Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo akipokea mifuko 200 ya Saruji kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Akiongea wakati wa kupokea msaada huo, Bw. Chongolo, pamoja na kulishukuru Shirika la Nyumba la Taifa ameuelekeza msaada huo katika ujenzi wa madarasa katika shule za Sekondari ili kupunguza pengo la madarasa 100 yanayohitajika kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari Januari Mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo (kulia) akipokea mifuko 200 ya Saruji kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni. Kutoka kushoto ni Dereva wa Shirika la Nyumba la Taifa, Jackson Bagera, Afisa Manunuzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Paskalina Monko, Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Msigwa, Yahya Charahani na Kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Afisa Huduma kwa Jamii, Yamlihery Ndullah na wa kwanza kulia ni Abeld Ngassa Joram Afisa wa NHC.
Shehena ya mifuko 200 ya Saruji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Shehena ya mifuko 200 ya Saruji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo (kulia) abaada ya kupokea mifuko ya saruji wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo (kulia) akisalimiana na Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Msigwa wakati wa hafla hiyo.
Shehena ya mifuko 200 iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni ikiingizwa ndani ya ghala la kuhifadhia.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo akisalimiana na Afisa Manunuzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Paskalina Monko.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Daniel Chongolo akisalimiana na Dereva wa Shirika la Nyumba la Taifa, Jackson Bagera.
Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) imekabidhi jumla ya mifuko ya simenti 200 kwa mkuu wa wilaya ya
Kinondoni, Godfrey Chongolo ikiwa ni mchango wake kwa jamii katika kuhakikisha
sekta ya elimu inaboreshwa.
Akiongea wakati wa
kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Chongolo, pamoja na
kulishukuru Shirika la Nyumba la Taifa ameuelekeza msaada huo katika ujenzi wa
madarasa katika shule za Sekondari ili kupunguza pengo la madarasa 100
yanayohitajika kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari
Januari Mwaka huu.
Alisema kuwa Wilaya ya
Kinondoni ilipata baraka ya kusajili watoto wengi kwaajili ya kujiunga na elimu
ya kidato cha kwanza na kwamba elimu bila malipo imehamaisha watoto wengi
kujiunga na elimu hiyo na hivyo kusababisha kuwa na upungufu wa vyumba vya
kujifunzia.
Alisema uongozi wa
wilaya kwa maana ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja
na watendaji wote kwa ujumla walichukua jukumu la kuendesha harambee
itakayowezesha kujenga angalau madarasa 100 ili kukabili upungufu wa madarasa
na yakamilike kabla ya Machi mwaka huu.
“Napenda kuwahakikishia
wadau na watoto wetu waliobahatika kujiunga na elimu ya sekondari mwaka huu kwa
wilaya ya Kinondoni kwamba, madarasa tunayoyapigia kampeni ya kuyajenga
yatakamilika Machi na watoto kuingia, pamoja na changamoto ndogo ndogo tulizo
nazo ambazo tutawaomba wadau waendelee kutuunga mkono kuzimaliza,” alisema
Chongolo.
Kwa upande wake, Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Yahya Charahani alisema kuwa Shirika limetoa vifaa hivyo ili
kuhakikisha wanafunzi hawakosi masomo na wanasomea katika mazingira mazuri.
Alisema Shirika la
Nyumba la Taifa liayo sera iliyojikita katika kusaidia vijana na kwamba sera
hiyo imeshasaidia vijana takribani 6,000 nchi nzima kwa kuwapatia mashine za
kufyatulia tofali za kufungamana kwa ajili ya kujengea nyumba na hivyo
kujiongezea kipato.
“Pamoja na sera hii ya
Shirika kujikita kuwasaidia vijana kujiajiri, pia shirika linasaidia katika
sekta za afya na majanga mbalimbali yanayojitokeza ili kuwaokoa wanaokutikana
na majanga,” alisema.
Alisema hii ni sehemu tuyta jitihada zao katika kuhakikisha sekta za elimu na afya, hasa kwa kizazi
kijacho zinahudumia wananchi katika hali ya ubora.
Alisema kuwa sekta ya
elimu ina changamoto nyingi lakini Shirika kwa kushirikiana na wananchi
watahakikisha wanazikabili kwa kutoa misaada mbalimbali iliyomo ndani ya uwezo
wao ili kuboresha mazingira ya usomaji.
No comments:
Post a Comment