Sunday, February 26, 2012

TABORA BOYS WAKUTANA MBALAMWEZI BEACH

Mwenyekiti wa Mkutano wa Wana Tabora Boys, Edwin Kidiffu wa kwanza kulia ambaye pia ni mwanasheria wa Ewura akimsikiliza kwa makini Makwinya aliyeinua mikono juu akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika ufukwe wa Mbalamwezi, wanaomsikiliza ni Bina Katikiro mwenye fulana ya bluu


Mzee wa Mshitu akiwapo kwenye mjadala uliokuwa ukiendelea kwa baadhi ya wana Tabora Boys Secondary School waliopata kusoma katika shule hiyo kongwe na yenye sifa tele nchini walipokutana jioni ya jana katika ufukwe wa Mbalamwezi jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kukutana, kutafakari na kujadili way forward ya wana Tabora School hao.

Braza Kamtande Sikalwanda (Mchawi wa hesabu) aliyeipandisha chati mno Sekondari ya Tabora enzi hizo (katikati) akijadili jambo na Braza Kipeya wakati wa mkutano huo wa wana Tabora Boys uliofanyika jana katika Ufukwe wa Mabamwezi. Anayewashuhudia kulia ni Danny Lyimo.

Makwinya naye alikuwapo, huyu jamaa enzi hizo akiwa Tabora Boys alikuwa mkoba wa kutumainiwa wa timu ya shule na hasa pale timu ilipoweza kuitandika timu ngumu ya Uyui Sekondari mabao mawili kwa bila jambo lililizua balaa. Hapa jamaa anapiga maji ya mende.


Dokta Mzee Gombo ambaye ni Specialist wa Meno Muhimbili enzi hizo alikuwa PC wa PCB kwa lugha rahisi alikuwa kiranja wa darasa la wakali wa kombinesheni ya PCB akiwa na akina Charles Sebastian na Rahim Mzee, kwa mbali waweza kumuona Second Chief George, ambaye sasa ni daktari wa magonjwa sugu.

Danny Lyimo akishuhudia wakati Makwinya akisalimiana na Luwaga Kizoka (Nyigu) , nyuma yake anaonekana Renasco Mbilinyi. Taarifa na picha zaidi za matukio hayo zitaletwa kwenu na timu ya Mzee wa Mshitu.

Wednesday, February 15, 2012

JK ashiriki ufyatuaji matofali Msoga





Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.

Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.

Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.

Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.

PICHA NA HABARI NA IKULU


WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...