Friday, February 19, 2010

Bomani aishangaa serikali kuogopa mgombea binafsi

Asema baba wa taifa Mwalimu Nyerere alibariki hilo mwaka 1995


MWANASHERIA Mkuu wa Kwanza mzalendo nchini, Jaji Mark Bomani amesema serikali inakwamisha bila sababu suala la mgombea binafsi katika uchaguzi, ambalo licha ya kupata baraka za mahakama lilishapata baraka zote za baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Mbali na kuitaka serikali kuacha kigugumizi katika kuruhusu utekelezaji wa suala hilo; alikosoa mfumo wa sasa wa uchaguzi na uteuzi wa mawaziri na kupendekeza kwamba, siyo lazima waziri awe mbunge.

Suala hili lilifunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa DP, Christopher Mtikila ambayo ilitoa hukumu mwaka 2006 iliyoruhusu kuwepo mgombea binafsi, lakini serikali imeendelea kuweka ngumu kwa kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa kuomba hukumu hiyo ipitiwe upya.
Februari 8, mwaka huu Jaji Mkuu, Augustine Ramadhan aliahirisha kusikiliza rufaa hiyo baada ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu kutojiandaa vizuri hivyo kuomba isogezwe mbele. Akiahirisha rufaa hiyo, Jaji Ramadhan alisema hukumu ya Mahakamu Kuu itaendelea kama ilivyo hadi hapo rufaa itakapopitiwa na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa na kumlaumu Naibu Mwanasheria Mkuu kwa kutojiandaa kikamilifu wakati wao ndiyo walioomba ipitiwe upya.

Katika taarifa yake maalumu aliyoitoa kwa gazeti hili jana, Jaji Bomani alisema mfumo wa mgombea binafsi katika chaguzi sio haramu kwa kuwa umeshakubaliwa na wataalamu mbalimbali.

Kauli hiyo ya Jaji Bomani imekuja karibu majuma mawili tangu jopo la majaji saba wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuitaka serikali kuwa makini katika rufaa waliyoikata dhidi ya hukumu ya mahakama kuu kuwepo kwa mgombea binafsi.

Walisema endapo serikali italegalega katika rufaa yake dhidi ya hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, suala la kuruhusiwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao, liko palepale.

Jaji Bomani ambaye alishawahi kushiriki katika kamati mbalimbali za kutafiti mfumo sahihi wa uchaguzi unaofaa Tanzania, alitoa changamoto kwa Rais Jakaya Kikwete kuwa ndiye anayepaswa kusimamia suala hilo.

Alisema Rais Kikwete ana nguvu na nafasi ya kihistoria kutekeleza uamuzi huo wa mahakama kwa kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao.

Jaji Bomani alisema hatua nzuri na muhimu ya kuanzia katika utekelezaji wa suala la mgombea binafsi na kuboresha mfumo wa uchaguzi Tanzania, ni kupitia upya ripoti ya Jaji Kisanga, jambo alilosema kuwa serikali haijachelewa.
Imeandikwa na Salim Said na Nora Damian: SOURCE:MWANANCHI

Kada CCM akabiliwa na mashtaka sita ya utapeli


ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa CCM, mkoani Dar es Salaam, Haji Manara (35), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu mashtaka sita ya kujipatia mali na fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alipandishwa kizimbani saa 7:45 mchana na kusomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Benadictor Beda.

Mwendesha mashtaka Batseba Kasanga alimwambia hakimu Beda kuwa katika shtaka la kwanza mtuhumiwa aliiba gari aina ya Toyota OPA mali ya Abdul Ngalawa.

Kwa mujibu wa Kasanga tukio hilo lilifanyika Novemba 27 mwaka jana eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mwendesha mashtaka huyo alifafanua kuwa katika tukio hilo, mtuhumiwa alipewa gari hilo na mlalamikaji ili akaiuze kwa Sh10 milioni na kumpa fedha hiyo lakini, baada ya kuiuza, hakumpelekea fedha wala kumrudishia gari yake.

Kasanga alizidi kudai mahakamani hapo kuwa Desemba 19, mwaka jana, kwa njia ya ulaghai, mtuhumiwa alijipatia magari mawili yenye namba aina ya Toyota IPSAM na Toyota NADIA mali ya Asma Miraji.

Alisema mtuhumiwa alipewa magari hayo kwa makubaliano kuwa angeyarudisha baada ya siku kumi lakini, hakufanya hivyo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, katika shtaka lingine Manara alijipatia pia Sh5 milioni kutoka kwa Jocob Manyanga kwa makubaliano kuwa angemuuzia gari lake, kitu ambacho hakufanya.

Alisema tukio hilo lilitokea Januari tano mwaka huu manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kasanga alimweleza hakimu Beda kuwa Desemba 20 mwaka jana, eneo la Magomeni mtuhumiwa huyo alijipatia tena Sh3 milioni kutoka kwa Wilson Matimba kwa makubaliano ya kumuuzia gari yake.

Alisema pia Januari 29 mwaka huu eneo la Magomeni saa 11:00 jioni, Manara alijipatia Sh19 milioni za mkopo kutoka kwa Dotto Hussein akieleza kuwa yeye ni mfanyabiashara na kwamba angemrudishia fedha hiyo baada ya siku tano.

Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa Manara pia alijipatia Sh36 milioni kutoka kwa Fadhili Mtandika mkazi wa eneo Magomeni jijini Dar es Salaam kwa njia ya utapeli.

Alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 13 mwaka huu saa 2:00 usiku.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alikana makosa yote sita na kurudishwa rumande kwa kukosa dhamana hadi Machi 4 mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea.

Mtuhumiwa aliswekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili wanaofanyakazi zinazofahamika, wawe na mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 35milioni au fedha tasilimu Sh 17milioni.Ummy Muya

Wednesday, February 17, 2010

Maunga adakwa na dawa za kulevya



HALID Salim Maunga (35), raia wa Uingereza aliyekuwa na hati ya kusafiria namba 109483453, juzi asubuhi alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kete 69 za madawa ya kulevya aina ya cocaine pamoja na bangi gramu 610.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamishna Msaidizi wa Polisi wa viwanja vya ndege nchini, Mwajuma Kiponza alisema Halid alikamatwa na askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege (TAA) wakati akiwa katika hatua za mwisho za ukaguzi katika uwanja hapo.

Alisema polisi pamoja na maofisa hao, walimtilia mashaka raia huyo, wa Uingereza aliyekuwa amefikia maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam na kuanza kumpekua na walibaini alificha kete 16 kwenye pindo la suruali yake sehemu ya kiunoni na kete 14 zilikutwa katika pindo ya chini ya suruali yake.

“Baada ya kumgundua kuwa amebeba vitu hivi polisi walimkamata na kumpeleka kituoni kwa ajili ya kumhoji zaidi, lakini walipofungua begi lake walikuta vinyago vitatu ambavyo vilikuwa na kete hizo za madawa ya kulevya pamoja na bangi.

“Vinyago hivyo vilikuwa na mfano wa mnyama na binadamu na kimoja kilikutwa na bangi pamoja na kete 21 za madawa ya kulevya na kingine kilikutwa na bangi pamoja na kete 18 na hivyo kufanya jumla ya kete hizo kuwa 69, alikuwa akienda nchini Uingereza na ndege ya Shirika la ndege la British Airways,” alisema Kiponza

Alisema baada ya kumhoji aliwaeleza kuwa alikuwa akiishi maeneo ya Makumbusho na Polisi walifika mpaka nyumba aliyokuwa akiishi, lakini hawakufanikiwa kukamata kitu chochote.

Alifafanua ndugu wa Halid walithibitisha kumfahamu ndugu yao ila walipoulizwa kazi anayoifanya walidai hawaifahamu na kufafanua kuwa wanachokijua ni kuwa ndugu yao anaishi nchini Uingereza.

Alipoulizwa swali na gazeti hili, njia zinazotumiwa na jeshi hilo kuwabaini watu mbalimbali wanaobeba madawa ya kulevya, Kiponza alisema; “kitu cha kwanza kinachotusaidia ni mashine zilizopo pale uwanjani, sikatai wapo wanaopita ila huwa tunakuwa makini sana hasa kwa wasafiri ambao hutoka au kwenda nchi ambazo zinasifika kwa biashara za madawa haya.”

Alisema wanatunza kumbukumbu za hati za kusafiria za wasafiri wanaokwenda katika nchi hizo na kunakili tarehe wanazoondoka na watakayorejea ili iwe rahisi kwao kuwafuatilia licha ya kuwa wakati mwingine wasafiri hao hurudi bila kuwa na mzigo wowote. Fidelis Butahe na Zaina Malongo: SOURCE:: MWANANCHI

mwana wa mkulima afuata kilimo Rome


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa IFAD, Dk. Kanayo Nwanze kabla ya kuhutubia mkutano wa IFAD jijini Rome, Italia alikomwakilisha Rais, Jakaya Kikwete. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wanafunzi Temeke wafunga barabara



ZAIDI ya wanafunzi 1000 wa shule za msingi za Umoja na Miburani zilizoko Temeke Dar es Salaam, jana walifunga barabara kwa zaidi ya saa nne na kusababisha vurugu kubwa katika eneo la Sudani, makutano ya Barabara ya Tandika na Temeke.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kutaka eneo hilo liwekewe matuta, wanafunzi hao waliokuwa na silaha mbalimbali, walirusha mawe hovyo na wengine kurukaruka barabarani.

Vurugu hizo pamoja na zile za kurushia mchanga magari, zilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika eneo hilo.

Habari zilizosema fujo hizo zilitokana na mmoja wa wanafunzi hao kugongwa na daladala.

Kwa mujibu wa habari hizo, tukio hilo ni la tatu kutokea katika eneo hilo. Juzi mwanafunzi mmoja alinusurika kugongwa na gari na mwingine aligongwa na guta.

“Hatutoki hapa mpaka matuta yajengwe leo, serikali mbona mnatuua, Jengeni matuta basi, hapa hakieleweki tunataka haki yetu.” alisema mmoja wa wanafunzi hao.

“Tumeenda wilayani eti wanatuambia turudi shuleni watakuja kujenga matuta baada ya siku tatu lakini, sisi bado tunakuja shule na kuvuka barabara hii, hatudanganyiki,” alisema mwingine.

Mashuhuda wa tukio hilo walilieleza gazeti hili kuwa saa 1:00 asubuhi ya jana, mwanafunzi Abdul Idrisa wa darasa la pili katika Shule Msingi Umoja, aligongwa na daladala iliyokuwa inatoka Tandika kuelekea Kariakoo.

Mwanafunzi huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa katika Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

Hata hivyo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dk Gilbert Buberwa, alisema hali ya mwanafunzi huyo inaendelea vizuri.

“Tulimpokea mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka saba, saa 3:00 asubuhi na baada ya kumfanyia X-ray, tumegundua kuwa amejeruhiwa maeneo ya miguuni lakini, uchunguzi bado unaendelea," alisema Dk Buberwa na kuongeza; Habari imeandikwa na Felix Mwagara: SOURCE: MWANANCHI

'Haturidhiki na uamuzi wa bunge kuhusu Richmond'



WANAHARAKATI wa FemAct na vikundi vingine vya kiraia nchini wameeleza kutoridhishwa na kushtushwa na utendaji wa Bunge na Wabunge baada ya kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya kashfa ya Richmond na nyingine.

Kutokana na hatua hiyo wananaharakati hao, wametangaza kuandaa maandamano nchi nzima kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa Bunge.
Aliema wananchi watahamasishwa kuonyesha hasira dhidi ya chombo hicho na kudai mfumo mbadala wa demokrasia nchini.

Wakitoa tamko la pamoja lililoshirikisha asasi na vyama vya kiraia zaidi ya 50, makao makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam, wanaharakati hao wamelitaka Bunge kujisafisha kwa kuweka maslahi taifa mbele badala ya maslahi ya vyama na wabunge binafsi.

“Tofauti na matarajio ya wananchi, Bunge limemaliza kikao chake bila kuchukua hatua madhubuti kuhusu kashfa ya Richmond, Kiwira, Ticts, TRL, Loliondo na North Mara. Jambo hili limetushtua na kutusikitisha sana,” alisema Kaiza Buberwa mkurugenzi wa asasi ya Fordia.

“Sisi wananchi tunanona kuwa Bunge limeshindwa kutekeleza wajibu wake kikatiba wa kuisimamia serikali, kutokana na mfumo mbaya wa madaraka na uwajibikaji kati ya serikali na bunge unaoruhusu maslahi ya chama tawala kuchukua hatamu kuliko maslahi ya taifa,” alisema Buberwa.

“Tunapendekeza Bunge lijisafishe na kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko maslahi ya vyama na wabunge binafsi,” alisema mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Francis Kiwanga.

“Kama Asasi za kiraia tumeamua kuandaa maandamano makubwa ya kitaifa kuonyesha kutoridhishwa na utendaji usioridhisha wa Bunge la sasa na kudai mfumo mbadala wa demokrasia shirikishi ambao una uwezo zaidi kutetea maslahi ya wananchi,” alisema.

Wanaharakati hao walibainisha kuwa fedha zilizopotea katika kashfa ya Richmond zinazofikia Sh173 bilioni zingeweza kutosha kujenga nyumba19,211 za walimu wa shule ya msingi huku kila shule ikigharimu Sh9 milioni.

Walisema kutokana na mfumo uliopo hivi sasa, ni vigumu Bunge kuiwajibisha serikali na ndiyo sababu Bunge limefunika kisiasa kashfa za Richmond, mgodi wa makaa ya mawe Kiwira, TRL na Ticts. Imeandikwa na Exuper Kachenje: SOURCE -MWANANCHI

Tuesday, February 16, 2010

President Kikwete praises Karimjee Family


H.E. Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, The President launched the Karimjee Jivanjee family book on Saturday February 13th from 5.00pm to 8.00pm at an exclusive function at the Kilimanjaro Kempinski Hotel.

Hatim A. Karimjee, Chairman of Karimjee Jivanjee Ltd began by welcoming H.E. The President, the Honorable Minister of Home Affairs Lawrence K. Masha, MP, Honorable Regional Commissioner for Dar es Salaam William Lukuvi, Ambassadors and distinguished guests including Karimjee Jivanjee family members visiting from the UK, Mauritius and Pakistan.

He began by saying “This is a very special day for the Karimjee Family because it has been our intention to write this history for many years and finally it has been achieved. This book has taken three years of research and writing”.

He congratulated Professor Gijsbert Oonk for writing an excellent book, well illustrated with many historical photos. He continued by highlighting Professor Oonk’s strength as an academic and a historian and his approach which was always to cross reference and look for other sources to reach the truth.

The book which records the 200 year history of the family is firstly a fascinating adventure story and secondly is a tribute to the Karimjee family’s ancestors who crossed the “kali pani” in a dhow from India to Africa at the beginning of the 19th Century. Having reached Zanzibar, the family ancestors prospered in the face of amazing difficulties through determination, hard work and an enterprising spirit. SOURCE KARIMJEE FAMILY

MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...