Bwagamoyo

Haya ni magofu maarufu sana hapa nchini kwenye mwambao wa bahari ya Hindi kule Bwagamoyo. Inasemekana kuna baadhi ya sehemu za aina hii huko huko Bagamoyo zimeuzwa!

Comments

Ndesanjo Macha said…
Mzee, hebu kusanya picha hizi ili tutunze historia hii kabla hawa jamaa hawajauza maeneo haya. Pia picha hizi tutakuja kuzitumia baadaye kama ushahidi mahakamani katika kesi dhidi ya wale wanaochezea historia yetu kwa manufaa yao binafsi.
mwandani said…
Ni makosa kuuza au kubadilisha maeneo ya urithi wa historia!
Kuna habari za kina juu ya uuzwaji huo? hebu tuhabarishe Bwana Charahani.
mzee wa mshitu said…
Yaap Ndesanjo kitu ulichosema ni cha hakika kabisa, picha hizi ngoja tuendelee kukusanya kwa wingi ili tusije kugeukwa kama yule jamaa wa Darwin's Nightmare kibali wamempa wenyewe kazungumza ukweli kisha wanamwakia. Kwani ni uongo kwamba wananchi wanakula panki, labda hizo silaha.
Bw. Mwandani hakika ni kosa kwa wenye kuelewa lakini matajiri hawajui hilo wanataka kuvuna kisha waache nchi pabaya wajaze matumbo yao. Nakusanya taarifa hizo ntakufikishia mzee usiwe na shaka.

Jeff Msangi said…
Makosa sio kuuza tu bali pia kutoyatunza.Nasikia raisi wa nchi anatokea huko huko Bwagamoyo.Maeneo kama haya yanatakiwa kutunzwa kwa gharama zote jamani!
mloyi said…
Ndesanjo unataka makubwa sana na ya siku zijazo! Ya leo mbona huyasemi? huyafanyii kazi? Tangu utoto wangu nimeishi Darisalama, lakini bagamoyo naisikia na kuiona kwenye picha tuu! Nitawezaje kupanda mahakamani kutoa ushahidi kwamba historia yangu imehifadhiwa pale?
Changamoto, wengi zaidi tusaidiwe kufika pale tuione hiyo Historia yetu. Ndipo tutakapopata mwamko wa kuidai ihifadhiwe kwa kizazi kijacho.