Thursday, October 01, 2015

WADAU MARA WAMHAKIKISHIA AMANI IGP MANGU

X1
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa Mkoa wa Mara wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo jana.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
X2
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen wakati walipokutana jana .IGP yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa huo kukagua utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.
X3
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Zeletho Stephen akizungumza katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
X4
Baadhi ya wadau wakichangia mawazo katika kikao cha wadau wa amani mkoani Mara kilichohudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.
…………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wadau wa Amani mkoani Mara wamemhakikishia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kuendelea kuitunza amani  na kuimarisha  usalama katika mkoa huo hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
Waliyasema hayo wakati walipokuwa wakitoa maoni yao wakati wa kikao kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa amani mkoani humo wakiwemo Wanasiasa, Viongozi wa Uchaguzi, Wagombea, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini, Wazee wa kimila na Viongozi wa dini mkoani humo.
Walisema mkoa huo umekuwa shwari hasa baada ya kuundwa kwa Kanda maalumu ya kipolisi ya Tarime na rorya hivyo wananchi wote hawana budi kuendeleza juhudi za Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unaenda salama mkoani humo.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ameahidi Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano wa kutosha na kusimamia vyema uchaguzi ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu bila kutishwa na wahalifu.
Alisema Tume ya Uchaguzi imeweka utaratibu mzuri wa kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo hivyo hakuna haja ya wafuasi kukaa nje ya vituo vya kupigia kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kujenga mazingira ya kuleta vurugu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe,Zeletho Stephen alisema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha anashiriki kwa nafasi yake kuimarisha usalama na amani hasa katika kipindi hiki.
IGP Mangu yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi ambapo pia amekuwa akitumia fursa hiyo kukutana na wadau mbalimbali ili kushauriana jinsi ya kuimarisha amanai na usalama katika maeneo yao.

NIMESTUKA WAWASTUA WAKAZI WA IGUNGA


Msanii Inspector Haarun akiwa ameongozana na Kasala wakiingia eneo la mkutano mjini Igunga.
Msanii Kupa akiwa amembeba msanii wa vichekesho, Tausi huku Msanii Ndede akipunga mkono kuwasilimia wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini hapo kwa shuguli za Kampeni.
Msanii Kajala akitoa ishara ya Gole Gumba kama alama ya CCM kwa wakazi wa mji wa Igunga alipoitwa jukwaani kuwasalimia wana Igunga.
Msanii Ray Kigosi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Sehemu ya baadhi ya wakazi wa Igunga waliohudhuria mkutano huo.
Msanii Aunt Ezekiel akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii wa vichekesho, Mr Kupa akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Wasanii wa Bongo Muvi, kuanzia kushoto ni Stan Bakora, Aunt Ezekiel na Kajala wakifuatilia mkutano wa kampeni ulifanyika mjini Igunga.
Msanii wa Bongo Muvi, Sajent akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kitale akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Kajala akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii vichekesho, Mboto akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii Ndende akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Msanii vichekesho, Tausi akizungumza na wana Igunga katika mkutano wa kampeni zizoendelea mjini hapo.
Mboto akiwaaga wana Igunga mara baada ya mkutano kumalizika.
Picha zote na Sule Junior

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MERCK SADICK ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA KUANZA KESHO



MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Merck Sadick anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa mwaka  wa 46 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania utakaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 4 octoba mwaka huu katika eneo la kitonga, Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaaM.

Hayo yamesemwa na Amir Mbashiri Mkuu Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Sheikh Tahir amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya Islam, kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wanajumuiya na wananchi kwa ujumla na kuhamasisha amani katika jamii.

Ameongeza kuwa kwa muda wa miaka mitano Jumuiya imekuwa ikiandaa mikutano ya amani katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuhamasisha jamii, dini mbalimbali na asasi za kijamii kuishi kwa amani licha ya kuwepo kwa tofauti za itikadi na mitazamo.

Kwa uapande wake Katibu Mkuu waJumuiya hiyo Seif Hassan amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, amewaasa viongozi wote wa dini tofauti kutojihusisha na mambo ya kisiasa na kushukuru ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka serikalini katika kutekeleza shughuli na kutarajia kuwa serikali na wadau wengine kujitokeza kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zijazo.

Aidha Jumuiya inatoa huduma ya elimu ya sekondari katika mkoa wa Dar es salaam na shule ya msingi katika mkoa wa morogorona kupitia asasi ya Humanity First Jumuiya imetoa msaada wa vifaa tiba ikiwa ni pamoja na mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammogram) katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 

Takribani washiriki 3500 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, na Msumbiji watahudhuria katika mkutano huo uliobeba kauli mbiu isemayo “mapenzi kwa wote, chuki si kwa yeyote”

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AMPONGEZA NDEJEMBI, AMSIFIA KWA UADILIFU NA UCHAPAKAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba , amempongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuaminiwa ...