshe jamaa zetu wa hapa ili kusudi haya mapinduzi ya kweli ya sayansi na teknolojia yafike mbali kwa kasi.

Naona Ndesanjo ameshaandika makala kama tatu hivi kuhusu Blogu. Kazungumzia kwa kina sasa watu wajibu wao ni kuchimbua, makala zinaonekana kuwavutia wengi juzi wengine wamenifikia kuniuliza kumbe blogu ndivyo zilivyo bila shaka hawa nao wataingia mtandaoni muda si mrefu.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...