Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania Bw. Nikubuka Shimwela (kulia) akiwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Idd watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Mbagala jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mjumbe wa bodi wa benki hiyo Bi. Zuhura Muro.
Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania, Bw.Nikubuka Shimwela, (kulia) akimkabidhi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina Children Home kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam, msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya sikukuu ya Idd, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christina Manyenye.
Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam,Bw.Clement Mwanzalima,akimkabidhi Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Hissani cha Mbagala jijini Dar es Salaam,Idaya Shukrani msaada wa boksi ya sabuni ulioambatana na vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho kusherehekea sikukuu ya Idd.
No comments:
Post a Comment