Friday, February 23, 2018

UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA GEITA WAFIKIA ASILIMIA 35

Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta  akielezea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.
Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta  akionesha michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa.
      
Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita, Dkt Joseph Odero akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita wakati walipofika kwa ajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Geita. 

Michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu akizungumza na  Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta  wakati alipofika kwaajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji,Leornad Bugomola  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita.Leornad Kiganga Bugomola akikagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu,akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyopo kwa sasa ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero  akizunguma juu ya changamoto ambazo zipo kwa sasa kutokana na hospitali iliyopo kuwa ndogo.


Na,Joel Maduka,Geita.
 
 
Hospitali ya rufaa Mkoani Geita inayojengwa Mtaa wa Magogo kata ya Bombambili mjini Geita inatarajiwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu moja wa nje na zaidi ya 480 watakaokuwa wakilazwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mwenyekiti wa bodi teule ya hospitali hiyo, Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Gladys Jefta alisema katika hatua ya kwanza ya ujenzi wanaendelea na ujenzi wa majengo manne na wanatarajia kukamilisha baada ya miezi 9 ambapo umefikia asilimia 35.
 
“Tunatarajia  hospitali hii itakapokamilika itahudumia idadi ya wagonjwa wa nje zaidia ya elfu moja na wa kulazwa mia nne na themanini na tunaamini   ndani ya muda wa miezi mitatu ambayo tumeomba  kuongezewa tutakuwa tumekamilisha ujenzi,”alisema Mhandisi Gladys.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu alisema matarajio walitarajia Hospitali hiyo ingekamilika ndani ya miezi 9 lakini kukosekana kwa umeme na maji ndio sababu zilizokwamisha mradi huo kwa kuwa Mkandarasi amekuwa akinunua maji kutoka nje na wakati mwingine kutumia mafuta kwa ajili ya jenereta.
 
Kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Geita Dr Joseph Odero alisema hospitali ya rufaa ya sasa ambayo ilikuwa ya wilaya ni ndogo kwa kuwa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa  150 hadi 200 na wale wa kulazwa 200 hadi 250
na kwamba  hali ya wagonjwa kwa sasa ni kuanzia 300 hadi 350 hivyo kukamilika kwa hospitali hiyo ya rufaa kutasaidia kukabiliana na changamoto ya wingi wa wagonjwa.
 
Mradi wa ujenzi  wa hospitali ya rufaa kwa sasa umefikia asilimia 35 kwa hatua ya kwanza ambayo inatarajia kugharimu kiasi cha Sh Bilioni 5.9

TANZANIA YAIPONGEZA FIFA KWA KUPAMBANA NA RUSHWA

PMO_8613

SERIKALI ya Tanzania inalipongeza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na shirikisho hilo katika mapambano dhidi ya rushwa.
Kauli hiyo imetolewa jana (Alhamisi, Februari 22, 2018) na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa katika kikao chake na Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino kilichofanyika jijini Dae es Salaam.
“Serikali  tunaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo pamoja na matumizi mabaya ya fedha na ya madaraka yanayofanywa na FIFA”.
Waziri Mkuu amesema wanaunga mkono mapambano hayo ili Taifa liweze kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye maono ya mbali katika kuendeleza mchezo huo.
Amesema FIFA ambayo ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo , hivyo Tanzania inaiunga mkono kwa kuhakikisha sekta ya michezo inatumia vizuri fedha zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo.
Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inasimamia matumizi sahihi ya madaraka katika sekta ya michezo nchini ili kuleta maendeleo kwenye mpira wa miguu.
Serikali inaipongeza FIFA kwa jitihada za dhati za kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kuwa mipango mbalimbali ya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana wadogo wa kike na wa kiume nchini.
“Tunatambua msukumo wa FIFA wa kuendelea mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na kuboresha viwanja vya michezo pamoja na maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta hiyo.

Pia ameishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani jijini Dar es Salaam na kwamba Serikali itayasimamia vizuri na inajiandaa kwa kushinda.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa FIFA Bw. Infantino kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendesha mkutano mkubwa wa viongozi wa mpira wa miguu duniani Tanzania. Mkutano huo ulihusisha Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 21.
Pia alimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Bw. Ahmad Ahmad kwa jitihada zake za anazozifanya katika kuendeleza mpira barani Afrika na kwamba Serikali  ya Tanzania inamuunga mkono.
Rais wa FIFA Bw. Infantino ambaye ameahidi kuisaidia Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo aliwasili nchini leo alfajiri akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Bw. Ahmad Ahmad kwa ajili ya mkutano wa FIFA uliofanyika nchini Tanzania February 22, 2018.

Bw. Infantino amewasili kwa mara ya kwanza Tanzania toka awe Rais wa  FIFA na alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dtk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leodger Tenga na Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia.

WAZIRI JAFO AAGIZA DARAJA LA CHIPANGA LIKAMILIKE KABLA YA MWEZI JULAI, MWAKA HUU



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Badwel na viongozi wengine wa wilaya ya Bahi.
  Daraja la Chipanga linaloendelea kujengwa
Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa daraja la Chipanga.


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Medes Company Limited na Millenium Master Builders (T) Limited anayejenga daraja la Chipanga wilayani Bahi, kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo mwezi Julai, mwaka huu bila visingizio vyovyote.

Akikagua ujenzi wa daraja hilo, Jafo amesema awali kazi ya ujenzi wa Daraja hilo ilitarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu lakini kutokana na Mvua zilizokuwa zikinyesha amewaelekeza kukamilisha ifikapo Julai mwaka huu.

Jafo amewaagiza wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kukaa na mkandarasi kukubaliana tarehe ya mwisho ya kukamilika kazi hiyo lakini kinachotakiwa ifikapo Julai mwaka huu daraja hilo liwe limekamilika.

Amebainisha kuwa daraja hilo ni kiunganishi cha kata ya Chipanga na Makao makuu ya wilaya ya Bahi na ujenzi wake unagharimu kiasi cha Sh. bilioni 2.11.

Akizungumza katika mkutano wa hadharana wananchi wa Chipanga, Waziri Jafo amewataka wananchi hao kuacha tabia ya kupitisha ng'ombe na majembe ya ng’ombe kwenye barabarani zinazojengwa kwa kuwa wanasababisha uharibifu wa barabara.

Amesema serikali haiwezi kuvumilia uharibifu wowote wa miundombinu ambayo inagharimu gharama kubwa.

MAKAMU WA RAIS APOKEA MISAADA KUTOKA UBALOZI WA CHINA KWA AJILI YA MAENDELEO MKOANI SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 178,488,00/- kutoka kwa Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Nkoma iliyopo Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Vyerehani 50 kwa ajili halmashauri ya mji wa Bariadi ili kuanzisha Kiwanda cha Ushonaji.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Tuesday, February 20, 2018

HESLB YAWAKUMBUSHA WAAJIRI KUZINGATIA SHERIA


 Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB Bw. Phidelis Joseph akizungumza na waandishi habari kuhusiana ufatilialiaji mkopo kwa walionufaika leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bw. Nzinyangwa Mchany (kulia) na Meneja Mawasiliano wa EWURA Bw. Titus Kaguo(katikati) wakionesha ngao ya utambuzi ya utambuzi walioyokabidhiwa leo (Jumatatu, Februari 19, 2018) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (kushoto) kutambua mchango wa taasisi katika urejeshaji mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wafanyakazi wanufaika EWURA. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Academic, Mariam Mtelesia ngao ya utambuzi wa ushirikiano wao katika kufanikisha kazi ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika ambao ni wafanyakazi katika taasisi yao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB Bw. Phidelis Joseph akiongea leo (Jumatatu, Februari 19, 2018) jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwakabidhi waajiri ngao za utambuzi wa ushirikiano wao katika kufanikisha kazi ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika wafanyakazi.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewakumbusha waajiri nchini kote kuzingatia matakwa ya Sheria ya bodi hiyo inayowataka kuwasilisha orodha ya majina ya waajiriwa ambao ni wahitimu wa shahada au stashahada ili kuiwezesha Bodi kubaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Akizungumza na waandishi habari wakati wa wa hafla fupi ya kuwatambua baadhi ya waajiri wanaotimiza masharti ya Sheria ya HESLB, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo,Abdul-Razaq Badru amesema kuwa sheria hiyo inawataka waajiri kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mwajiriwa na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB ndani ya siku 15 baada ya tarehe ya mwisho ya mwezi.

Amesema kuwatunuku ngao ni kutambua mchango wao katika kurejesha mikopo ili kuwasomesha watu wengine na kuwataka waajiri watekeleze sheria hiyo na kuongeza ufanisi wa shughuli za HESLB hususan katika urejeshwaji wa mikopo.

Taasisi zilizokabidhiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Benki ya NMB, Benki ya CRDB, Benki ya Stanbic, Deloitte Tanzania, Kampuni ya Sigara Tanzania, na Kamouni ya Coca Cola Kwanza. Kampuni nyingine ni Vodacom Tanzania, Nokia Solution Tanzania, Shule za Academic, Shule za Al-Hikma na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

“Nyie ni wadau wetu muhimu sana. Tunavyosema tumeongeza makusanyo ya mikopo iliyoiva kutoka wastani wa TZS 2 bilioni kwa mwezi miaka mitatu iliyopita hadi wastani wa TZS 13 hivi sasa ni kwa sababu ya waajiri kama ninyi … tunawashukuru sana,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB katika hafla hiyo.

Amesema takwimu zinaonyesha, Benki za CRDB na NMB kwa pamoja ziliwasilisha kiasi cha TZS 274.4 milioni kama makato ya mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wafanyakazi wao kwa mwezi Disemba, 2017 pekee. Fedha hizi zinaweza kukopeshwa kwa wanafunzi 78 wa elimu ya juu kwa wastani wa TZS 3.5 milioni kwa mwaka ambazo hutolewa na HESLB hivi sasa.   

Aidha amesema baadhi ya waajiri waliokabidhiwa ngao wameanzisha utaratibu nafuu ndani ya mashirika yao unaowawezesha waajiriwa wanaodaiwa mikopo ya elimu ya juu kuchukua hati ya deni HESLB na kulipa kwa mkupuo kwa uwezeshaji wa mwajiri.
Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB Bw. Phidelis Joseph amesema wataendelea kuwatembelea waajiri ili kubadilishana mawazo kwa lengo la kuongeza ufanisi na makusanyo.

“Ni wajibu wetu kuwafikia waajiri popote walipo ili kuwasikia na kubadilishana mawazo ili hatimaye tuwe na waajiri wengi zaidi wanaotimiza matakwa ya kisheria,” aliongeza.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ngao, Mwakilishi wa Nokia Solution Tanzania Bi. Doroth Namuhisa mara baada ya kuajiri, huchukua majina kamili ya mwajiriwa, jina la chuo alichosoma na namba kamili ya mtihani yenye mwaka aliofanya mtihani huo wa kidato cha nne na kuwasilisha HESLB ili wanufaika waweze kubainika.

“Tumejiwekea utaratibu wa kuwasilisha taarifa zote muhimu kwa Bodi ya Mikopo na ndiyo sababu hatupati changamoto kubwa,” alisema Bi. Namuhisa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Stanbic Bi. Eutropia Vegula ameipongeza HESLB kwa ushirikiano inaowapatia na kuongeza kuwa benki yake imeingiza matakwa ya Sheria ya HESLB katika sera yao ajira kwa kuhakikisha kila mwombaji kazi anafahamika kama ni mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu au hapana. 

BINSLUM ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION

Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Coastal Union baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao katika halfa iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum 
Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa 
Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda katika akiwa na Kocha wa Makipa Salim Waziri kushoto na kocha Msaidizi Joseph Lazaro kulia 
Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akisalimiana na mchezaji wa timu hiyo,Athumani Iddi Chuji
Mfadhili wa timu ya Coastal Union Nassoro Binslum kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Mchezaji Athumani Iddi Chuji ambazo zimeandaliwa na mfadhili wa timu hiyo ,Nassoro Binslum kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kuipandishi timu hiyo kucheza Ligi kuu
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Mlinda Mlango wa timu ya Coastal Union Sharifu Kasilasi kwa mchango wao wa kusaidia timu hiyo kupanda daraja
Kocha Msaidizi wa timu ya Coastal Union Joseph lazaro akipokea naye tuzo kutrokana na mchango wao waliuonyesha kwenye michuano ya Ligi Daraja la kwanza na kusaidia timu hiyo kupanda daraja(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha) 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union Juma Mgunda baada ya kufanikisha timu ya Coastal Union kupanda daraja
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akimkabidhi tuzo Kocha wa Makipa wa timu ya Coastal Union,Salim Waziri 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akimkabidhi tuzo beki wa timu ya Coastal Union Hamad Juma 
Sehemu ya wachezaji wa timu ya Coastal Union wakiwa na wake zao wakipata chakula kwenye halfa hiyo 
Mwenyekiti wa Kamat ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora kushoto akiteta jambo na Mwandishi wa Gazeti la Majira mkoani Tanga Mashaka Mhando 
Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Resort Joseph Ngoyo akiteta jambo na mdau wa michezo wakati wa hafla hiyo ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union Hemed Aurora katika akiwa na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Salim Bawaziri


Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu ya Coastal Union,Hafidhi Kidoh kulia akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Majira Tanga Mashaka Mhando kwenye halfa hiyo ya kupongeza wachezaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga 


UONGOZI wa timu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” umetakiwa kushikamana na kutoruhusu migogoro na makundi yasiyokuwa na tija kwani yanaweza kukwamisha ndoto zao za kupata mafanikio katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara. 
Lakini pia waaache vurugu na chokochoko iwapo wanataka kupata mafanikio huku wakitakiwa kuangalie wale wachache watakaopelekea hali hiyo wasiwaunge mkono kwa kuonyesheni mfano wamewachoka. 
Hayo yalibainishwa na Mfadhili wa timu hiyo,Nassoro Binslum wakati akizungumza kwenye ghafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo sambamba na utolewaji wa zawadi baada ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort 
Alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likirudisha nyuma mafanikio ya timu hiyo ni majungu,fitina na makundi ndani na nje ya timi hiyo hivyo ni bora viongozi,wapenzi ,wanachama wakabadilika na kuongeza mshikamano . 
Binslum alisema umoja ulioonyeshwa na viongozi,wanachama na washabiki wakati timu ilipokuwa inatafuta nafasi ya kupanda ligi kuu unatakiwa uendelezwe ili uwe na tija kwa timu hiyo ili iweze kurudisha heshima yake ya miaka ya nyuma kuchukua ubingwa. 
Aidha alisema wakati timu zinapokuwa kwenye madaraja ya chini kunakuwa hakuna majungu wala makundi maana kipindi hicho hakuna udhamini wale fedha lakini inapopanda timu kila mtu anaweza kujitokeza kwa kueleza anaweza kuongoza. 
“Ndugu zangu niwaambie tuwaache viongozi,benchi la ufundi na wadhamini na sisi wengine tubaki tu kama wachezaji wa kumi na mbili kuisapoti timu na tukifanya hivyo tutafanikiwa sana kwani tutakuwa tumeweka msingi mzuri na imara “Alisema Binslum. 
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya usajili Hemed Aurora alisema mbali na mafanikio hayo jambo kubwa litakalozingatiwa kuhakikisha makundi hayatakuwa na nafasi ili kuepusha yaliyoikuta timu hiyo na kupelekea kushuka daraja. 
Aurora alisema uwendeshaji wa timu unagharama kubwa itakayokuwepo si kutafuta ubingwa wa ligi kuu bali kuhakikisha kunajengwa umoja utakaoleta mafanikio na kupambana na wale wasiokuwa na nia njema na timu hasa baada ya timu hiyo kupanda. 
“Tunatambua sasa kazi ndio inaanza ni zaidi ya miaka 30 kihistoria tangu timu hiyo iliptwaa ubingwa lakini ubingwa si kazi kama tutashikamana na kuwapinga kwa pamoja wale maadui zetu wanaosubiri timu ipande waseme timu yao tutawashughulikia safari hii”Alisema. 
Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa alisema timu kurudi kucheza ligi kuu kunafaida kubwa sana kwa wanamichezo tu ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwani itasaidia kuinua ukuaji wa uchumi ndani ya Halmashauri ya Jiji. 
Aidha alisema serikali iliahidi vitu vingi juu ya timu hiyo siku ya
mapokezi yake ilipokuwa ikitokea Morogoro na jukumu lililopo ni utekelezaji wake ambao unaweza kuleta tija zaidi na timu nyingine kupanda na kufikia idadi kama ya zamani. 
Hata hivyo alisema serikali imejitoa zaidi kuhakikisha inaisaidia timu hiyo iweze kuwa tishio na kwenye michuano ya Ligi kuu msimu ujao huku akizitaka zilizobakia nazo kuhakikisha zinaweka mipango imara ya kupanda ili kukuza vipaji vya vijana wetu na uchumu wa pato mkoa kwa kupitia michezo. 
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa timu hiyo,Steven Mguto alisema wataendelea kushikamana ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania Bara msimu ujao. 
Aliongeza kuwa mshikamano waliouonyesha wakati wa michuano hiyo ya Ligi Daraja la kwanza wataendelea nao ili kuhakikisha wanarudisha enzi za miaka 1988 walipotwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

DMF, MAKJUICE WAWAPA FARAJA WAZAZI WA WATOTO NJITI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR KATIKA SIKU YA WAPENDANAO


Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa wauguzi wa zamu wa Wadi ya Watoto Njiti katika Hospitali ya Mwananyamala, sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya kuonyeshana upendo (Valentine’s Day) ambayo huadhimishwa duniani kote kila ifikapo Februari 14. Taasisi ya Doris Mollel walishirikiana na Kampuni ya MakJuice na baadhi ya wapigapicha, wanahabari pomoja na wadau wengine waliojitoa kufanikisha zoezi hilo, lililofanyika jana jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Warda Walid (Muwakilishi wa Taasisi ya DMF Zanzibar), Mariam Gerion (DMF Dar es salaam), Mtangazaji wa Clouds TV, Shadee pamoja na baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo.
 Picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo pamoja na vitu vingine mbalimbali.
 Muwakiliwa wa Kampuni ya MakJuice, Zahir akimkabidhi zawadi ya khanga mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), Doris Mollel akizungumza jambo na mmoja wa kinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati (Njiti) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
 Wakinamama waliojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), wakipoza koo zao na Juice za Mak walipotembelea Hospitalini hapo.

Mwigulu awaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32000

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.

Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.

Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.

“Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanaitaji kurudi makwao,naagiza muwaandikie barua leo hii kuwa hao wakimbizi ambao wapo katika kambi za Nduta,Nyarugusu na mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanaitaji kurudi kwao wakajilete maendeleo” alisema Dr Mwigulu

Waziri Nchemba aliongeza kuwa hatakaa kikao cha pande tatu kujadili kuhusu kuondoka kwa wakimbizi hao kwani wamesha kaa mwaka jana wakakubaliana jinsi ya kuondoka kwa wakimbizi hao nchini kwani mda huu ndii mda wa kilimo na kuwapeleka mwezi wa nne huko nikiwafanya wakaishi maishi magumu zaidi.

Naye mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma Tonny Laizer amesema kutokana na hali ya usalama nchini burundi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutopokea waomba hifadhi, kituo cha Lumasi kinafungwa na serikali ya wilaya itakabidhiwa na UNHCR kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA UKEREWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wananchi  wa Ukerewe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia  mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio  Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mongella katika mji mdogo wa Nansio kuhutubia mkutano wa hadhara, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa chanjo ya Polio kwa mtoto mchanga aliyepakatwa na mama yake mzazi, Dianna Malele (kushoto)  wakati alipozindua  zahanati ya Nakatunguru wilayani Ukerewe, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa chanjo ya Polio kwa mtoto mchanga aliyepakatwa na mama yake mzazi, Rizika Shaka (kushoto)  wakati alipozindua zahanati ya Nakatunguru wilayani Ukerewe, Februari 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...