Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso E. Lenhardt kushoto akipata maelezo ya kipeperushi kinachoonyesha jinsi miundombinu ya Barabara ilivyoharibiwa vibaya na mvua zitokanazo na mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh.Dkt Batilda Salha Burian, alipotembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini dar es Salaam Leo
Monday, May 10, 2010
Balozi wa Marekani nchini Tanzania amtembelea Waziri Dr Batilda Burian
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso E. Lenhardt kushoto akipata maelezo ya kipeperushi kinachoonyesha jinsi miundombinu ya Barabara ilivyoharibiwa vibaya na mvua zitokanazo na mabadiliko ya Tabia Nchi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh.Dkt Batilda Salha Burian, alipotembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini dar es Salaam Leo
Miaka 20 ya Tawla
Baadhi ya wadau mbalimbali Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali zililokuwa zikitolewa na viongozi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya utendaji kazi wa TAWLA hapa nchini.sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Aron Msigwa-Maelezo na Amour Nassor -VPO)
Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akizinduwa Mpango Kazi kwa mwaka 2010/ 2015 wa Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA), kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Umoja huo yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja huo Bibi Victoria Mandele, kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki ya Mwanamke ni haki ya Wote.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanasheria Wanawake wa Tanzania (TAWLA) Bibi Victoria Mandale kutokana na kutambuwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza Umoja huo, katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya Umoja wa Wanasheria Wanawake Nchini (TAWLA)zilizoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam, kauli mbiu ya mwaka huu ni haki ya Mwanamke ni Haki ya Wote.
Sunday, May 09, 2010
Chelsea Ndio Mabingwa wa Uingereza

Wazee wa darajani Chelsea wamekatisha matumaini ya Manchester United kutwaa ubingwa wa Uingereza kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuunyakua ubingwa wa Uingereza kwa kutoa kipigo cha nguvu kwa Wigan kwa kuiburuza magoli 8-0.
KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA BBC
Fainali za Kiduku




Fainali ya mashindano ya kucheza mtindo wa taarabu unaoitwa KIDUKU (Pichani) ambao vijana wa kiume huvaa nguo za kike na kukata mauno kama wanawake ilifanyika Mei 2 huku shutuma kali zikiwaendea waandaaji wa mashindano hayo kuwa wana malengo ya kuwaharibu watoto wa kiume. Mtindo wa KIDUKU uliobuniwa na mtangazaji mahiri aliyekuwa akitangaza katika kituo cha televisheni ya Afrika Mashariki EATV, Maimartha wa Jesse umekuwa gumzo katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na jinsi mchezo huo ulivyo wahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 18.
Wengi wa vijana huwa ni watoto wa shule za msingi na sekondari wengine wakitokea tu mitaani kushindana kucheza mchezo wa Kiduku.
Hivi karibuni Maimartha aliandaa shindano la kumtafuta bingwa wa kiduku mwaka 2010 ambalo limewashirikisha vijana toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Miongoni mwa vikundi vinavyoshiriki ni Vidoleki, Mazombi, Wanaume fasti, Wakali wa kitengo, Wakupoteza, Stavanga na Mazombi.
Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alitarajiwa kupata zawadi ya dola 250, mshindi wa pili atapata music system na watatu wangeambulia feni. Fainali ya mashindano hayo ilifanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa Travertine uliopo magomeni.
Kwa upande mwingine wapenzi wa muziki wa taarab wamekuwa na maoni tofauti kutokana na vijana hao kucheza huku wakiwa wamevalia nguo za akina dada jambo ambalo wengi wanalihisi kuwa linaweza likawa ni njia mojawapo ya kuwapotosha vijana hao kwa kujiingiza katika njia ya uasherati ikiwa ni pamoja na kuwa mashoga.
Athumani Khamis arejea na kupokelewa na wadau
Mpigapicha wa gazeti HABARILEO, Athumani Hamisi (kwenyekiti) alirejea nyumbani Dar es Salaam leo akitokea nchini Afrika Kusini alikwenda Septemba 28, 2008 kwa matibabu kufuatia ajali ya gari aliyoipata Septemba 12 mwaka huo akiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi kikazi. Kushoto aliyeshika shada la maua ni muuguzi kutoka Afrika Kusini aliyemsindikiza.
KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA KWA MROKI
Saturday, May 08, 2010
Mnuso wa kuhitimisha mkutano wa uchumi
Rais wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katikati, Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma, Wazi Mkuu wa Kenya Mhe.RailaOdinga na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Dk. Salim Ahmed Salim, wakisakata Rumba katika Tafrija ya kukamilisha Mkutano wa Uchumi Duniani iliyofanyika jana katika Viwanja vya Ikulu Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akisakata Rumba na Bi Elsie Kanza kwenye Tafrija ya kukamilisha mkutano wa Uchumi Duniani iliyofanyika jana wa kuamkia leo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar
,
Mkutano wa Uchumi Duniani wamalizika

H.E. Jakaya M. Kikwete (President of the United Republic of Tanzania) and H.E. Jacob G. Zuma (President of the Republic of South Africa) at the World Economic Forum on Africa held in Dar es Salaam, Tanzania, May 7, 2010.

Klaus Schwab (Founder and Executive Chairman, World Economic Forum) and H.E. Jacob G. Zuma (President of the Republic of South Africa) at the World Economic Forum on Africa held in Dar es Salaam, Tanzania, May 7, 2010.

DAR ES SALAAM/TANZANIA, 7MAY10 - H.E. Jakaya M. Kikwete (President of the United Republic of Tanzania), Anna Tibaijuka (Undersecretary-General and Executive Director, UN-HABITAT, Kenya) and Katherine Tweedie (Head of Africa, World Economic Forum) at the World Economic Forum on Africa held in Dar es Salaam, Tanzania, May 7, 2010.KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA ukurasa huu
Subscribe to:
Posts (Atom)
NANENANE 2026: RAIS SAMIA ASISITIZA KILIMO CHA TIJA, MASOKO NA TEKNOLOJIA KUELEKEA DIRA 2050
Dodoma, Agosti 8, 2026 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kilele cha Maadhimisho ya Nanena...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...