DK Palangyo awataka tanesco na Tanroads kufanya kazi kwa pamoja kukamilisha mradi wa umeme Dar es Salaam kwa wakati
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini , Dk. Juliana Palangyo amewaagiza wahandisi wa Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara nchini Tanroads kufanya nguvu kwa pamoja ili kuweka alama za miundombinu ya mradi wa kuboresha umeme wa Dar es Salaam itapita katika barabara ya Mandela mpaka kurasini.
Dk .Palangyo amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akikagua sehemu ya miundombinu hiyo itakayopita kwa kushirikiana na Tanroads .
“Tanesco wamekubaliana na Wakala wa Barabara nchini kupitisha sehemu ya miundombinu ya umeme kando kando mwa barabra ya Mandela hili kuweza kuongeza nguvu katika kituo cha kurasini na mkoa mzima wa Dar es Salaam.Makubaliano haya yamefikiwa jana mara baada ya mimi kutembelea katika ofsi za Tanroads na sehemu ambapo miundombinu hiyo itatakiwa kupita”.
Dkt. Palangyo amesema kuwa wameamua kufanya mazungumzo na Tanroads hili kufikia muafaka kwakuwa wao nao walitaka kutumia eneo hilo katika moja ya miradi yao hivyo kufikia muafaka wa hili kumewezesha mradi wa tanesco kwenda kwa kasi zaidi ya awali.

No comments:
Post a Comment