Monday, May 30, 2011

Mdau wa Mwananchi afunga ndoa

Mdau msanifu wa gazeti la Mwananchi na Mwanaspoti (Fatuma) Elizabeth Mushi akiwa na mewe Enock Tambule baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Uvunaji haramu wa magogo


Sehemu ya shehena ya magogo ambayo yalikamatwa kutoka kwa wavuanji haramu yakiwa nje ya ofisi ya misitu wilayani Geita.

Miti mbalimbali ikionekana kuwa imevunwa na wavunaji haramu ambao baada ya kukurupushwa na Doria walikimbia na kuiacha katika Msitu wa hifadhi wa Geita wilayani Geita mkoani Mwanza.

Wilaya ya Geita ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa mkoa sasa ni miongoni mwa Wialaya zenye misitu ya hifadhi yenye jumla ya Hekta 81,922.1, lakini hekta hizo za misitu zipo katika hatari kubwa ya kutoweka kutokana na kukumbwa na uvunaji haramu ambao umekuwa ukiendelea ndani ya wilaya hiyo ya Geita.

Jitihada za kupambana na uvunaji huo haramu na mambo yanayokwamisha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.

Wednesday, May 25, 2011

Wafahamu mambo ya viadhi


Wakulima wa viazi vitamu wakazi wa kata ya Puma wilayani Singida, wakisafirisha viazi hiyo kuvipeleka kwenye kituo cha magari makubwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Zambia. Picha na Gasper Andrew.

Tuesday, May 24, 2011

maiti zatelekezwa Nyamongo



Jamani jamani hata kama maiti haina haki, hii si sawa hata kidogo, maiti zinasumbuliwa kwasababu ya kutafuta umaarufu wa kisiasa. I don't understand kwa kweli, watu wanang'ang'ana kila mmoja anavutia kwake kwanini msiihifadhi hii miili ya hawa binadamu wenzetu kisha mkaendelea na michezo yenu. Kwa hakiki hii ni hali mbaya na haikubaliki by any standards katika jamii yoyote iwe ya kitanzania na hata ili nje ya tanzania.
Hapa ndugu na jamaa wakiwa wamepigwa butwaa wasijue la kufanya baada ya maiti hao wanaonekana wakiwa wametelekezwa mitaani katika vijiji vya Bonchugu wilayani Serengeti leo hii ambako ilikutwa maiti ya Chawali Bhoke. Ni kitendo kibaya sana. Mungu atusaidie, hii hali inawasha kiberiti.

Miss Universe ziarani Mwananchi



Mhariri wa habari wa gazeti la The Citizen, Peter Nyanje akiwapa maelezo washiriki wa shindano la Miss Universe jinsi gazeti hilo linavyokusanya habari wakati washiriki hao walipotembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL), Tabata jijini Dar es Salaam jana. MCL ni moja wa wadhamini wa shindano hilo. Picha na Edwin Mjwahuzi

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...