Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemtembelea na kumjulia hali, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jaji. Joseph Sinde Warioba, katika makazi yake, Mbezi Juu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, katika makazi yake yaliyopo Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo imeonesha heshima na kuthamini mchango mkubwa wa viongozi wastaafu walioitumikia nchi kwa uadilifu na uzalendo. Katika mazungumzo yao, viongozi hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Taifa na ustawi wa wananchi.
Hatua ya Makamu wa Rais kumtembelea Jaji Mstaafu Warioba imepokelewa kama ishara ya kuenzi utumishi wa viongozi walioweka msingi imara wa uongozi na utawala nchini, huku ikidhihirisha umuhimu wa kuendelea kuwajali na kuwathamini wazee wa Taifa kwa mchango wao katika kujenga Tanzania ya leo.






No comments:
Post a Comment