Monday, November 16, 2009

Katikati ya jiji la Dar




Eneo hili lipo katikati ya Jiji la Dar es Salaam ni karibu sana pia na maeneo muhimu ya soko kuu kabidha la bidhaa nchini, lakini hebu cheki maji yanavyotitika h

Sunday, November 15, 2009

Mo Ibrahim: Viongozi Afrika si makini




MMILIKI wa taasisi ya Mo Ibrahim amesema matatizo yote yanayoikumba nchi za bara la Afrika, ikiwemo vita, njaa na magonjwa, yanatokana na viongozi wake kutokuwa makini na kutofuata misingi ya utawala bora.
“Viongozi wetu wengi si makini na pia hawafuati misingi ya utawala bora na kutokana na haya ndio maana bara hili bado lipo nyuma kiuchumi na linasumbuliwa na matatizo ya njaa, magonjwa na vita,” alisema mmiliki huyo, Mo Ibrahim jijini Dar es Salaam juzi katika hafla maalum ya muziki ikiwa ni sehemu ya maadalizi ya mkutano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Milimani City.
Katika mkutano uliokutanisha viongozi mbalimbali kutoka nchi za bara la Afrika, pamoja na mambo mengine walijadili masuala mbalimbali yakiwemo ya mabadiliko ya hali ya hewa, kilimo na maendeleo ya nchi za Afrika.
Mo Ibrahim, ambaye ni milionea alifafanua kwamba viongozi wa nchi za Afrika ni wepesi wa kuzungumza lakini si watendaji katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya wananchi wanaowaongoza.
Alisema kutokana na hali hiyo, Afrika inaonekana ni bara masikini na lenye matatizo mengi ikiwa ni pamoja na vita, njaa na magonjwa. Imeandikwa na Sadick Mtulya.

Siku ya kisukari duniani





Baadhi ya wakzi wa jiji la Dar es Salaam, wakipimwa msukumo wa damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Kisukari duniani, yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja leo. Picha na Zacharia Osanga

Spika Sitta Mkutanoni UN Marekani

























Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa wa kudumu wa umoja wa mataifa toka Tanzania Dr. Augustine P. Mahiga mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jana. Spika yupo marekani kuhuduria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU mkutano unaofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

























Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akihudhuria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York marekani jana. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Switzand Pascale Bruderer Na Spika wa Bunge la Africa Kusini Max Sisulu.
















































Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akihudhuria kikao cha kamati ya maandalizi ya kongamano la Maspika kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na umoja wa Mabunge Duniani IPU katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York marekani jana. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Switzand Mhe. Pascale Bruderer Na kulia ni Mbunge toka wa la Viet Nam Mhe. Ngo Quang Xuan

maafa ya mafuriko


Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya mkondoa wilaya ya Kilosa mkoani wakivua nyuma ya majengo ya shule hiyo baada ya kukumbwa na mafuliko yalisababaisha wanafunzi kukosa masomo kwa siku tatu. Picha na Juma Mtanda

Kwa wale wapenda ulabu tu











Hii imetokea huko Iran ambako Pombe ni kitu haramu! hii ni operation iliyofanyika mitaani ya kuharibu vitu vyote vya aina ya kilevi ilikufanya watu wasilewe. Jamani hapom mpo?Tukio hili limechangiwa sana na imani za KIDINI!!!!!!!

Friday, November 13, 2009

Maafa ya Same katika picha







SIMANZI na vilio jana vilitawala kwenye mazishi ya watu 2O waliofariki dunia kwa kufunikwa na kifusi kilichoporomoka mlimani na kufukia nyumba zao usiku wa manane katika Kata ya Mamba Miamba, wilayani Same, Kilimajaro.
Gazeti hili lilishuhudia watu zaidi ya 1,000 waliokusanyika katika msiba huo mkubwa wakiwa wamefunikwa na simazi, huku wakilia kwa uchungu kutokana na kupoteza ndugu zao katika mkasa huo wa kutisha.
Asilimia kubwa ya watu walionyesha masikitiko yao, hasa kwa familia ambayo imepoteza watu 15 na kati ya hao wanne hawajapatikana mpaka sasa.
Wanachi hao waliiomba serikali iwasaidie kutafuta miili ya watu hao na ikiwezekana watumie kikosi cha mbwa ili kubaini mahali ilipo.
Elineema Shambi, mmoja wa ndugu wa wanafamilia 15 waliofariki dunia na ambaye alinusurika kwa vile alikuwa amekwenda mjini Moshi kwa shughuli za kibiashara, alisema kwa majonzi kwamba amepoteza mke na watoto wake wanne ambao walifukiwa na kifusi hicho.
Alisema alikwenda mjini Moshi kununua bidhaa za kuuza, na kesho yake asubuhi alipigiwa simu na kuondoka mara moja. Alieleza kuwa alipofika alikuta nyumba yake imefunikwa kabisa kiasi cha kutoonyesha kama kulikuwa na nyumba na mwili wa mkewe ulikuwa haujapatikana hivyo akasaidia kuutafuta na kuupata pamoja na miili ya watoto wake.
Alifahamisha kuwa yeye ni mmoja kati ya ndugu wa watu 15 waliofariki katika tukio hilo la kutisha.
Akisimulia juu ya maporomoko hayo, alisema, dalili za mlima huo kuporomoka zilianza kuoneka mwaka jana kwa kuwa kulikuwa na ufa, hata hivyo hakueleza kwamba ni kwa nini hawakuhama katika eneo.
Akiunga mkono maelezo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega alibainisha kuwa wananchi wa Kata ya Mamba Miamba walishaona dalili za kuporomoka kwa mlima ulioua watu 20, tangu mwaka jana, lakini hawakuchukua tahadhari.IMeandikwa na Daniel Mjema na Rehema Matowo kutokea Same.

MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...