Saturday, June 30, 2007

Uwanja mpya wa Taifa



Pichani unaweza kuona aerial view ya uwanja mpya wa taifa wa michezo wa Dar es Salaam ambao wazo lake lilichipukia toka kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na sasa unakamilika chini ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete sijui watauitaje?? Picha ya Fredrick Felix.

Uwanja mpya wa Taifa



Baadhi wa wananchi waliofika kucheki uwanja mpya kama alivyowanasa mpiga picha Fredrick Felix wa Mwananchi na Citizen.

Mambo ya Uwanja Mpya



Rais wa TFF, Leodegar Tenga akiwa na Waziri Habari, Utamaduni na Michezo Muhammed Seif Khatib wakizungumza jambo baada kukagua uwanja mpya.

Wednesday, June 27, 2007

Medy Mpakanjia



Baba na mwana Rahmani.

Buriani Amina Chifupa



Mheshimiwa Amina Chifupa hatunaye tena, kwa mujibu wa baba yake Amina, Mzee Hamis Chifupa, bintiye alikutwa na mauti saa tatu kasorobo usiku katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo alikokuwa amelazwa. Kifo chake kimepokelewa kwa hisia mbalimbali na watu wa rika tofauti nchi nzima.



Medy Mpakanjia analia.



Gari iliyobeba mwili wa Amina.



Kwaheri Amina Picha hii imepigwa na Mpoki Bukuku.

RATIBA YA MAZISHI ILIYOPATIKANA NYUMBANI KWA MZEE CHIFUPA
MIKOCHENI ENEO LA TPDC ZINASEMA...

Mazishi yatafanyika Kesho, Kijijini Kwao Luhanjo, Lupembe, Njombe Mkoani Iringa, Ngugu, jamaa na Marafiki wanaotaka kuhudhuria Mazishi hayo kutoka Dar es salaam Wanatakiwa Kutoa Mchango wa Tshs 40,000/= Ili waondoke kwa Msafara wa Pamoja! Dk. Tamba ndo Mweka hazina wa kamati ya Mazishi na ndo anapokea Michango hiyo ya tshs. 40,000/= kwa Kila mmoja kama nauli ya kwenda na Kurudi Mazishini!

Taarifa hizi kwa mujibu wa Ngowi au Michuziutapata taarifa za kina.

Mola ailaze pema Roho ya Mpendwa wetu Amina Chifupa- Amina.

Tuesday, June 26, 2007

Mambo ya Pemba hayaaa



Mambo yanaonekana hivi huku kijijini Pemba maisha yanaendele softly.

Saturday, June 23, 2007

Sio Geneva Wala nini ni Kijenge



Unaweza kuona kwa mbali majumba ya kifahali yaliyopo katika eneo la Kijenge, watu iko dolari si mchezo.

Mlima Meru uleee



Hapa ni karibu kabisa na njia panda ya kuelekea Sanawari, Arusha ndipo unapoweza kuona kwa mbaali Mlima Meru ambao ni mkubwa kiasi unapamba mandhari ya jiji la Arusha.

Palipozaliwa Azimio la Arusha



Hapa ndipo mahala lilipozaliwa Azimio la Arusha mwaka 1967

KITUO CHA KIMATAIFA CHA MIKUTANO (AICC)



Hapa ndipo yalipokuwa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa ni kituo cha mikutano na kuna Makao Makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda (ICTR), ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki na ofisi nyingine kibao.

Mnara wa Saa A Town



Hapa ni katikati ya jiji la Arusha maarufu kama A Town au wengine wanapaita Geneva ya Afrika mji sasa umechangamka ni matata kweli kweli, utalii umelifanya jiji kuwa hai.

Sky Scrapper yetu ya PPF



Hapana shaka kwamba nchi yetu sasa yasonga mbele na kupendeza baadhi ya maeneo huku mengine yakizidi kudorora zaidi na kufanana na nini sijui.

Bongo si mchezo sasa kama majuu vile



Hapa ukikata kona kidogo hapo kushoto unaingia ofisini kwa Issa Michuzi!

Watoto wa Tanzania



Watoto wa Tanzania miongoni mwao wakiwa hawa wamewekewa mkakati gani wa kuwafanya waishi katika usawa bila ubaguzi, bila matabaka kama tulivyokuwa wazazi wao. Hivi sasa mali zote zinauzwa si misitu, madini yetu yote na kila rasilimali ipo siku watoto hawa wenye taifa lao watakuja kuuliza hivi wazazi tulikuwa wapi?

Saturday, June 16, 2007

Miwaa



Wafanyabiashara wadogo wakikokota baiskeli zao zilizosheheni miwa kuelekea kuliko na wateja. Miwa ni chanzo kikubwa cha nishati mbalimbali ikiwamo ya umeme tunaitumiaje?

Mizani Chalinze


Mizani hii lengo lilikuwa zuri tu, lakini bwana mambo yaliyopo katika mzani huu na ule wa Kibaha, Himo na kisha kule mikumi shughuli yake pevu.

Safari ya Arusha



Safari za basi siku hizi bwana zinatisha, lakini hatuna njia walala hoi lazima tusafiri na usafiri wetu ni mabasi kwani hamjasikia kejeli za Waziri Andrew Chenge alipotoa maoni yake alionekana kuponda yaani anaona usafiri wa basi ni usafiri wa hovyo mno, any way hata ndege za bongo ni yale yale tu.

Njombe

Ugali

Ugali

Safari na muziki

Tuesday, June 12, 2007

Kwa mtaji huu, tunaelekea kwenye utawala wa kifalme-2

NIMELAZIMIKA kuendeleza mjadala huu kutokana na mwitikio mkubwa wa wasomaji wetu wa safu hii ya siasa. Wiki iliyopita, nilizungumzia kwa kina kuhusu namna ambavyo watoto wa maskini na au maskini wenyewe wazazi au wao walivyo na fursa ndogo ya kuweza kupata madaraka katika chama na au serikali.

Nimefurahi kwamba wapo wengi ambao walikuwa na mtazamo kama wangu, yaani wa kupinga mifumo inayowafanya nafasi watoto wa vigogo na watu wengine wenye uwezo kuwa na uwezekano mkubwa wa kunyakua madaraka ya uongozi kwa hali yoyote ile na hivyo kuwanyima fursa wale wasio nacho hata kama wana uzoefu au uwezo mkubwa.

Nimefurahi, pia kwamba wapo watu wengine wenye mitazamo inayoafiki kwamba wao ndiyo wao, ndio wateule na kwamba eti kwa sababu watoto wao wamezaliwa katika siasa, basi wataendelea kuwa wafalme wa siasa, daima dawamu hadi dunia hii inakwisha. Bonyeza hapa

Sunday, June 03, 2007

Mpango wa njia tatu Dar ufutwe, haufai



Barabara ya Morogoro.

WIKI hii tumeshuhudia utekelezwaji wa maamuzi makubwa na ya haraka haraka mno ambayo kwa upande mmoja yanaweza kuonekana kama ni ukombozi kwa watu wengine, lakini kwa upande mwingine ni kero na tatizo kubwa zaidi kwa raia wa taifa hili walioko jijini Dar es Salaam.

Hii inafuatia utekelezwaji wa amri ya Waziri Mkuu Edward Lowassa, aliyetaka kumalizwa kwa tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam na hivyo kuchukuliwa maamuzi ya haraka haraka ya kuanza kutumika kwa njia nyingine ya ziada kwa magari yanayokwenda na au kurudi mjini wakati wa asubuhi na jioni.

Sikatai kwamba ili kifanyike kitu kikubwa, ni lazima kufanya maamuzi magumu, lakini kwa mantiki ya sasa uamuzi huu mgumu hauna manufaa makubwa kuliko hasara zilizopo. hapa

Kwa mtaji huu, tunaelekea kurudi kwenye utawala wa kifalme



Mmoja wa watoto wa Vigogo akikabidhiwa fomu.

HATA kama hatutaki, basi hivi ndiyo ilivyo, pia ndivyo ilivyojengwa ikafanyiwa mikakati ya makusudi na kama haikemewi haitabadilika, tunaelekea kunako utawala wa familia, utawala wa kifalme wa baba kumwachia mwana na mwana, mke na hadi mjukuu au mkwe na mzunguko unabakia kuwa ule ule.
<>

Sasa hivi ni wakati wa mchakato wa wanachama kuomba kuteuliwa kuwa viongozi ndani ya chama tawala, kile cha Mapinduzi, CCM, hasa kwa ngazi ya ujumbe wa halmashauri kuu na hatimaye kamati kuu, ngazi ambazo ni nyeti ndani ya chama hicho.
Kutokana na mchakato huo, wiki iliyopita tumeshuhudia watoto wa vigogo, wake zao, wajukuu na hata babu zao wakifurukuta na kuchukua fomu hizo kwa nia au lengo la kubakia katika madaraka ya ngazi za juu ndani CCM. Hawa wanajidanganya kama vile kwamba baba akiwa na kipaji basi na mwana anacho. La hasha kila mtu na kipaji chake kwa maana hiyo siyo kweli kwamba kila mtoto wa kigogo ana kipawa na au uwezo wa kuongoza. Uongozi siyo inherent. Bonyeza hapa kuendelea kujipatia uhondo.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...