Wednesday, November 22, 2006

Usafiri



Wakazi wa wilaya ya Meatu, mkoani Sinyanga wakiwa safarini kuelekea kijiji cha Mwamalole kilichomo wilayani humo. Pichani wasafiri hao wanaonekana wakiwa wamelundikana katika gari moja lililosheheni baiskeli, mbao mabadi na wao kutokana na tatizo la usafiri.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Kweli bado safari ndefu tunayo!

MK said...

Alafu walio wengi wanapiga kelele kuhusu JK, Kila wakati nafungua vyombo vya habari vya Tanzania nakuta sifa nyingi tu zisizo na mpango kuhusu JK wakati uchumi ovyo, hali ya maisha kwa wananchi ni mabaya, wala rushwa na wauza unga wapo kibao ana cheka nao, Thamani ya pesa ya nchi yetu ina kwenda chini kila siku leo hii pound moja ni sawa na shilingi 2,500/= alafu yeye kila siku anachoma mafuta ya ndege na kutembea tembea ovyo na kuacha nchi na wananchi hawana umeme na masikini, wakati huo huo vyombo vya habari ndani ya nchi vina andika habari za sifa zisizo na mpango kuhusu yeye na serikali yake.

Kama kweli ni wachapa kazi waondoe shida, umasikini wa watanzania na tanzania, waondoe kero ya umeme na kero zote zinazo onekana ndani ya nchi, Na hapo hivyo vyombo ambavyo havijui nini maana ya uandishi ndio waweze kuleta hizo sifa.

Imefikia wakati kuna vyombo fulani vya habari sivitembelei kutokana na kukerwa na tabia zao.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...