Thursday, November 06, 2025

RAIS SAMIA AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA URUSI IKULU CHAMWINO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Sergei Kiriyenko, Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimir Putin, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Novemba, 2025.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Urusi Mhe. Vladimir Putin uliowasilishwa kwake na Mhe. Sergei Kiriyenko, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Novemba, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Sergei Kiriyenko, Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Urusi, Mheshimiwa Vladimir Putin, leo tarehe 06 Novemba 2025, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Mhe. Dkt. Samia alipokea kwa heshima ujio wa Mhe. Kiriyenko mara alipowasili Ikulu, ambapo viongozi hao walipata nafasi ya kubadilishana mawazo na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.

Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii uliopo kati ya mataifa haya mawili, hususan katika maeneo ya uwekezaji, elimu, nishati na teknolojia.

Ziara hiyo ni ishara ya kuimarika kwa mahusiano ya kihistoria kati ya Tanzania na Urusi, huku serikali zote mbili zikiahidi kuendelea kushirikiana katika kuleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi wa nchi zao.

#IkuluChamwino #RaisSamia #TanzaniaUrusi #DiplomasiaYaMaendeleo #BuildingPartnerships #Dodoma

RAIS SAMIA AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA URUSI IKULU CHAMWINO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Sergei Kiriyenko, Mjumbe Maalum wa Rai...