Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) mkoa wa Geita, Glagys Jeffta wanaoshuhudia ni maafisa uendelezaji biashara, Clara Lumbanga, Olivia Musanga Zoka na Phoibe Keu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi Banyani leo jioni.
Eneo lililopimwa la Rubambangwe linavyoonekana kwa picha ya Drone,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mtemi Simioni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani wakijadiliana jambo jioni ya leo baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja Chato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga.
Mazungumzo yakiendelea baada ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Eliud Mwaiteleke akijadiliana jambo na na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani akizungumza kutoa neno la shukurani katika uzinduzi huo kulia kwake ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni na kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani kwa mchango wake katika upimaji wa viwanja hivyo vilivyozinduliwa mauzo.
Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
Hadhira ikifuatilia hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akizunguma katika uzinduzi huo kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Philip Shoni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani akizungumza katika hafla hiyo na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Wakifuatilia hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Injinia Msafiri Mtemi Simioni akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Maulidi
Banyani na Waziri wa Nishati na mbunge wa jimbo hilo, Dk. Medard Kalemani.
Wakiagana mara baada ya kuhitimisha hafla ya uzinduzi wa mauzo ya viwanja.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UUZAJI WA VIWANJA KATIKA ENEO LA RUBAMBANGWE
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
Halmashauri
ya Wilaya ya Chato ikishirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
inautangazia umma juu ya uuzaji wa viwanja 1,035 vilivyopimwa na kuwekewa
barabara katika eneo la Mlimani na Rubambangwe kata ya Muungano. Mauzo ya
viwanja yanaanza wiki ijayo.
Wananchi
wote mnakaribishwa kununua viwanja vyenye matumizi mbalimbali kama vile makazi,
makazi na biashara, viwanja vya biashara, maeneo ya kumpumzikia, viwanja vya
michezo na huduma mbalimbali za kijamii kama zahanati, Shule, Vituo vya Mafuta
kwa bei ya kuanzia Tsh 1,300 kwa mita ya mraba.
Viwanja
vipo mita chache kutoka katikati ya mji wa Chato. Vipo mkabala na barabara kuu
iendayo Bukoba. Pembezoni mwa Ziwa Victoria.
Viwanja
vilivyopimwa na kupangwa kwa ajili ya makazi vina ukubwa kama ifuatavyo:
1.
Ujazo wa juu (High density)
2.
Ujazo wa kati (Medium density)
3. Ujazo wa chini (Low density)
VIWANGO
VYA GHARAMA YA VIWANJA KWA MATUMIZI MBALIMBALI
1.
Makazi –Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,300/=
2.
Makazi na biashara- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 1,700/=
3.
Biashara (Hotel, Vituo vya mafuta, maduka makubwa)- Bei ya kiwanja kwa mita moja
ya mraba ni Shilingi 2,200/=
4.
Huduma za jamii (Zahanati, shule ya awali, sekondari) Bei ya kiwanja kwa mita
moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
5.
Ibada/kuabudu- Bei ya kiwanja kwa mita moja ya mraba ni Shilingi 2,200/=
UTARATIBU WA KUNUNUA KIWANJA
Chukua
fomu ya maombi kutoka ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato au Ofisi ya NHC
iliyo karibu nawe.
Lipia
angalau asilimia 30 ya thamani ya kiwanja unachonunua na kiasi kinachobaki
kilipwe ndani ya siku 90.
Malipo
yote yafanyike kwenye akaunti ya benki ifuatayo: Jina la Akaunti : MRADI WA
VIWANJA CHATO Nambari ya akaunti : 327 100 116 07 Benki: NMB Tawi la Chato
Rejesha
fomu ya maombi uliyojaza kwa usahihi ukiambatanisha pamoja na vielelezo
vinavyohitajika ikiwemo nakala ya malipo (deposit slip) kutoka benki.
Utapatiwa
barua ya uthibitisho (Offer Letter) mara tu ombi lako litakapokubaliwa, pamoja
na masharti ya kukamilisha malipo ya kiwanja unachochagua.
Kwa
maelezo zaidi tembelea ofisi za Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya
Chato.
Au
KAMBARAGE House, 1 Mtaa wa Ufukoni, Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mawasiliano
piga namba +255 282 228 007/ +255 754
444 333.
PHILIP SHONI
KWA NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
21/02/2019