Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 28, 2026 amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 28, 2026 amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.
Na Jackline Minja MJJWM-Dodoma
Serikali imesema haina haja ya kuweka sharti la kisheria linalowalazimisha watoto kuwahudumia wazazi wao wasiojiweza, ikieleza kuwa suala hilo tayari linashughulikiwa kupitia misingi ya kifamilia na kijamii.
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa kinondoni Mhe. Tarimba Gulam Abbas lililohoji "Je Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kutunza wazazi wao wasiojiweza"?
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inatambua umuhimu wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kuwahudumia wazee, akisisitiza kuwa huo ni msingi wa mila na desturi za Watanzania.
Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee kupitia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2024, ambayo inasisitiza wajibu wa familia na jamii katika kuwahudumia wazee wao.
“Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kutunza wazee, kwani huu ndio msingi wa mila na desturi za Kitanzania na nguzo muhimu katika kujenga mshikamano wa kijamii," amesema
Amesema pia kuwa katika kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee, Serikali imefanikiwa kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na kuandaa toleo la mwaka 2024, ambalo linaeleza bayana wajibu wa familia na jamii katika kusimamia matunzo ya wazazi na wazee kwa ujumla, Sera hiyo pia imeweka msisitizo wa kuimarisha mifumo ya kisheria utakaolinda na kuendeleza ustawi wa wazee pamoja na watoto wanaowatunza.
Amsema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kutoa maoni juu ya masuala muhimu ya kuzingatiwa katika sheria hiyo.
Hata hivyo, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha maadili ya uwajibikaji wa kifamilia na kuimarisha mifumo ya kijamii inayosaidia ustawi wa wazee nchini.
Halmashauri ya Mji Ifakara Januari 27,2026 imetoa mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya Shilingi milioni 600 ikiwa ni Mikopo ya Asilimia 10 inayotokana na Mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa sera ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya mabasi kibaoni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felista Mdemu, ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo isiyo na riba.
Mdemu amevitaka vikundi vilivyonufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa, kuzingatia masharti ya mikataba, pamoja na kurejesha mikopo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kunufaika.
Shilingi 404,787,300 tayari imekwishatolewa kwa vikundi 41, vikiwemo vikundi 20 vya wanawake, 17 vya vijana na 4 vya watu wenye ulemavu na Shilingi 195,212,700 zitatolewa kwa vikundi 17 vilivyosalia mara baada ya kukamilisha maboresho yaliyoelekezwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Pilly Kitwana amewasihi wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuendelea kuunda Vikundi kwani pesa bado zipo ambazo zitasaidia kuwainua pia ameahidi kuendelea kufanya tathimini na ufuatiliaji kwa vikundi vilivyonufaika ili kuhakikisha mikopo hiyo inaleta tija na kuchangia maendeleo ya kiuchumi kwa wanufaika na jamii kwa ujumla.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Ziwa imefanya kikaokazi na Mameneja wa Kampuni za Bima zinazofanya shughuli zake katika kanda hiyo, kwa lengo la kuweka mikakati madhubuti ya kufikia wananchi wengi zaidi na kuongeza mchango wa sekta ya bima katika pato ghafi la kanda ya Ziwa.
Kaimu Meneja TIRA Kanda ya Ziwa, Bw. Oyuke Phostine, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya Mamlaka na Kampuni za Bima ili kupanua wigo wa huduma za bima.
“Bado kuna idadi kubwa ya wananchi katika kanda ya ziwa ambao hawajafikiwa na huduma za bima, hivyo kunahitajika mikakati ya pamoja ya elimu kwa umma, ubunifu wa bidhaa na matumizi ya teknolojia rahisi kuwafikia wananchi wa kada zote” alisisitiza Bw. Oyuke.
Aidha, kikao hicho kimejadili mikakati ya kuongeza pato ghafi la bima katika kanda ya Ziwa kwa kuimarisha mauzo ya bidhaa za bima zinazokidhi mahitaji halisi ya wananchi, hususan katika sekta za afya, kilimo, madini, ufugaji, uvuvi, biashara ndogo ndogo na usafirishaji.
Bw. Oyuke amewahimiza Mameneja wa Kampuni za Bima kuhakikisha wanazingatia viwango vya kitaaluma, maadili ya kazi na ufanisi katika kuhudumia wateja, ili kujenga imani ya wananchi kwa sekta ya bima.
Kikao hicho kimehitimishwa kwa makubaliano ya kuendelea kufanya usajili wa mawakala na mbinu mpya za usambazaji bima ili kutekeleza kwa urahisi mikakati iliyopangwa na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya wananchi na ukuaji wa sekta ya bima katika Kanda ya Ziwa.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo tarehe 27 Januari 2027, ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupanda miti katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili ba Utalii Dkt. Hassan Abbas ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika tukio hilo la upandaji miti wengine mbalimbali na wananchi, zoezi hilo la upandaji miti akiwa pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi, Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja na kutaka kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miti ikiwa na kauli mbiu ya “Uzalendo ni kutunza mazingira, Shiriki kupanda miti”
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 27, 2026 ameshiriki zoezi la upandaji miti, mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma.
Zoezi hilo ni sehemu ya hatua ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa vitendo vya kulinda mazingira.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu akiwa ameambatana na mwenza wake Mama Neema Mwigulu, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uongozi wake kwa kuendelea kudhihirisha namna alivyo kiongozi mwenye maono, mbunifu na anayejali maslahi mapana ya Taifa.
“Shughuli hii imekuwa na utofauti kwa kusababisha miti ipandwe kila kona ya nchi, kwenye vitabu vyetu vitukufu, kupanda mti ni moja ya ibada kwasababu wanufaika wa miti ni wengi”
Kadhalika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuadhimisha siku zao za kuzaliwa kwa kupanda miti. “Tunapokuwa na jambo la kukumbuka la aina hii, tufanye kitu ambacho kinaweka alama na manufaa kwa watu wengine”.
Mheshimiwa Waziri Mkuu amepanda mtu aina ya MDODOMA/MTIMAJI (Trichilia Emetica)
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akisafiri kwa Treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU, unaofanyika leo Januari 26, 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...