Thursday, February 11, 2010

Ufukwe wa bahari Masaki wauzwa



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari katika eneo la wazi la ufukwe wa Bahari eneo la Masaki wakati wa ziara ya kutembelea wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. katikati ni Afisa mipango miji, Lucy Kimon (katikati) akifuatiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la uifadhi na usimamizi wa Mazingira-NEMC, Bonaventure Baya. Picha na Venance Nestory

Tamasha la Saba, Sauti za Busara 2010




HATIMAYE,kuna habari njema kutoka Zanzibar… Ukiachana na hali mbaya ya kiuchumi ya Dunia iliyoathiri bodi ya Utalii, na ukosefu wa umeme wa muda mrefu, tangu kati kati ya Disemba, hatimaye kuna mtazamo chanya juu ya Tamasha la saba la muziki la Sauti za Busara limefunguliwa rasmi leo na hivyo kung’arisha Zanzibar!
Tofauti na miaka iliyopita, Sauti za Busara 2010 linakuja na vionjo adhimu, zaidi ya wanamuziki 400 watapanda jukwaa moja. Mbali na vikundi kumi na mbili kutoka Zanzibar na nane kutoka Tanzania Bara, Tamasha hili pia limeshirikisha makundi ishirini kutoka nje ya Nchi kama vile Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Mozambique, Mayotte, Egypt, Guinea, Senegal, Gambia na Zambia.

Yatima wakabidhiwa misaada


Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Mkunde Senyagwa (kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya shule kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Tumaini Positive, Emmanuel Ndolimana (kulia) ikiwa ni sehemu ya mpango wa AICC wa uwajibikaji kwa jamii. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ofisi za kituo hicho cha yatima eneo la Kwangulelo, nje kidogo ya Mji wa Arusha. Waliosimama nyuma ni watoto wa kituo hicho na wafanyakazi wa AICC. (Picha kwa hisani ya AICC)

Babu Seya, Papii basi tena!!!

Babu Seya akisindikizwa Jela

Shangazi ya Babu Seya akilia kwa uchungu

WANAYE WAWILI WAACHIWA, YEYE NA PAPII NGUZA WAKWAMA

HUKUMU ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu leo hii imeibua vilio na majonzi baada ya kumtia hatiani mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Kongo, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza hivyo kuendelea kutumikia kifungo cha maisha jela.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaacha huru wanaye wengine wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika kuwa hawana hatia.

Babu Seya na wanaye, Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwatia hatiani kwa makosa ya kubaka na kuwalawiti watoto wa kike waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo walikata rufaa Mahakama Kuu ambako Jaji Thomas Mihayo (mstaafu kwa sasa), aliwatia hatiani na kuunga mkono hukumu ya Hakimu Mkazi Mkuu, Addy Lyamuya; kisha wakakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

Katika hukumu ya Mahakama ya Rufaa, iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Salum Massati , Mbarouk Mbarouk, wakiongozwa na Jaji Nathalia Kimaro waliosikiliza rufaa hiyo, iliyosomwa jana na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa (DRCA), Neema Chusi, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walitiwa hatiani, huku Nguza Mbangu na Francis Nguza wakiachiwa huru.

Wakati akitoka nje ya mahakama kuelekea gerezani, Babu Seya aliendelea kusisitiza kuwa hakufanya kosa hilo na asingeweza kufanya hivyo na watoto wake, huku mwanaye Papii Kocha akisema kuwa wanategemea huruma ya Rais Kikwete na kwamba, wana imani kuwa atawatoa.

Wakili wao Mabere Marando alisema, "Tumeshinda nusu, tumeshindwa nusu. Huo ni uamuzi wa mahakama na kuwa hajawa na mpango wa kuendelea zaidi ya hapo."

Akisoma hukumu hiyo, Chusi alisema mahakama imeridhika na ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kwa kila kosa na kwamba mrufani wa kwanza (Babu Seya) na wa pili (Papii Kocha), walihusika katika kutenda makosa na kwamba, utetezi wao kuwa hawakuwepo katike eneo la tukio ulikataliwa.


Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Rufaa, Babu Seya alitiwa hatiani kwa makosa matano ya kubaka na Papii Kocha alitiwa hatiani kwa makosa mawili, wakati Mbangu na Francis hawakupatikana na hatia kwa makosa yote.

“Mrufani wa kwanza amepatikana na hatia ya makosa mawili ya ubakaji kosa la 7 na la 12 kinyume cha kifungu cha 130 (2)(e) na 131A vya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) kama vilivyorekebishwa na vifungu vya 5 na 7 vya SOSPA (Sheria ya Makosa ya Kujamiiana),” ilisema hukumu hiyo na kuongeza:

Kwa kosa la 10 na 18 warufani namba moja (Babu Seya) na namba 2 (Papii Kocha) wamepatikana na hatia ya ubakaji kinyume cha kifungu cha 131A cha Kanuni ya Adhabu.

Hata hivyo katika kosa la 1,3,5,14, 20 na 22, warufani wote hawakupatikana na hatia, wakati katika kosa la 7 na 12 mrufani namba 1 mpaka namba 4 hawakupatikana na hatia huku kosa la 10 na 18 yakiwaondoa mrufani wa tatu (Mbangu) na wa nne (Francis).

“Hatimaye, hatia kwa mrufani namba tatu na wa nne inatanguliwa na hukumu pamoja na amri ya fidia inatupiliwa mbali. Wamewekwa huru isipokuwa kwa sababu nyingineyo. Na kwa mrufani wa kwanza na wa pili amri ya fidia bado inasimama tu kwa makosa ambayo yamewatia hatiani na inatupiliwa mbali kwa makosa yaliyobaki ambayo hayakuwatia hatiani,” ilisisitiza hukumu hiyo.

Mara baada ya Chusi kusoma hukumu hiyo majira ya saa 4:22 asubuhi, baadhi ya warufani hao waliangua kilio wakiwa kizimbani hususan Francis ambaye aliangua kilio kwa sauti kuu, huku Papii Kocha machozi yakimtiririka, lakini Babu Seya na Mbangu wakionekana kujawa na huzuni.

Chusi alianza kusoma hukumu hiyo kwa kuelezea kumbukumbu za mwenendo mzima wa kesi hiyo, akielezea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote katika kesi ya msingi, hukumu ya rufaa ya kwanza ya Mahakama Kuu na hoja zilizotolewa na pande zote katika rufaa zote.

Kisha alisema; “Suala lililoko mbele yetu sasa ni kama ushahidi katika kumbukumbu ulithibitisha utendaji wa kosa. Kama ambavyo tayari imeshaonyeshwa PW 9 (Shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka alikuwa ni mtoto wa miaka saba na alitoa ushahidi bila kiapo, ushahidi wake ulihitaji kuungwa mkono."

Katika ushahidi kwenye kumbukumbu hakuna mashaka kuwa PW9 alibakwa. Alithibitisha na kulikuwa na ushahidi wa PW20 kuwa PW9 alibakwa na PW9 alisema waomba rufaa ndio walimbaka.

Alisema jambo la msingi lilikuwa ni kuthibitsha kama waomba rufaa ndio walimbaka.

“Tumekwishatoa maoni juu ya mashahidi wa upande wa mashtaka na hatuhitaji kurudia kile ambacho tumekwishakisema. Inatosha kusema kwamba, kwenye kumbukumbu kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa watoto walikuwa na uwezo wa kuingia katika nyumba ile bila kuonekana,” alisema Chusi.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa hali ya nyumba iliyodaiwa kufanyika makosa yale kupitia kwa PW13, unaonyesha kuwa kulikuwa na mlango ambao ungeweza kutumiwa na watoto kuingia ndani ya nyumba ile namba 607 bila kuonekana.

Alisema kilichounga mkono ushahidi huo ni mazingira ya chumba cha mrufani wa kwanza (Babu Seya) ambamo ndimo kulimodaiwa kufanyiwa ubakaji, ambapo PW9 alieleza kuwa kuna godoro kitandani na godoro lingine ukutani na kwamba watoto wengine walikuwa wakilazwa kitandani na wengine kwenye godoro sakafuni.

“Tumesema mwanzoni mwa hukumu hii kuwa waathirika wa makosa ya ubakaji walikuwa ni watoto 10 na ushahidi wao katika maelezo yao kuhusu chumba cha mrufani wa kwanza unafanana,” alisema.

Akizungumzia utetezi wa Babu Seya kuwa alikuwa na matatizo ya nguvu za kiume na hivyo asingeweza kutenda kosa kama hilo na kwamba upande wa mashtaka ulikataa kwenda kumpima ili kuthibitishwa na daktari kama ana uwezo au hana uwezo wa kutenda kosa la ubakaji, mahakama iliutupilia mbali.

“Kwa maoni yetu upande wa mashtaka haukuwa na wajibu wa kufanya hivyo,” alisema Chusi katika hukumu hiyo na kuongeza:

“Tunasema hivyo kwa sababu katika kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Ushahidi (LEA) sura ya 6 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 suala la uwezo wa nguvu za kiume za mrufani ilikuwa katika ufahamu wake na suala la kuthibitisha lilikuwa juu yake kuthibitisha kuwa uume wake haukuwa ukifanya kazi”.

Mahakama pia iliongeza kuwa ingawa kulikuwa na mazoezi katika nyumba hiyo(wanamuziki wa Bendi ya Akudo) haikuwa sababu ya kumzuia mrufani wa kwanza kutenda makosa kwa kuwa, kwa mujibu wa ushahidi matukio hayo yalikuwa yakifanyika kwa muda mfupi sana wakati wa mapumziko na wakati watoto hao wakitoka shule.

“Zaidi hakuna sababu kwa nini watoto wote hao waseme uongo dhidi yake na alikiri kuwa hakuwa na uhasama na mmoja wapo,” iliongeza.

Kuhusu mrufani wa pili Papii Kocha, mahakama katika hukumu hiyo ilisema utetezi wake kuwa hakuwepo hauondoi uwezekano wa kutenda kosa.

“Tunasema hivyo kwa sababu kama ambavyo tumekwishaonyesha makosa yalikuwa yakitendeka kwa muda mfupi kama saa moja tu. Hii ina maana kwamba, hata kama mrufani wa pili alikuwa akifanya shughuli za kutumbuiza nje ya Dar es Salaam, lakini kuna wakati ambao alikuwa Dar es Salaam;

Kwa mujibu wa utetezi wake alikuwa akitoka nje ya Dar es Salaam kwa vipindi na si muda wote. Kwa namna hiyo hatuoni sababu yoyote PW8 ( mmoja wa watoto waathirika) kutengeneza ushahidi dhidi yake. Alikuwa ni mtoto mdogo ambaye hakujua hatari iliyokuwa mbele yake kwa kujihusisha katika, matendo ya ngono katika maisha yake”.

Katika hukumu hiyo mahakama ilichambua ushahidi wa kila mtoto na kueleza jinsi ulivyoweza kuungwa mkono na mashahidi wengine, wakiwemo madaktari waliowafanyia vipimo baadhi ya watoto hao na kuthibitisha kuwa walikuwa wameingiliwa.
SOURCE: MWANANCHI Imeandikwa na James MAGAI na HUSSEIN Kauli

Wednesday, February 10, 2010

Richmond kwisha kazi!!!



BUNGE limefunga rasmi mjadala wa mkataba tata wa Kampuni ya Richmond Development (LLC) na Tanesco na kuacha serikali iendelee kutekeleza maazimio yake huku wabunge wawili Christopher Ole Sendeka na Dk Willibrod Slaa wakipambana hadi mwisho.

Dk Slaa na Sendeka wakionyesha ujasiri katika mapambano, sehemu kubwa ya wabunge wakiwemo wanaojipambanua kupambana na ufisadi jana walionekana kumezwa na kushindwa kung'ara huku Kamati ya Nishati na Madini yenye dhamana na sakata hilo, ikionyesha utiifu mkubwa kwa maamuzi ya serikali.

Tofauti na ilivyokuwa kwenye mkutano wa 16 wa Bunge na viapo vya baadhi ya wabunge kutaka kufa na Richmond, mjadala huo wa taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya kampuni hiyo, ulianza kwa kupooza huku Mbunge wa Viti Maalumu (Ruvuma) Mhandisi Stella Manyanya, akiamua kuvirushia makombora vyombo vya habari na kusifia serikali na mawaziri wa serikali waliojiuzulu.

Lakini, Dk Slaa, ambaye alikuwa mchangiaji wa pili kwa mchana baada ya Juma Kilimbah, alianza kurusha makombora mazito akihoji ripoti kushindwa kubainisha mambo mengi ya msingi ambayo yalikuwemo kwenye taarifa kama hiyo iliyotolewa kwenye Mkutano wa 16 wa Bunge.

Kwa mujibu wa Dk Slaa, hakuelewa mantiki ya kukosekana majina ya watu muhimu waliopaswa kuwajibishwa kama aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini (Arthur Mwakapugi), kuachiwa hadi wanastaafu na wengine kutowajibishwa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mbunge huyo wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chadema, alihoji pia mantiki ya Kamati ya Nishati na Madini kumwacha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hoseah, kwa sababu nyepesi ya uchunguzi wa posho mbili unaofanywa na taasisi hiyo dhidi ya wabunge.

"Kuna mambo mengi ya msingi humu kwenye ripoti hayamo, kumwacha Hoseah kisa eti anafanya uchunguzi wa posho mbili dhidi ya wabunge ni jambo ambalo halina maana, kwa sababu hivi ni vitu viwili tofauti kabisa," alifafanua Dk Slaa.

"Kama ni uchunguzi wao kuhusu posho mbili waendelee na yeye kama ni kuwajibishwa hilo ni jambo jingine, kuliacha jambo hili katika mamlaka ya juu wakati Bunge ni chombo chenye nguvu na kushusha heshima ya Bunge."

Dk Slaa aliongeza kwamba, :"Uchunguzi wao waendelee kama mimi nimekula posho mbili wanichunguze waje wanikamate, lakini kuogopa uchunguzi wa Takukuru kuna walakini, nilikwishasema uchunguzi wa Takukuru usije ukafunga watu midomo."

Katika kuonyesha msisitizo, Dk Slaa aliweka bayana kwamba Dk Hoseah alionywa kwa kutokuwa makini na kutaka serikali ifafanue kama kosa hilo adhabu yake ya mwisho ni onyo au vinginevyo.

Mbunge huyo ambaye amejizolea sifa kutokana na kupambana na ufisadi, alihoji pia serikali kujaribu kusafisha hata wajumbe watano wa Timu ya Mashauriano ya Mikataba Serikalini (GNT), wakati walikuwa ni sehemu ya ushauri katika mkataba huo ambao uliitia serikali hasara.

Makombora hayo ingawa yalikuwa ya wabunge wawili, lakini yalitikisa Bunge, baada ya Sendeka kupata nafasi na kuhoji kama dhima za Bunge la kidemokrasia linavyoweza kufanya katika kusimamia rasilimali za taifa zisiporwe na watu mbalimbali wakiwemo wageni kwa kisingizio cha uwekezaji.

"Tumejiuliza kama mabunge ya wenzetu ya kidemokrasia yanafanya nini katika kusimamia rasilimali za taifa, sauti ya wanyonge na kupigania haki bila hofu na kufanya mambo kwa ujasiri?"
imeandikwa na Ramadhan Semtawa na Exuper Kachenje, Dodoma.

Kikwete mazishini kwa Mnikulu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa mnikulu marehemu Rajabu Kianda, huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro jana mchana.Marehemu Rajabu Kianda alifariki jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya kuugua shinikizo la damu na kupata kiharusi (picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto) akiwa na waumini wengine wakiuombea mwili wa marehemu RaJABU Kianda aliyekuwa mnikulu muda mfupi kabla ya mazishi yake huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro jana mchana.

Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu huko Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.

Tuesday, February 09, 2010

Wahariri wa Mwananchi wamvaa Spika


Spika wa Bunge, Samuel Sitta (kushoto) akisalimiana na Mhariri wa gazeti la
Mwananchi Jumapili, Daniel Mwaijega na Mhariri wa makala wa Mwananchi,
Rashid Kejo (katikati) walipotembelea Bunge mjini Dodoma jana. Picha na
Edwin Mjwahuzi

MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...