Tuesday, April 10, 2012

HAIJAPATA KUTOKEA MAZIKO YA KANUMBA

Mmoja wa waombolezaji akipitishwa juu juu kwenye vichwa vya waombolezaji ili kupata huduma ya kwanza baada ya kuzirai, katikati anayetazama mbele ni Mussa Kisoky Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Saimon Mwakifwamba akizungumza katika msiba huo kutoa salamu zao za rambirambi kwa marehemu Steven Kanumba
Askari wa kike wakiweka sawa utaratibu wa waombolezaji kupita katika eneo hilo ili kukaa.
Ndugu wa karibu wakielekea sehemu waliyotengewa kukaa.
Mwigizaji Steven Jacob kushoto akizungumza jambo na mbunge wa Maswa Mashariki Mh. John Shibuda katikati.
Jeneza la mwili wa marehemu Kanumba likiwa limewekwa tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho
Kundi maalum lililoandaliwa kwa nyimbo za maombolezo likiimba nyimbo za maombolezo katika katika msiba huo.
Mama wa Marehemu Steven Kanumba Flora Mtegoa akiwa katika hali ya majonzi mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akimfariji Mama Kanumba
Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga sal;ute mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa heshima kwa marehemu Steven Kanumba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulioagwa leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam huku viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, Wanamuziki Waigizaji na watu maarufu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji huo aliyekuwa maarufu zaidi nchini Tanzania na nje ya nchi pia, Marehemu Steven Kanumba anazikwa mchana huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii. Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia). Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.

Mmoja wa waombolezaji akisidiwa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu mara baada ya kuzimia katika msiba huo mkubwa.
Picha zote hizi ni kwa hisani ya

http://www.fullshangweblog.com

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...