Saturday, September 13, 2008

Waandishi wa Habari wapata ajali Wakielekea kazini Kilwa

Herry Makange (kushoto) na Athuman Hamisi.

Herry Makange akimsaidia Athumani mara baada ya kumtoa katika gari



Gari ambalo alikuwa akisafiria Athumani Hamisi, Hery Makange na Anthony Siame namba T 961 AGT baada ya kupata ajali.
Wapigapicha za Habari wa tatu wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo wamenusurika kufa katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi wakiwa njiani kelekea Kilwa katika futari maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kupitia Voda Foundation.
Wapigapicha hao ni Athumani Hamisi wa Daily News na Habarileo, Herry Makange wa DTV na Channel 10 pamoja na Anthony Siame wa New Habari Cooperation.

Halizao zinaendelea vyema isipokuwa Athumani aliyepata majeraha kichwani tumboni na mkononi baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka mara kadhaa kabla ya kutua nje ya barabada.
Athumani amesema walikuwa katika mwenzo wa kawaida na walipokaribia Kibiti sehemu ambako barabara ina changarawe juu ya lami, gari iliyumba na kuserereka na kuanguka.
Globu hii ya jamii inamuombea mpiganaji huyu apate nafuu ya haraka. Pia inatoa shukrani kwa msaada wa hali na mali ambayo Vodacom inatoa kwa majeruhi, pia asante ziende kwa Ruge Mutahaba wa Clouds FM ambaye alihakikisha gari inavutwa hadi Dar ambako imeegeshwa kituo kikuu cha kati cha polisi.
Vile vile shukrani za pakee ziwaendee pia Herry Makange aliyebaki kulinda gari na vifaa vya kazi ambavyo vyote vipo salama, na Anthony Siame ambaye hakubanduka ubavuni pa Athumani hadi anafika Muhimbili.
Picha zilipigwa na Siame, na hiyo ya hospitali ilipigwa na bernard rwebangira na pia zipo katika
mrokim.blogspot.com na issamichuzi.blogspot.com na haki-hakingowi.blogspot.com

Thursday, September 11, 2008

Watoto wanapimana nguvu


Watoto wawili walikiwa katika harakati za kuamulia ugomvi baina ya wenzao wawili katika eneo la Mkamba, wilayani
Kilombero. Picha na Jube Tranquilino

Wednesday, September 10, 2008

Seminar with Mwalimu Mwakasege from Tanzania

Pigo la kwanza kwa Makamba



Nape Nnauye aitikisa CCM


UAMUZI wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM) wa kumvua uanachama Nape Moses Nnauye, sasa unaonekana dhahiri kukitikisa chama kizima.

Mtikisiko huo umedhihirika kufuatia kauli za wazi za kutoridhishwa na kustushwa na uamuzi huo wa Baraza Kuu, ambazo zimetolewa na makada waandamizi wa chama hicho, wakiwemo Mawaziri Wakuu wawili wastaafu Cleopa David Msuya na Frederick Sumaye.

Licha ya kauli hizo za wazi za makada hao waandamizi, taarifa kutoka ndani ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, hadi jana bado ilikuwa ikitambua nafasi za Nape, ambaye ni mwana wa aliyekuwa kada mwandamizi wa CCM marehemu Brigedie Moses Nnauye.

Kauli mpya ya Katibu Mkuu Yusuph Makamba, kwamba Nape bado atabaki na nafasi zake ndani ya chama ni ishara pia kwamba, chama ikiwemo CC na NEC hazijabariki maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM.

Mtoto akatwa uume wote akitahiriwa



MTOTO Franciss Gasper, mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi
mmoja (pichani) anakojoa kwa kutumia mpira maalumu baada ya kukatwa uume wake wakati akitahiriwa kwenye zahanati inayofahamika kwajina la Olorein iliyopo Mererani mkoani Manyara.
Mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Spola Onero, 24, aliiambia Mwananchi kuwa alimpeleka mtoto wake katika hospitali hiyo Juni 15 mwaka 2008 kwa nia ya kumtahiriwa na alimkuta dakrati aliyemtaja kwa jina la Elisha Elunde na kumfahamisha kuwa anaweza
kufanya kazi hiyo.
Aliendelea kusema kuwa kabla ya hapo mwanae alikua
akisumbuliwa na maradhi (lawalawa) na kuona umuhimu wa kumtahiri ili kuondokana na maradhi hayo. Lakini baada ya kumtahiriwa mtoto huyo alilia sana na alimrejesha katika zahanati hiyo lakini daktari huyo, alimtoa wasiwasi na kumwambia kuwa uume wa motto wake utarejea taratibu.
"Nilimrudisha hospitali na nikamweleza kuwa mtoto hawezi kukojoa na daktari Elunde akanimbia kuwa nirudi nyummbani na nisimwambie mtu
mpaka mtoto atakapopona. Lakini nikaona mtoto anazidi kulia na uume
hakuna," alisema Bi. Spola kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa mara kwa mara alipomrudisha mtoto kwa
daktari huyo alimwambia kuwa anaomba iwe siri na anafanya jitihada za kumpa dawa ili uume wa mtoto urejee katika hali ya kawaida.
Naye baba mkubwa wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Ray Maseli alisema kuwa aligundua kuwa daktari huyo hakuwa na uwezo wa kumtahiri mtoto huyo baada ya kufanya uchunguzi na hivyo wakaripoti suala hilo kituo cha polisi Mererani na daktari huyo kukamatwa.
Aliongeza kuwa daktari huyo pamoja na kukamtwa aliachiwa huru
siku chache baadaye na kesi haikufunguliwa.
"Tulirejea kituo cha polisi kutoa taarifa upya na ndipo siku ya Alhamisi alikamatwa tena na kupelekwa katika kituo cha polisi kilichopo wilayani Babati. Habari na Hemed Kivuyo, Arusha.

Maamuzi mazito CCM




HATIMA ya mwanasiasa kijana, Nape Nnauye na jina la mgombea wa ubunge ya jimbo la Tarime Mjini ndio mambo yanayotarajiwa kukuna vichwa vya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) baada ya vichwa 39 vya Kamati Kuu kujadili jana hadi usiku wa manane.

Hakuna uamuzi uliotangazwa jana baada ya Kamati Kuu, chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kujadili masuala hayo, pamoja na agenda nyingine za NEC kwa vipindi viwili, cha kwanza kikianza saa 9.00 alasiri na kingine saa kikianza saa 3:00 usiku.
“Wameamua kupumzika kwa ajili ya futari na tumeambiwa kuwa watakutana tena saa 3:00 usiku kuendelea na kikao cha maandalizi ya NEC,” alisema mmoja wa wafanyakazi kwenye jengo la CCM Makao Makuu mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete aliwasili Dodoma jana mchana na aliingia kwenye chumba cha mkutano, akiwa na lundo la nyaraka, hali iliyoonyesha kuwa kikao hicho kilikuwa na shughuli kubwa ya kujadili kabla ya kuyasukumia masuala hayo moto kwenye kikao cha leo.

Tuesday, September 09, 2008

watoto jamani


Vipaji vya watoto huanza kujichomoza mapema wangali wachanga hebu cheki kama hapa hawa watoto wanaonekana kuwa na vipaji vingi, wengine hapa ni madaktari, wengine watakuwa wanasiasa na wengine ndo hivyoo maji lazima yafuate mkondo wake.

MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...