BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu nchini HESLB imeamuru eti wahitimu wote walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994/95 hadi sasa, wajitokeze na kuanza kuirejesha ili iweze kutumika kuwako pesha wengine, vinginevyo itawachukulia watu hao hatua za kisheria.
Agizo au tuseme kauli hii kimsingi siipingi maana ni nia yangu kuona Watanzania wengi tunasoma katika elimu ya juu, ingawa inachekesha kidogo kwa watu wapenda nchi wanaofikiri kwa kiwango hata cha kawaida tu.
Inachekesha kwa sababu kwanza, imetolewa kivitisho kama vile ina ugomvi na wakopaji, wakati hili ni suala la kawaida kueleweshana na kukumbushana.
Hivi inakuwaje unabagua wafaidika wa fedha za umma kwa makundi, eti hawa ndiyo wanaostahili kulipa na wengine uwaache, wakati unaowaacha ndiyo pengine waliotumia fedha nyingi kuliko hawa wa kipindi hiki, na ndiyo wenye uwezo mkubwa.
Suala la kurejesha fadhila za serikali si tatizo, wala siyo kitu cha ajabu, kosa ni kubagua watu na kujiondoa, maana wakati ule wakati bunge lilipokuwa likitunga sheria, kila mhitimu aliyekuwemo na aliyeona ‘kikombe’ kinamwelekea alikwepesha na badala yake wakaweka vigezo vilivyowakwepa wote.
Vipi waliosoma kuanzia miaka iliyopita tuchukulie hapa karibu tu kuanzia mwaka 1973 hao hawakuchukua fedha ya nchi? Walisomea pesa za nani na kwanini wasirejeshe?
Cha msingi hapa kingekuwa ni kuanzisha utaratibu ambao utawabana watu wote ambao kwa namna moja au nyingine walionufaika na fedha za umma, iwe na kukopa au kusomeshwa bure.
Natambua kuwa bodi za mikopo si mfumo mpya duniani, ni mfumo wa kawaida kabisa katika nchi nyingi. Bodi kama hizi hutoa dhana ya kulipia gharama za masomo ya wanafunzi na katika mfumo wa Ukabaila, hili halina swali.
Lakini kinachofanyika katika nchi zilizoendelea mathalani Marekani ni kuunda vituo vinavyohusiana na masuala ya msaada wa kifedha katika kila chuo. Vituo hivyo hutoa taarifa kwa kila mwanafunzi anapoomba kudahiliwa na chuo hicho.
Kama anataka kuomba mkopo pia basi hupewa fomu moja kwa moja kutoka katika chuo alichoomba na kisha kuzijaza sambamba na fomu ya kuomba udahili.
Mwanafunzi anapokubaliwa kujiunga na chuo anakuta masuala yake yanayoambatana na fedha yamekamilika na kazi yake inakuwa kuingia darasani na kupambana kutafuta ujuzi.
Kuendelea kuendekeza masuala kama haya ni kutaka kusababisha maandamano na upungufu wa amani katika jamii.
Kwa mtindo huu waliotunga sheria wanaweza kujiona wajanja kwa kuwalipisha baadhi na kujikwepa wao lakini naamini ipo siku nao wataingizwa tu katika mkumbo huu.
Kitu kingine ni kama serikali inataka ufanisi basi iepukane na hatari inayoweza kutokea kama haiwi makini kubaini matatizo yanayoikabili elimu ya juu nchini na badala yake inaishia kukaba baadhi na kuacha wengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
1 comment:
Kama mambo yote yatakwenda sawa suala la kulipa madeni ya elimu linaweza kufanyika bila kelele.
Hapa nilipo ikiwa mtu atapata mshahara zaidi ya dola 35 elfu kwa mwaka, ofisi ya kodi wanakata asilimia fulani ya mapato, hivyo wakati wa kuandika tax returns lazima ulipe serikali kilicho chao.
Pili kwa wale waliosoma wakati wa elimu bure sidhani kama wanapaswa kulipa chochote. Sheria haiwahusu. Haya mambo ya IMF yalikuja baadaye.
Kisha, kwa wale wanaozama ughaibuni sijui walipe vipi.
Post a Comment