Sunday, August 19, 2012

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MKONO WA EID KWA VITUO SITA VYA KULELEA YATIMA

Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania Bw. Nikubuka Shimwela (kulia) akiwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Idd watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Mbagala jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mjumbe wa bodi wa benki hiyo Bi. Zuhura Muro.
Mkurugenzi wa benki ya KCB Tanzania, Bw.Nikubuka Shimwela, (kulia) akimkabidhi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina Children Home kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam, msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia ikiwa ni sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya sikukuu ya Idd, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bi.Christina Manyenye.
Meneja wa benki ya KCB Tanzania tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam,Bw.Clement Mwanzalima,akimkabidhi Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Hissani cha Mbagala jijini Dar es Salaam,Idaya Shukrani msaada wa boksi ya sabuni ulioambatana na vyakula mbalimbali kwa ajili ya watoto wa kituo hicho kusherehekea sikukuu ya Idd.

SALAAM ZA IDDI KUTOKA TAWI LA CHADEMA UINGEREZA

 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO TAWI LA LONDON
WANAWATAKIA IDD NJEMA WAISILAMU WOTE DUNIANI 

Rais Kikwete katika swala ya Eid Kinondoni Muslim leo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam kwa ajili ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa miongoni wa waumini kusikiliza  mawaidha kutoka kwa Sheikh Abubakar Zubeir katika  msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam baada ya  ya Swala ya Idd leo Agosti 19, 2012

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...